Ntapata wapi kitabu hiki tulichoambiwa tusome na mkurugenzi wa mashtaka (DPP)?

pombe kali

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
221
431
Siku kadhaa zilizopita, tulisoma kwenye vyanzo mbali mbali vya habari kuhusu kutokuonekana kwa wakili wa serikali ndugu Maneno Mbunda, ambapo kila mmoja alisema lake, kisha mkurugenzi wa mashtaka aliitisha press na kuuambia umma kuwa wakili yule hakupotea bali alikuwa anashikiliwa na polisi pamoja na watumishi wengine kwa makosa mbali mbali.
Aliongea mengi pia alitutaka tukasome kitabu kiitwacho "licence to kill" mwenyewe alisema ni kitabu kinachoelezea jinsi watu wanavyotekwa, kupotezwa na kuuawa, mwenye kujua jinsi naweza kupata kitabu hicho ambapo mwandishi ni David Fraser tafadhali naomba tuwasiliane.
 
Back
Top Bottom