Nukuu 25 za Shaaban Robert kutoka katika riwaya ya kusadikika.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,297
NUKUU ISHIRINI NA TANO ZA SHAABAN ROBERT KUTOKA KATIKA RIWAYA YA KUSADIKIKA.

1. "Kipawa chochote cha mtu kama hakikuongozwa vyema huweza kuwa hatari au maangamizi kwa wengine".
2. " Mchwa akikaribia kuangamizwa hufanywa kuwa kumbikumbi na huoteshwa mabawa mawili".
3. "Msiba wa kujitakia hauna kilio".
4. " Msema kweli hukimbiwa na marafiki zake".
5. "Hekima ni kitu adimu kupatikana".
6. "Elimu ilipokuwa haijulikani duniani,mvi zilihesabika kuwa alama ya hekima jambo lisilobadilika ni kuwa kila mzee anastahili heshima ya kila kijana siku zote".
7. "Uvumilivu ukitumiwa siku sita ni sawa na saa sita".
8. " Ulimi wa adabu ambao ni azali ya utu wema".
9. "Kila msafiri ni ndugu wa wasafiri wengine".
10. " Kama nchi ina mazao namna gani lakini haina njia ya kuyapeleka mazao yake katika soko kubwa,faida haipatikani hata kidogo".
11."Kilimo ni uti wa mgongo wa maisha ya mwanadamu,bila ya kilimo maisha hayawezi kudumu".
12. "Udongo usipohifadhiwa hupotelewa na rutuba yake".
13. " Ushujaa ni husuni kubwa na hazina ya kudumishwa".
14. "Watu wanaoteswa ndio wanaojua kabisa mateso makubwa".
15. "Mwenye nguvu yenye mipaka,hadhulumu wala yeye hadhulumiwi".
16. "Ni haramu muheshimiwa kuwavunjia wengine heshima zao".
17. "Hakuna Uhuru wa matendo maovu".
18. "Waovu wachache hawawashindi wema wengi".
19. " Hakuna sikio ngumu duniani lisilo sikia vinywa vingi vikisema kwa umoja".
20. "Mtu yeyote anaekabili mashaka bila ya kutetemeka,hata kama hadiriki kuyashinda kama atakavyo,huishi maisha mema,mtu yeyote anaekabili mashaka akayashinda nusu,huishi maisha mema,na anaeyakabili mpaka akayashinda yote,huishi maisha bora kabisa".
21. "Watu watumiao Mali zao kwa uangalifu,huyaepa maanguko ya umasikini".
22. "Mtu yeyote asiyetunza pato lake dogo,hawezi kuwa tajiri".
23. "Matendo makubwa huchukua wakati mwingi kukamilika,kwa hivi haifai kuchelewa kila dakika moja,na kila nukta moja ni hazina".
24. "Ukitaka biashara ya vitabu isitawi,watu hawana budi kufunzwa kusoma"
25. " Hasira isiyo sikiliza hoja,huandamwa na kisasi kisicho kwisha".

MUAANDAAJI- Idd Ninga
Tengeru,Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Mungu na amrehemu,
Shaaban alikuwa mkarimu,
Mwerevu mwenye fahamu,
Hekima na akili timamu,
Kinywa chenye maneno matamu

"Waovu wachache hawa washindi wema wengi" Sheikh Shaaban Robert
 
Kati ya taswira zionekanazo anazotumia Mathias Mnyampala liko kundi la zile za harakaharaka ambazo mshairi kaziunda ndani ya tamathali za usemi. Taswira hizi znajitokeza katika lugha inayohusianisha vitu, mambo, mawazo, au hata watu mbalimbali. Kwa mfano, ubeti wa pili wa shairi la "Kifo cha Bwana Robert" (uk. 151) unasems:



Ni hasara kwa nchi nzima, ninayosema kwa dhati,
Ni kama taa kuzima, usiku wa katikati,
Kiswahili tainama, kwa kukosa kalafati,
Kifo cha Bwana Robert, hasara kwa Kiswahili.
 
Mkasikilize na album ya Mzimu wa shaban Robert. Mtunzi Nash mc
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom