Nukuu za Dkt Bashiru Katibu Mkuu CCM Taifa mkoani Lindi

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
NUKUU ZA DK. BASHIRU ALLY KATIBU MKUU CCM AKIZUNGUMZA NA WAJUMBE WA MASHINA LINDI WILAYANI KILWA.

11 Oktoba, 2019

01. "Katika kuazimisha miaka 20 ya kifo cha Mwl. Nyerere, Kuna jambo kubwa ambalo Mwl. amelifanya na wengi hawalisemi wanaishia kwenye ukarimu wake tu, kwa kuwa kulisema lile linahitaji ujasiri na uwendawazimu, hivyo tunahitaji majasiri wengi zaidi wa kulisemea Azimio la Arusha lililoweka bayana sifa za kuwa kiongozi kwenye nchi ya kijamaa kama hii".

02. "Kuna haja ya kiongozi kulinganisha maneno na vitendo, na maneno mengi kwenye Azimio la Arusha wameshindwa kuyabadilisha kwenye matendo. Tumepuuzwa vya kutosha, tumenyonywa vya kutosha sasa tunahitaji vitendo ili tukomeshe unyonyaji huo wa muda mrefu".

03. "Kwenye zao la korosho kumekuwa na wanyonyaji wengi, wanaoishi mjini na wanakuja msimu wa korosho wanawanyonya kwa ulanguzi na hawawekezi hapa Lindi, hivyo hivyo kwenye Pamba, kahawa, tumbaku n.k lolote linalomuhusu mkulima ni la kunyonya, katika uongozi huu wa Rais John Pombe Magufuli hilo hatutalikubali na tunalisimamia wakati wote".

04. "Katika vita yoyote ya kukabiliana na unyonaji, ili kushinda ni lazima tushikamane, na pia ni lazima tuwe karibu na wanawake, kwa kuwa ukizungumzia umasikini wanauelewa kwa vitendo, ukizungumzia ugumu wa upatikanaji wa mavazi kwa watoto wao wanajua, ukizungumzia unyanyasaji wanajua, hawa tukiwaweka nyuma hatutashinda na walaghai wamelijua hilo, wanaanza kujiweka karibu nao kwa mbinu nyingi, UWT na wabunge wanawake kaeni karibu na wanawake hawa wauza mbogamboga, mama ntilie, wauza samaki n.k acheni kupoteza muda kupanga safu, kupanga safu ni shirki kwa kuwa ni jambo la ramli."

05. "Kama tunawapenda wanawake tupende nao wote tunavyovipenda sisi, ni haki yao ndio maana tumeamua hatuuzi fomu za kugombea, na waliojaribu kuuza walizitapika, wakina mama hawana hela za kununua fomu ila wanasifa za uongozi, na pia acheni kuhongana, wakina mama hawana fedha za kuhonga, ila miongoni mwenu wapo wanaweza kuongoza."

06. "Wapo wanawake wanaobaguliwa na kutishwa wanapotaka kugombea nafasi za uongozi, hilo kwenye chama chetu tunalikemea na tunawataka wanawake wengi wenye sifa wagombee nafasi za uongozi kwa sababu CCM inaamini katika usawa wa binadamu."

07. "Mwezi Novemba mwaka huu, tutakuwa na uchaguzi wa serikali za mitaa, ninawasihi tuchague viongozi wenye sifa za uongozi zinazofanana na Rais na Mwenyekiti wa CCM Ndg. John Pombe Magufuli za uchapakazi na uwajibikaji wa haki."

08. "Mapambano yoyote ya kulinda haki za watu, yanahitaji nguvukazi, ubunifu na mshikamano, hivyo ni lazima tushirikiane vema na vijana wetu kwa kuwapa malezi bora ya kuwakinga na biashara za magendo, ulevi na ulaghai, bila ya hivyo, tutakuwa na vijana walanguzi wa siasa na wapiga debe wa wagombea saba na wote wanaahidiwa ushindi na kijana mmoja. Vijana ni lazima walelewe na tuwahusishe kwenye shughuli za maendeleo."

Imetolewa na;
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
MAKAO MAKUU DODOMA.
 
Back
Top Bottom