Ili baadaye muambie hakuna sababu ya kusema kuwa mnahitaji hela zenu mkanze maisha kipindi mkiwa hamna kazi.Sasa kile kisingizio kuwa mnaendanazisha biashara au kununu ardhi na kujenga watasema unaweza yapata hayo kupitia mikopo.Yaani hela yako uikope kwa riba.NSSF wanacheza faulu. Kweli Watanzania tunaonewa.
NSSF wametangaza masharti ya mikopo kwa Wafanyakazi, duuu it is impossible.
NSSF imefilisika kabisa, No money.
Bora kukopa benki kuliko NSSF.
NSSF wanasema watu wakope kupitia SACCOS.
Swali lake la pili, ninadhani lina mantiki kwamba, hawa wanachama wangepewa mikopo wakiwa bado kazini ili kuwaendelea. Hili ninajibu kwamba, Shirika letu la NSSF nimeliona na ndiyo maana limeshaanza kuangalia uwezekano kwa kupitia SACCOS za Wanachama kwenye maeneo yao ya kazi, kuwakopesha kupitia SACCOS na hili limeanza kufanyiwa kazi. Lingine ni kwamba, Shirika linaangalia utaratibu wa kuwakopesha wanachama wake waweze kujenga nyumba kwa kupitia katika mamlaka, baada ya mamlaka ya NSSF kuweka utaratibu kwamba, tunaweza tukawakopesha Wanachama mikopo ya kujenga nyumba, lakini hii inahitaji utaratibu ambao unatakiwa udhaminiwe au uidhinishwe na mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa hifadhi za jamii. Pindi hili likifanyika, NSSF itaangalia uwezekano wa kuwakopesha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba, yaani michango yao ile iwe ni dhamana ya kuweza kukopeshwa katika mabenki mbalimbali.