Number don't lie; Viwanda 8000+ vimeajiri raia wa Tanzania?

Eng. Zezudu

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
7,811
10,815
Serikali ya awamu ya tano aka serikali ya wanyonge, wazalendo na vieite, inajinadi kujenga viwanda 8000+, Je ivi viwanda vipo au ni hewa au vilikuepo kisiasa ili kumnadi mwendazake. ?

1) Watu 818+ wenye shahada ya uhandisi umeme, mitambo (mechanical) wameitwa kwenye usahili( interview) wa Project engineer, REA (Rural enery agency). 10/04/2021.

Pamoja na serikali kuwa na miradi mingi ya maendeleo mfano SGR, bwawa la umeme JNHPP na kuwa na viwanda 8000+ ,lakini bado tatizo la ajira kwa wahitimu limebaki pale pale, ukiangalia viwanda 8000 vinauwezo wa kuajiri wa wahandisi wengii fani za uhandisi mitambo na umeme na wasitoshe. Kwa makadilio ya chini tu uki assume kila kiwanda kinauwezo wa kuajiri wahandisi mitambo 2, umeme 2,
8000x 2= 16000 , mitambo
8000x2=16000, umeme
Idadi ya vyuo vinavyotoa shahada za uhandisi mitambo na umeme Tanzania ni DIT, UDSM, MUST, St. Augustine na idadi ya wahitimu wanao maliza katika vyuo hivyo kwa mwaka hawazidi mia tano. Je hivi viwanda vipo au ni viwanda vya kusaga, kukoboa na kuassamble bidhaa na magodown makubwa ambayo yana pack bidhaa zilizotengenezwa nchi za watu.

2) Ripoti ya CAG inaonyesha watu zaidi ya 1500 walikuwa hawana vibari vya kufanya kazi Tanzania kwenye hii project ya Hydro power, Je Hawa ni raia wa nchi gani ambao wanachukua nafasi za Watanzania katika soko la ajira chini ya utawala wa kiongozi mzalendo.?

3) Katika awamu ya mwendazake zaidi ya vijana 11000 waliopata mafunzo ya JKT wamerudishwa nyumbani , ndani ya miaka hii mitano . Hapa naweza kusema mzee wetu alikuwa Hana busara na akuthamini viongozi wastafu alishindwa hata kumuuliza JK alifanikishaje suala la ajira.

Mkubali , mkatae mzee alitumia maneno haya kutukandamiza watanzania wa chini na kutupumbaza;
Mnyonge, mzalendo .

Hatuhitaji kuwa bachelor of research methodology ili kufahamu madudu ya awamu ya tano. Tulikuwa tunaelekea shimoni .

Tumshukuru Mungu kwa maamuzi sahihi katika wakati sahihi hata Kama kachelewa.

 
Kuna raia wa Tanzania na kuna raia wa CCM.
Viwanda haviko visible kwa Watanzania, ila kwa viongozi wa CCM tu.
Viwanda vimeajiri majini na si watu, ndio maana Hali Ni tete.
Pia utawala wa mwendazake ulijuwa na kauli mbinu moja tu, tuishi kama mashetani.
Hata kungekuwa na viwanda milioni kumbi, vingeajiri mashetani na si watu.
Hi ndio ilikuwa ndoto na matarajio ya mwendazake
 
Kuna raia wa Tanzania na kuna raia wa CCM.
Viwanda haviko visible kwa Watanzania, ila kwa viongozi wa CCM tu.
Viwanda vimeajiri majini na si watu, ndio maana Hali Ni tete.
Pia utawala wa mwendazake ulijuwa na kauli mbinu moja tu, tuishi kama mashetani.
Hata kungekuwa na viwanda milioni kumbi, vingeajiri mashetani na si watu.
Hi ndio ilikuwa ndoto na matarajio ya mwendazake
Tanzania inajiri mazombie, Kuna ajira million nane zinakuja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom