Nuh Mziwanda: Shilole ni mcheza shoo tu, sio mwanamuziki yule

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
xnuhu.jpg.pagespeed.ic.4ckpmD_Wuy.jpg


Msanii wa muziki, Nuh Mziwanda ameendelea kumponda aliyekuwa mpenzi wake, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ kwa kudai sio mwanamuziki bali ni mcheza shoo.

Muimbaji huyo wa wimbo ‘Jike Shupa’ amekuwa akitupiana maneno na Shilole kupitia mitandao ya kijamii toka wimbo huyo utoke.

Akiongea katika kipindi cha The Base kinachoruka katika runinga ya ITV, Nuh alisema hawezi shindana na Shilole kwa kuwa sio mwanamuziki.

“Mimi sitaki kiki, mimi mambo ya kiki nimeshayaacha, sasa hivi na fans base kwa ajili ya Jike Shupa,” alisema Nuh. “Ila yeye (Shilole) anajaribu kunichokonoa ili maisha yake yaende. Mimi ni mwanamuziki babu, siwezi kushindana naye, yule ni mcheza shoo,”

Shilole na Nuh hawakuachana vizuri, kila mmoja amekuwa akimtupia maneno machafu mwenzake.

Wakati huo huo Shilole ameonesha masikitiko yake kufuatia madai ya kudhalilishwa na baadhi ya wasanii wenzake kwa kuipa promo video ya wimbo mpya wa Nuh Mziwanda wa Jike Shupa.

Kwa mujibu wa Shilole, video ya wimbo huo inaonesha matukio ya kumdhalilisha ambayo inaonekana yeye alikuwa akimfanyia Nuh enzi za uhusiano wao kama vile kumpiga na kumzodoa, mambo ambayo hakuwahi kuyafanya.

“Nimesikitishwa sana na kitendo cha baadhi ya wasanii wenzangu kuiposti video hiyo kwenye mitandao mbalimbali, huko ni kunidhalilisha kwa sababu jamii ikiangalia inaweza kunitafsiri tofauti,” alisema Shilole.

Katika video hiyo, msichana anayefanana na Shilole aitwaye Zuwena aliyetumika kama video queen anaonekana akimfanyia vitimbi Nuh huku akitafsiriwa kuwa, ndivyo Shilole alivyokuwa akimfanyia jamaa huyo.
 
Nuhu analazimisha bifu ili awe juu,mi namshauri Shilole asimjibu wala asimuongelee kabisa.
 
Kulikuwa na yule mwanamuziki wa kuitwa Mau Santiago, Ni mwimbaji mzuri sana. Yuko wapi siku hizi?
 
Mimi na my X wangu ukitukuta utashangaa sana, tunapiga story sana na mambo mengi sana tunashauriana, Lakini Kila mmoja yuko na Maisha yake na mtu wake
 
Hivi Nuh naye ni mwanaume wa Dar? Nimemkubali sana kwa ngoma yake ila nauliza tu!
 
unaweza ukawa umetekwa alafu haujui kama umetekwa. yaani hauna minyororo wala kamba zilizokufunga lakini hauko huru.
sasa tunaanza kugundua kuwa dogo nuhu kumbe anakipaji cha kuimba.
 
Hicho nacho kinatudhihirishia kweli hakina nguvu za kupambana na shilole sasa ndo kinaamua kupiga makelele weee ili kipewe sapoti kijinga kweli yaani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom