Al Zagawi
JF-Expert Member
- Mar 17, 2009
- 2,461
- 1,446
i. Katika Siasa
- ......Katika zama zetu hizi za hadaa, muonekano ndio ukweli na wanaofanya mambo yanayoendana na mantiki na wakaruhusiwa kuendelea kuwa katika nafasi zao ni wachache. Rahisi imekuwa ndiyo sarafu, miigizo imechukua nafasi ya halisi na bazazi sasa ni Imam!....Jenerali Ulimwengu, Raia Mwema, Nov 11-Nov 17,2009
- Elimu ilipokuwa haijulikani duniani mvi zilihesabiwa kuwa alama ya hekima. Fikira hii ilikuwa njema sana, lakini wakati wake umepita wala haurudi tena. Sasa kama mtu hakuelimishwa, mvi zake hazihesabiwi kuwa dalili ya hekima. Jambo lisilobadilika ni kuwa kila mzee anastahili heshima ya kila kijana siku zote.....Kusadikika, Shaaban Robert
- Jibu likisadifu swali, shaka huondoka.......Kusadikika, Shaaban Robert
- .....Sasa alitamani Peterson atokee, amshukuru tena, shukrani halisi,toka katika uvungu wa moyo wake, si kwa ajili ya kumpa tunu hizo za zenye thamani tu, hasa kwa kuwa yeye alikuwa binadamu wa kwanza ambaye alionyesha kila dalili ya kumtamani, kumpenda na kumthamini kama binadamu halisi....Dar Es Salaam usiku, Ben R. Mtobwa