Mwandwanga
JF-Expert Member
- Dec 2, 2011
- 3,059
- 1,569
WanaBodi Wasalaam,
Zifuatazo ni baadhi ya nukuu za Hayati Mwl. J. K. Nyerere unaweza zisoma na kuweka komenti kwenye nukuu moja wapo ukihusianisha na Tanzania ya leo.
"Amini nawaambieni enyi Waswahili wachache mnaotawala; mnategemea kweli kuwa mtawaongoza Watanzania kwa lazima wakati wamepoteza matumaini, na mtegemee kuwa watasalia wamekaa kimya kwa amani na utulivu?
Amani ni zao la matumaini, pindi matumaini yatakapotoweka kutakuwa na vurugu katika jamii.
Nitashangaa kama hawa Watanzania watakataa kuasi. Kwanini wasiasi?
Wakati wengi wa wananchi wanapopoteza matumaini unajenga volcano. Volcano hii italipuka siku moja. Labda kama watu hawa ni wajinga.
Wengi katika watu wa nchi zetu ni wajinga ndiyo maana hukubali kutawaliwa hivyo.
Kukubali kukandamizwa namna hiyo wakati wanayo nguvu inayotokana na wingi wao, ni kwa sababu ni wajinga tu.
Hivyo basi Watanzania watakuwa ni wajinga na mataahira (idiots), kama watakubali kuendelea kukandamizwa na watu wachache (viongozi) katika nchi yao wenyewe.
Ni ukweli usiopingika kuwa masuala ya maendeleo ni masuala halisi na hayawezi kuwa masuala ya ubabaishaji tu.
Na hakutakuwa na watu wa kizazi hiki na karne hii ambao watatakiwa kujitoa muhanga kwa ajili ya maisha bora katika siku zijazo wakakubali, wakati wanawaona watu wachache wakiendelea kuneemeka machoni pao bila kujali wakati ujao, wakati wao (wananchi) na watoto wao wakiendelea kuishi katika maisha duni na dhalili.
Nukuu hizi zimo katika kitabu kinachoitwa 'Reflections On Leadership in Africa' VUB University Press, 2000.
Karibuni