Ntawezaje kuanza kutoka sifuri hadi mafanikio?

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Feb 18, 2010
4,066
4,085
Sina kazi wala biashara, pesa pekee niliyo nayo ni sh. 300,000/=.
Nina shamba ambalo sijaliendeleza, naombeni mawazo yenu waungwana.
 
mafaniko sio jambo la siku moja. Maadamu una akili timamu, nguvu, ari na ardhi, basi weka jitihada zako zote kwenye namna ya kuliendeleza shamba lako.
Kwa sh.laki tatu unaweza kuanza ka kujinga hata mabanda ya miti na tope, ukaweka kuku wa kienyeji, na kwakuwa huu ni msimu wa masika kuna maji mengi, lima shambani mwako mboga za majani na miche ya matunda yanayozaa haraka. Mboga za majani ukiuza zitakupatia pesa ya kujikimu kwa siku. Pia jaribu kuweka akiba hata kama unapata hela ndogo.
 
Kwa mtaji huo anzisha biashara ya vocha kwanza...

Hili nalo ni wazo zuri sana kwa short term plan. Ila ni lazima uifanye biashara hii mahali penye watu wengi. Maana ukiifanyia sehemu ambayo haiko bize mzunguko wake utakuwa mdogo, hivyo basi hutoiona faida yake
 
Mengi awataka vijana wajiamini

Vijana wametakiwa kujiamini na kutumia fursa mbalimbali kuonyesha vipaji vyao ili kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha.
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na wanafunzi 29 kutoka shule mbalimbali za sekondari wanaoshiriki mchakato wa kujiunga na chuo cha kimataifa cha uongozi (ALA), kilichopo Afrika Kusini.
Mengi alisema vijana wanapaswa kuwa na kiu ya kufanikiwa kuliko hata watu wanaowaona kama ndio mfano wa kuigwa.
"Kujiamini na ujasiri ndiyo nguzo muhimu, unapoamini kwamba huwezi kufanya jambo fulani unashindwa kwa sababu akili yako inakujengea mazingira ya kuamini kwamba huwezi…lakini ukiamini unaweza kufanya kitu, akili yako inakuwezesha kufanikisha lile unaloamini, epuka kabisa hofu maana ndiyo adui wa mafanikio," alisema.
Mengi alisema watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwa kuhofia kufanya maamuzi "na ukisharuhusu hofu unajitengenezea sababu nyingi…unajiona labda mimi ni mdogo, maskini au mzee na hatimaye unashindwa kufanya maamuzi,"alisema
Aliwakumbusha vijana hao kuwa kipaji cha uongozi huonekana mapema tangu utoto na kwamba ili kufanikisha ni kuendeleza ndoto hiyo kwa kuwa na dira na mtazamo chanya.
Alisema kiongozi hapaswi kuona matatizo isipokuwa anatakiwa kuyatazama kama changamoto anazoweza kuzitatua.
Aliongeza kuwa vijana wanatakiwa kuwa na macho yanayoweza kuona fursa mbalimbali na kuzitumia kujiletea maendeleo.
Akitoa neno la shukrani, Mkurugenzi wa ALA, Annelene Fisher, alisema lengo la chuo hicho ni kutafuta wanafunzi kutoka nchi mbalimbali za Afrika na kuwaandaa kuwa viongozi bora wa bara hili.
"Tunataka kukuza akina Nelson Mandela, Ellen Johnson Sirleaf na Bill Gates wa Kiafrika," alisema Fisher.
Julius Shirima ambaye alihitimu ALA mwaka jana, alisema elimu ya Tanzania bado inakabiliwa na changamoto kubwa kwa kuwa mfumo wa kusoma unaelekeza zaidi kukariri kwa ajili ya mitihani badala ya kujiandaa kimaisha.
CHANZO: NIPASHE :: IPPMEDIA
 

Attachments

  • success book.pdf
    421.8 KB · Views: 324
  • If You Want To Be Rich.pdf
    573.1 KB · Views: 229
Ntawezaje kuanza kutoka sifuri hadi mafanikio?

Mkuu hesbu soma hivi vitabu kwanza.naamini utapata mwelekeo mpya.
 
Hivi vitabu sijavisoma ila nahisi vitakuwa vizuri,vp naruhusiwa kuweka kwenye blog yangu?.
 
Miundo mbinu asante sana kwa vitabu hivyo;
Nitahakikisha nasoma mpaka mwisho na kitu muhimu ni kuvifanyia kazi.
asante
 
Hi Miundombinu, Asante sana kwa vitabu hivi ni material tosha ya kumfanya mtu kutoka hatua moja kwenda nyingine.

Mungu akubariki.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom