Old pirate
Member
- Nov 20, 2018
- 28
- 24
Jamani ili suala la NSSF limekuwa ni tatizo kubwa sana japo watu wamelifumbia macho ķama hawalioni. Tulizoea zamani unapokosa kazi hasa hizi kampuni zetu za private kimbilio lilikuwa ni vimichango hivi tulojikusanyia wakati tukiwa kazini.
Lakini kwa sasa hali ni mbaya sana unakosa ajira unakimbilia NSSF balaa unalokutana nalo huko utasema unaomba mkopo na s mali yako wahudumu wana majibu ya maudhi kweli kweli mpaka unajiuliza nani anawapa jeuri hawa?
Utapangwa miezi mitatu mitatu kuja kutahamaki miaka imekatika wala ata hawajali hilo, Namba yao ya ofisi 0800756773 imekuwa kama pambo haipokelewi kamwee hata ushinde unaipiga siku nzima na wakipokea hakuna la maana watalokueleza kwanini hupati fedha zako hali ya kuwa taratibu zote umetimiza.
KWA KWELI NI MAUMIVU MAKALI TUNAYOPITIA WAATHIRIKA WA HILI.
Una familia huna hela zako bado unashinda njaa wao wanaona sawa ni uzandiki mkubwa dhuruma yakinifu SERIKALI itutazame kwa jicho la huruma tunapita kwenye hali ngumu sana mpaka unajuta kuwa Mtanzania.
Serikali imetulazimisha kuchukua 33% ya mshahara wa mwisho tumekubali kishingo upande maana hatuna maamuzi juu ya fedha zetu lakini hili nalo limekuwa ni gumu kutekelezeka najiuliza ikitokea umekufa ndiyo basi tena maana angali hai lakini hali inakuwa hivi vipi ukiaga dunia na mtu akajifanya kudai stahiki zako anaweza pewa kesi ata ya uhujumu uchumi ili akome kabsa eeh Mwenyez Mungu tusaidie haki yetu ipatikane dhuluma hii ni uonevu mkubwa.