Nukuu mbalimbali toka kwenye kitabu "Eat That Frog"

Innocent Kirumbuyo

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
4,640
4,426
Kila mwanzo wa chapter ya kitabu hiki kuna nukuu kutoka kwa watu mashuhuri. Mi binafsi ninazipenda sana, zimebeba maarifa muhimu sana. Nukuu hizi ni Kama;

#"The first request for success is the ability to apply physical and mental energies to one problem incessantly without growing weary".- Thomas Edison.

Sharti mojawapo la kupata mafanikio ni kuwa na uwezo wa kuelekeza nguvu zako zote za kimwili na akili katika tatizo moja na kukabiliana nalo bila kukata tamaa hadi uone matokeo.

#"Persons with comparatively moderate powers will accomplish much, if they apply themselves wholly and indefatigably to one thing at a time."- Samuel Smiles

Watu wenye uwezo au nguvu za kadiri wanaweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa sana endapo watajitoa kwa dhati na kuzielekeza nguvu zao zote katika jambo moja baada ya jingine. Siyo kufanya mambo mengi kwa wakati huo huo mmoja.

#"The only certain means of success is to render more and better service than is expected of you, no matter what your task may be"- Og Mandino.

Njia moja ya uhakika ya kufanikiwa ni kutoa huduma iliyo bora kuliko matarajio ya wahitaji au wateja wako, na hii haijarishi unafanya kazi gani.

#"The first law of success is concentration, to bend all the energies to one point, and go directly to that point, looking neither to the right nor the left."- William Mathews.

Kanuni ya kwanza ya mafanikio ni kushughulika na kitu kimoja, kuelekeza nguvu zako zote eneo hilo, hakuna kupepesa macho huku wala kule. Ukilianza jambo nguvu zote zielekee hapo hadi likamilike.

#"Do what you can, with what you have, where you are" Theodore Rousevelt.

Fanya unaloweza, tumia kile ulichonacho mkononi kwa sasa mahali popote ulipo.

#"Do not wait; the time will never be 'just right.' Start where you stand, and work with whatever tools you may have at your command, and better tools will be found as you go along." - Napoleon Hill

Usisubiri wakati ufaao kuanza kulifanya jambo lako, huo wakati mzuri unaousubiri mara nyingi huwa hauji. Anzia hapo hapo ulipo na tumia zana au vifaa vyovyote ulivyonavyo mkononi kwa sasa, zana nzuri utazipata mbele ya safari we anza tu.

Kama unatamani kuanza huu mwaka , kwa kutimiza malengo yako vizuri basi utaposoma kitabu hiki nakuhakikishia lazima malengo yako yatimia pale ukiweza kusoma hiki kitabu na kufata kanuni zake

NITAKUPATIA BURE: kwa lugha ya kingereza na kama unataka kwa lugha ya kiswahili ninachopi nitakupatia pia kwa garama 10000 tu.​

elitebookstore_20200817_175451_0.jpg
 
Back
Top Bottom