Nssf yasaka maeneo ya uwekezaji mikoani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nssf yasaka maeneo ya uwekezaji mikoani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by shadhuly, Mar 20, 2011.

 1. s

  shadhuly Senior Member

  #1
  Mar 20, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 141
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), umezishauri halmashauri zote nchini, kuangalia uwezekano wa kutenga maeneo ya uwekezaji ambayo mfuko huo, unaweza kuyanunua na kujenga nyumba kwa ajili ya kuziuza kwa wanachama na Watanzania kwa jumla.

  Ushauri huo ulitolewa juzi na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk Ramadhan Dau, alipokuwa akifafanua sababu za mfuko huo kujikita katika uwekezaji mkubwa katika baadhi ya mikoa huku mengine mingi ikiwa haina vitega uchumi.

  Alisema mfuko wake ulishatoa matangazo ya kuomba kununua maeneo katika halmashauri mbalimbali nchini kwa ajili ya uwekezaji lakini ni halmashauri chache tu zilizotoa taarifa za kuwapo kwa maeneo.

  "Hadi sasa tumepata maeneo katika Halmashauri za Kibaha, Bagamoyo, Kahama, Arusha na Mwanza ambako tutajitahidi kuwekeza", alisema Dau.

  Kwa kipindi kirefu Mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Mwanza inatajwa kuivutia mifuko ya jamii kwa uwekezaji, huku majiji ya Mbeya na Tanga yakielezwa kuwa katika usingizi mnono na kusahau kazi ya kuwasaka wawekezaji.

  Wakati huohuo, Dk Dau amesema Mfuko wake una sababu nyingi za msingi za kutaka upewe mgodi wa Kiwira kwa ajili ya kuzalisha umeme.

  "Mwaka 2007 , tuliukopesha mgodi huo Dola 7 milioni za Marekani ambazo hadi sasa hatujalipwa na deni limekuwa kutokana na riba. Kwa hiyo tupo tayari kununua mgodi huo kwa Sh28 bilioni na kulipa madeni mengine yote ya mgodi wa Kiwira kwa wafanyakazi na wengine,", alisema.

  Mkurugenzi Mkuu wa NSSF alisema wakipata mgodi huo watatangaza zabuni ya kimataifa kwa ajili ya kutafuta kampuni za kuzalisha umeme wa kutosha.

  Alipoulizwa mikakati ya kukwepa hasara kutokana uendeshaji wa mgodi huo, alisisitiza kwamba mgodi huo hauwezi kusababisha
  hasara, bali utaongezaa mapato na kupunguza tatizo la umeme nchini.


  SOURCE MWANANCHI 120/3/2011
   
Loading...