Nukuu za Mwalimu Nyerere | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nukuu za Mwalimu Nyerere

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kivumah, Oct 14, 2010.

 1. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2010
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,387
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Ni Eleven Years After, tangu Mwl atutoke. Wanajamvi hebu yeyote anayekumbuka nukuu yoyote alioitoa Mwalimu katika hotuba zake aiweke hapa jamvini.


  Mojawapo ni hii: '' Mtu aliyejiandikisha kupiga kura, halafu siku ya Uchaguzi haendi kupiga kura, Huyo ni Mpumbavu'' JK Nyerere
   
 2. fige

  fige JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2010
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 377
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dhambi ya ubaguzi ni mbaya sana, sawa na kula nyama ya mtu,dhambi ya ubaguzi haiishi inaendelea tu,
  leo utabagua kwa kusema sisi ni wanzanzibari hawa ni watanganyika ,
  kesho utasema sisi ni wanzanzibari hawa ni wanzanzibara.
  Lazima utaendelea utaona kuna mpemba na muunguja.......:.............utaendelea tu haiishi sawa na kula nyama ya mtu
   
 3. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,675
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  "Ukiona mtu anakwambia jambo la kipumbavu na yeye mwenyewe anajua kuwa unajua ni la kipumbavu..ukilikubali ujue amekudharau"...J.K. Nyerere.
   
 4. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,675
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  " Wakati wa utawala wa awamu ya kwanza si kwamba rushwa haikuwepo, ilikuwepo lakini tulikuwa wakali sana.. Ikithibitika mahakamani kuwa mtu ametoa au kupokea rushwa hatukumuachia hakimu nafasi ya kutoa hukumu peke yake. Tukasema atakwenda ndani kwa miaka miwili na viboko 24....kumi na viwili siku anaingia kumi na viwili siku anatoka akamuonyeshe na mkewe" JK Nyerere!
   
 5. N

  Natasha Ismail JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 490
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 60
  ..mnaingia karne ya 21 mmepanda basi la ukabila,mnaona sifa kuulizana makabila......mnataka kutambika?
   
 6. J

  JAY2da4 JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2010
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 205
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Siku chama kilipokuwa kinamuaga mzee Kawawa (alipostaafu rasmi siasa za majukwaani), katika hotuba ya shukrani alisema, pamoja na mambo mengine: ‘Naahidi nitakufa nikiwa mwanachama mwaminifu wa CCM.'

  Ilipofika zamu ya Mwalimu Nyerere kuzungumza, akasema: ‘Rashid una roho ngumu. Utakufa mwanachama mwaminifu wa CCM? Mimi siwezi kuyasema haya. CCM inaweza kubadilika. Siku ikiacha misingi, nami naachana nayo, kwa sababu CCM si mama yangu. Ninaye mama mmoja na siwezi kupata mwingine...'
   
 7. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,675
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  " Nchi yetu inaongozwa kwa sheria...Hatuwezi kuchagua kiongozi asiyeheshimu sheria akawa anaongoza nchi kwa kushauriwa na mkewe, maana hamjui kesho akiamka atamshauri nini??" JKN
   
 8. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,560
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Njia pekee ya kumsaidia masikini ni kumwelimisha mtoto wake". Jk Nyerere
   
 9. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,561
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  akuna vyama vya upinani vyenye uwezo wa kuingoa ccm madarakani upinzani wa kweli utatoka ccm wenyewe kwa wenyewe wtatofautiana kisha waanzisha chama chao
   
 10. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Nyerere alikuwa mu-wazi sana na hata ikafikia akaongelea kuhusu CCM kuwa hicho chama kwa sasa kina '‘kansa ya Uongozi ambapo isipotibiwa itakiua chama kizima" na akathubutu hata kusema anatamani kuona chama kingine cha upinzani kitakachoweza kukiondoa madarakani,ila akasema hadi sasa bado hajaona chama kingine na kwa hiyo pamoja na kansa ya uongozi wa CCM watu wataendelea kukichagua,au watu wanaweza wakachoka na kusema potelea mbali wakachagua chama chochote ilimradi tu watokane na kansa ya uongozi wa CCM.
  Wosia wa Baba wa Taifa.

  Ole wako Tanzania ;
  Tusipoisaidia!
  Niwezalo Nimefanya,
  kushauri na kuonya,

  Nimeonya Tahadhali,
  Nimetoa ushauri,
  Nimeshatoka kitini,
  Zaidi nifanye nini?

  Namlilia Jalia
  Atumlikie njia
  Tanzania ailinde
  waovu wasiivunje

  Nasi tumsaidie
  Yote tusiya mwachie
  Amina tena Amina
  Amina Tena na Tena.
  :dance:
   
 11. evansGREATDeal

  evansGREATDeal JF-Expert Member

  #11
  Apr 4, 2016
  Joined: Jan 4, 2016
  Messages: 2,613
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
  duh
   
 12. G

  Gerald Simon New Member

  #12
  Apr 30, 2016
  Joined: Mar 22, 2016
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Nakwambia UTII ukizidi unakuwa UOGA na Mara zote uoga huzaa unafiki na kujipendekeza. Sasa ninyi watumishi wa umma kwa wingi wenu kama mmeshindwa kupiga kura kuondoa viongozi dhalimu, bora mfe tu.
   
Loading...