NSSF yazidi kuumbuka: Ufisadi wa ujenzi wa Hoteli Mwanza, jengo la biashara Mzizima

The Tomorrow People

JF-Expert Member
Jul 11, 2013
2,674
2,801
Kwa kashfa hizi, watetezi wa Dr Dau washaumbuka, maana tuliambiwa hakuna mtu wa kuziba pengo lake, kumbe siri ni upigaji deal tuuu.

=> Ujenzi wa hoteli Mwanza, kampuni mbili zapewa mabilioni kwa kazi zile zile

=> Mkandarasi wa ujenzi wa jengo la Biashara la Mzizima azidishiwa malipo.

=> Ujenzi wa hoteli ya kitalii Mwanza, wakandarasi walizidishiwa zaidi ya Bilioni 16 sawa na asilimia 23 ya mradi wote bila sababu za msingi.

=> Kuhusu ujenzi wa jengo la biashara Mzizima Tower ni kwamba kampuni tatu ziliomba mradi huo ambazo ni Atlas, Ginde na Jandu ambayo ilishinda.

Wataki wa kuwasilisha maombi ya zabuni ya Jandu ilikuwa sh. 8,346,155,654 lakini kamati ya Tathmini iliketi na kupitia upya mkataba na kubaini makosa hivyo ilirekebisha zabuni hiyo isomeke 8,340,700,710.94 pamoja na ongezeko la Thamani (VAT). Jandu aliridhia marekebisho hayo.

Pamoja na marekebisho hayo, mkataba waliosainiana kati ya NSSF na Jandu ulikuwa wa kiwango kile kile kilichokosewa cha sh. 8,346,155,654 chenye ziada ya sh. 5,454,943.

bcf1b0e04b93ced39f4d744dfd170f1c.jpg
 
Ndo maana jamaa alikuwa na genge lake la kumtetea kwenye mitandao kwa kutumia kigezo chu udini udini, magufuli hayo majipu yanyooshe ndo wakati wake huu kabla hata ya wabunge hawajayajadili, alikuwa anatumia kigezo cha dini yake imlinde sasa muislamu mwenzake profesa asad anamuumbua kwa kusema ukweli kwa data. Mungu ibariki Tanzania.
 
Alhaji Ramadhani kitwana Dau kitanzini hhahahahaah mwisho wa ubaya aibu kaanikwa madudu na muislam mwenzie,kwanin mbona waislam wengi tu kina Assad hawana lawama ?(they are clean i guess )ila sheikhDau ukonga panamhusu
 
Atapangiwa kazi nyingine kweli kwa uozo huu ulioibuka maskini Dr Dau kumbe ndio maana watu walidhani yeye ni mwanya sio pengo tena pale NSSF
 
"Hizi fedha za NSSF sio za Umma" ( tamka hayo in JK voice)
Mnazoza sana.
Kwani hujaona wapuuzi kadhaa kwenye ile thread ya kulipia daraja la Kigamboni kwa watumiaji wanasema eti pesa zilizolijenga sio za umma! Tanzania ni ngumu kutawaliwa lakini Watanzania tu wagumu zaidi na ndio maana tunaweza kukaa miaka zaidi ya kumi bila uongozi huku tukichekelea!
Hebu angalia Mh. Mnyika alipotanabaisha bungeni tuwa tumefikishwa hapa kwa sababu ya udhaifu wa mtu fulani waliomfukuza bungeni ndio hao hao eti wanasema #hapakazitu.
 
Kwa ufisadi huu wa Dau hata Chenge ni mtakatifu....
Kumbe tngelianza kuifanyia kazi kauli ya vijisent tangu alipoisema tungelikuwa tumeshamuelewa alichomanisha.
Hebu angalia dili la escrow yeye alikuwa na 1.6b lakini kuna watu wasiojulikana wana zaidi ya 250b, dili la rada alikuwa na 1.2b wakati wenyewe walikula 45b. Sasa angalia hawa wanaongelea trillions, rekodi mpya katika ufisadi wa nchi hii alafu unasema eti mapengo yao hayazibiki, mara tutawakumbuka.
Hivi nchi inawezaje kumsahau mtu anayekwapua pesa ambazo ni zaidi ya 30% ya makusanyo ya hazina kwa mwaka!?
 
Back
Top Bottom