Nukuu ya Raia Mwema na Ujambazi wa watendaji wetu


NewDawnTz

NewDawnTz

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2010
Messages
1,675
Likes
6
Points
0
NewDawnTz

NewDawnTz

JF-Expert Member
Joined Nov 15, 2010
1,675 6 0
Kwenye gazeti la Raia Mwema toleo la Jumatano Dec 8 - Dec 14 kuna nukuu moja kwenye ukurasa wa 3 makala ya "Njama za Mafisadi Kuimaliza Tanesco" ambayo ningependa tuijadili na kuona hatma ya watendaji wetu na nchi yetu. Hapa sikusudii kuwalaumu WATAWALA WETU, bali watendaji wetu ndani ya Tanesco na wale wa aina yao

Mwandishi (Waandishi) wa makala hii wameandika hivi, nanukuu :-
“Taarifa za ndani za Tanesco zinasema inakusudia kukata rufaa kupinga hukumu inayowataka kuilipa kampuni ya Dowans fidia ya mabilioni ya fedha na kwamba kama ikibidi mengi ambayo hadi sasa ni siri yataibuliwa ili kuweka picha halisi kweupe na kuzuia hatua hizo za fidia”​
Kama ningekuwa mwandishi wa makala hii ningeacha kujadili mengine yote na ningejikita zaidi kuhoji na kujadili hicho kipande ambacho nimeweka blue na italic. Hii ni kwa sababu uko utata mkubwa sana uliojificha katika nukuu hiyo hapo juu


Kipengele hiki kinaonesha wazi ya kuwa, watendaji ndani ya Tanesco wanaujua mchezo wote mchafu unaochezwa katika deal hili.Moja, utata mkuu ni nani mlipwaji wa fedha hizi? Maana wote wanaotajwa wanakimbia kuwa wamiliki halali wa kampuni ya Dowans. Tanesco mkishindwa mtamlipa nani?? Na sasa hivi mnatakiwa kumlipa nani??

Mbili, Kama hajulikani mlipwaji, je ni nani aliepeleka kesi hii?? Na huyu aliepeka kesi kama sie mmiliki basi itakuwa katumwa kupeleka kesi hii, je na yeyé hamjui alimtuma apeleke kesi hii?? Na kama aliemtuma apeleke kesi pia sio mmiliki, je huyo aliemtuma hamjui mmiliki halisi wa kampuni hii??

Tatu, Taneso wanaposema wakishindwa rufaa watafichua yote yaliyofichika hawaoni wanatutania watanzania?? Je watafichua kwa nani?? Na ni kwa nini wangoje mpaka washindwe rufaa??

Nne, kama Tanesco wanaujua ukweli wote, walikuwa wapi siku zote mpaka kesi inapelekwa mahamani na kuamriwa kuilipa Dowans? Je, TANESCO HAMUONI KUWA TUTAWAONA MAJUHA kwa kitendo chenu ambacho mnajidai nacho kuwa ni cha kishujaa??

Kwa utata huu ni wazi kabisa ya kuwa Tanesco na baadhi ya wahuni fulani nvhi hii wana mchezo wanaocheza na akili za Watanzania.


Je watu wa Raia Mwema mnaweza kutusaidia kwenda mbele zaidi ya hapa kwa kutupatia usiri ulioficha ambao Tanesco (ama wahusika ndani ya Tanesco wanasema watautoa baada ya kushindwa kesi)???

Kinyume na hapa tutakuwa tukiendelea kulinda majambazi huku tukijidai na kauli mbiu yetu ya Miaka 49 ya Uhuru “TUDUMISHE UZALENDO”

Ni bora mseme leo maana huenda kesho tusiwaelewe hasa kwa kuzingatia mnatuweka kwenye mgao usio wa lazima huku mkiwa mnawaficha majambazi wa utajiri wetu. TUTAWAHUKUMU SIKU MOJA

Najua watu wa Raia Mwema na Tanesco mnapita humu, sikilizeni na kutendea maoni yetu.

SISI NDIO WENYE NCHI
 

Forum statistics

Threads 1,238,335
Members 475,888
Posts 29,316,487