NSSF waja na hoja tatu kuhusu fao la kujitoa

sasa nikifukuzwa au kuacha...niendelee kuchangia kwa kutafuta chanzo kingine cha mapatao..... ...???..amemaanishaje huyuu...???...SITAKI SASA NIPENI CHANGU NIENDELEE NA UTARATIBU NITAKAOONA UNANIFAA NA FEDHA NIZOJIWEKEA....!!...ETI PESA NIWEKE MWENYEWE HALAFU WEWE UNIPANGIE MATUMIZI.....ULINISAIDIA KUVUJA JASHO...????
 
Wizi tu.
Niache kazi nikiwa ma miaka 60. ..halafu hawakupi fedha yako yote...napata mshahara wa 3m nachangia 600,000 kwa mwezi ...nimechangia miaka zaidi ya 15.. akiba yangu kwa nssf ni zaidi ya 75m .. nastaafu hawanipi million 75 .. wana fomula yao ya wizi...utambuli 15m ..nyengine ati pensheni ya 350,000 kila mwezi... unalipwa miezi miwili unakufa ..basi..nssf wanakomba pesa zote uloweka...familia yako haipati kitu..kila ulicho changa kimepotea...wizi mtupu....ndio maana nchi hii hatuendelei...laana ya dhulma ni kubwa.

Mimi mifanye kazi..nilipe nssf kila mwezi..nichange hadi ikifika million 50...napata ajali...nakua bedridden...ulemavu hauniruhusu kufanya kazi tena. Lkn huku nssf hawanipi million 50 zangu wala hawanipi pensheni kwa maisha yangu yalobaki.....
Samahani watu wa mifuko hiii sio social security...huu ni wizi na dhulma...
kwani ni lazima kubaki kwenye mfuko huo kama mtu ameacha kazi? halafu mtu anaweza kuwa na shida na fedha zake akafanyie shughuli nyingine bado mnamkatalia kumpa michango yake sasa akifa kabla ya kufikia huo umri mnaousema jamani lipeni fedha za watu. watu alioacha kazi wengi wanapata taabu kwa shida wakati hela yake ipo ndiyo maana hata imefikia wengine wanakufa kwa presha akifuatilia kulipwa.
 
sasa nikifukuzwa au kuacha...niendelee kuchangia kwa kutafuta chanzo kingine cha mapatao..... ...???..amemaanishaje huyuu...???...SITAKI SASA NIPENI CHANGU NIENDELEE NA UTARATIBU NITAKAOONA UNANIFAA NA FEDHA NIZOJIWEKEA....!!...ETI PESA NIWEKE MWENYEWE HALAFU WEWE UNIPANGIE MATUMIZI.....ULINISAIDIA KUVUJA JASHO...????
Ni professor au profound?
 
Professor nnamuunga mkono.

Wacheni kutaka kutumbuwa ujanani, hayo mafao yatawafaa nyie wenyewe uzeeni au mkitangulia basi warithi wenu wana japo cha kujivunia.

Professor, kaza buti.
 
Ni Mkurugenzi mkuu wa NSSF prof. Godius Kahyarara. Sababu alizotoa za kuunga mkono fao la kujitoa kuondolewa zimenifanya nijiulize maswali mengi yasiyo na majibu. hapa chini nanukuu kwa ufupi (nyekundu).

Profesa Kahyarara alifafanua mwanachama akiacha au kufukuzwa kazi anapaswa kutafuta nyingine au kuendelea kuchangia kwa kutumia vyanzo vingine kwa ajili ya maisha ya uzeeni na siyo kujitoa kwenye mfuko.

“Mfano mifuko ya wenzetu wa Zanzibar, Kenya na Uganda haina utaratibu wa fao la kujitoa,” alisema Profesa Kahyarara.

Profesa Kahyarara alibainisha sababu tatu zinazofanya uwepo ulazima wa kuondoa kipengele cha fao la kujitoa kwenye sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii.

Alitaja mambo hayo matatu kuwa ni watu wengi kughushi nyaraka za kuacha kazi, kulipa michango bila wanachama kupata faida na walio wengi kukosa pensheni baada ya kufikisha umri wa kustaafu.

Hivi huyu Prof ni Mtanzania? Anafahamu maisha wanayoishi watu baada ya kukosa kazi ama kustaafu? soma habari yote hapa chini ambayo imeandikwa na gazeti la NIPASHE leo na inapatikana IPPMEDIA.COM

NSSF waja na hoja tatu fao la kujitoa
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Profesa Godius Kahyarara aliiambia Nipashe katika mahojiano maalum hivi karibuni kuwa utekelezaji wa utaratibu wa fao la kujitoa umekuwa na athari kwa wanachama wanapofikia umri wa kustaafu.

Serikali ilikuwa inapanga kuwasilisha muswada wa sheria ya zuio la fao la kujitoa wakati wa vikao vya bunge vinavyoendelea mjini Dodoma ingawa mpango huo unadaiwa umeahirishwa.

Miongoni mwa mapendekezo yaliyomo kwenye muswada huo ni kuondolewa kwa kipengele cha fao la kujitoa na kupendekeza fao la kutokuwa na ajira kwa mwanachama aliyeachishwa kazi.

Hata hivyo, jambo hilo limepata upinzani kutoka kwa wadau mbalimbali na mwishoni mwa wiki iliyopita, vyama vya wafanyakazi na asasi za kiraia walitoa tamko la kupinga kuondolewa kwa kipengele cha fao la kujitoa.

TATIZO LA KUGHUSHI
Bila kutaja takwimu, Profesa Kahyarara alisema kasi ya wanachama wanaoacha kazi au kufukuzwa kutaka kujitoa kwenye mifuko hiyo ni kubwa.

Profesa Kahyarara, hata hivyo, amesema shirika hilo limegundua watu wengi wanaghushi nyaraka ili wapewe michango yao.

“Wanatumia nyaraka za kughushi ili kudanganya wamefikisha umri wa kustaafu, wamefukuzwa au kuacha kazi,” alisema Profesa Kahyarara.

Profesa Kahyarara alisema wamekamata watu wengi waliofanya uhalifu huo na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

MICHANGO BILA YA FAIDA
Akizungumzia athari nyingine ya fao la kujitoa, Profesa Kahyarara alisema kwa kitendo cha kuchukua michango mapema kimesababisha wanachama kukosa faida.

“Utaratibu wa mfuko pale unapomlipa mwanachama wake mafao yake basi anatakiwa alipwe na faida akiwa amefikisha umri wa kustaafu,” alifafanua Profesa Kahyarara.

Profesa Kahyarara alieleza kuwa wanachama wengi wa NSSF wamejikuta wakipoteza haki ya kupata faida kwa kitendo chao cha kuchukua michango yao mapema kabla ya kufikisha umri wa kustaafu.

ATHARI KWA WASTAAFU
Profesa Kahyarara alisema watu wengi hawajui wanapojitoa kwenye mifuko hiyo wanaathiri maisha yao kwa kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya kusaidia wanapozeeka au kupata ajali.

“Tungependa watu waweke fedha na wazichukue pale watakapofikisha umri wa miaka 55 au kama wamechangia miaka 15 mfululizo ili waishi maisha mazuri,” alisema Profesa Kahyarara.
Profesa Kahyarara alisema kuwa pamoja na kulipa mafao, pale wanachama wake wanapofikisha umri wa kustaafu basi hulipwa pia pensheni ya kila mwezi.

Alisema shirika lake halina dhamira ya kushikilia fedha za wanachama wake bali wanataka zisaidie katika maisha ya uzeeni.

“Wananchi wanapaswa kuelewa kuwa lengo la mifuko ya hifadhi ya jamii ni kutunza fedha za kusaidia uzeeni, uzazi au kupata ulemavu,” alifafanua Profeda Kahyarara.
Profesa Kahyarara alionya sio jambo zuri pale mtu anapostaafu basi anakuwa tegemezi kwa jamii inayomzunguka.

“Mtu anapokosa pensheni matokeo yake anakuwa tegemezi kwa familia, lakini angekuwa na fedha za pensheni angeendelea kuishi kwa raha na
heshima,” alisema.
Ni sawa sababu alizotoa Prof Kahyarara. Lakini kwa nini hataki kuzungumzia ukweli wa mambo haswa? Ukweli wa mambo ni liquidity problem kwa mifuko kutokana na kuwekeza kwenye non - perfoming investiment kama majengo makubwa na mikopo mikubwa ambayo hailipwi kulingana na makubaliano. Pia sababu nyingine ni kwamba nssf hawafuatilii michango ya wanachama wake ili kuhakikisha compliance rate ni nzuri. Tunajua fao la kujitoa lilikuwepo miaka yote huko nyuma lakini NSSF hawajawahi kuwa na symphaty hii ya sasa hivi.... eti wanachama wake watakosa faida ikiwa watajitoa. Hakuna mtu anayetaka kujitoa kwenye scheme hii kwa kupenda, ila mtu anapoachishwa kazi hana means nyingine yoyote ya ku- survive mfano kodi ya nyumba, nauli, ada za watoto shule, gharama za afya etc. Kupata kazi ni ngumu sana wakati huu enterprises nyingi zinayumba Tanzania hii.. kwa hiyo profesa mzima anaposema mtu aendelee kuchangia kwa sources nyingine angetusaidia kuweka bayana hizo sources na practicability yake.

USHAURI: Mimi nafikiri ni wakati wa kuangalia sheria ya mifuko hii upya kulingana na volotality ya labour market. Kwa mfano kwa sasa ili mtu aweze kuwa pensinable anatakiwa awe amechangia miezi 180, na umri usiopungua miaka 60 au 55. Kwa aina ya kazi zilizopo sokoni haswa kwenye private sector kukithi kiwango hiki ni vigumu sana, kwani kazi nyingi zinaishia kabla ya kufikisha michango hiyo 180, au kampuni zinafungwa.
Ili kuweka uwiano sawa kwa mifuko na wachaangiaji itengenezwe kanuni mpya ambayo mathalani mtu aliyechangia chini ya miezi 90 ata- qualify kwa hiyo unemployment benefit kwa miaka mitano, kama atakuwa hajapata kazi nyingine alipwe 30% ya contribution zake.
Kwa aliechangia zaidi ya miezi 90 lakini hajafikisha miezi 180 naye atengenezewe kanuni ambapo atalipwa some percentage kama malipo ya mkupuo na a fraction (between 40- 70%) of what he would have qualified as pension if at all he had attained all criteria
 
hii mifuko mungu anaiona inajua kabisa fao hili watanzania wte wanaunga mkono ila kwa sababu za kibashite wamekua wakigeuza ukweli huu
 
Huu uprofesa wanaupataje kama vitu vidogo kama hivi wanashindwa kuelewa? Mtu kaachishwa au kaacha kazi skiwa na miaka 30 akiwa amechangia miaka 7au 10 Sasa asubiri miaka mingine 30 ya kuzeeka ndipo achukue hela yake ambayo unaweza kuta haifiki hata mil 5. Hivi jamani hata kwa akili ndogo sana ya kufoji vyeti mil 5 baada ya miaka 25 au 30 ya kusubiri itafanya nini wakati huo? Na wakati wote huo mtu akisubiri kuzeeka ili alipwe mafao yake atakuwa anaishije? Ma dr na ma prof vipi?? Hizo kazi zingine ni zipi watu wamehitimu mwaka wa 3 huu hakuna ajira! Tatizo la hawa wakubwa huko juu kwa kuwa wanateuana na kupeana kazi wenyewe kwa wenyewe hawaoni tatizo la ukosefu wa ajira. Wenyewe hata wakistaafu wanateuliwa kwenye bodi mbali mbali.
 
Professor nnamuunga mkono.

Wacheni kutaka kutumbuwa ujanani, hayo mafao yatawafaa nyie wenyewe uzeeni au mkitangulia basi warithi wenu wana japo cha kujivunia.

Professor, kaza buti.
Dah Hata kama ni kuwa mpinzani hii ni too much!! Hujisikii vibaya Dada?
 
Huyu ni mwongo,

Kama kuna watu wame-forge barua za kuachishwa kazi hilo ni kosa la jinai na haukna kesi yoyote ya namna hiyo mahakamani!
 
Aiza za professar Limbumba wa Cuf kumbe wako wengi, Mwingine huyu hapa anaongea mashudu tu.
 
Dah Hata kama ni kuwa mpinzani hii ni too much!! Hujisikii vibaya Dada?

Ubaya wa nini? Kwani ni nini maana ya mafao ya uzeeni?

Unaleta mambo ya upinzani kwenye mafao ya uzeeni? Unafikiri wanaozeeka ni CCM tu?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Ni Mkurugenzi mkuu wa NSSF prof. Godius Kahyarara. Sababu alizotoa za kuunga mkono fao la kujitoa kuondolewa zimenifanya nijiulize maswali mengi yasiyo na majibu. hapa chini nanukuu kwa ufupi (nyekundu).

Profesa Kahyarara alifafanua mwanachama akiacha au kufukuzwa kazi anapaswa kutafuta nyingine au kuendelea kuchangia kwa kutumia vyanzo vingine kwa ajili ya maisha ya uzeeni na siyo kujitoa kwenye mfuko.

“Mfano mifuko ya wenzetu wa Zanzibar, Kenya na Uganda haina utaratibu wa fao la kujitoa,” alisema Profesa Kahyarara.

Profesa Kahyarara alibainisha sababu tatu zinazofanya uwepo ulazima wa kuondoa kipengele cha fao la kujitoa kwenye sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii.

Alitaja mambo hayo matatu kuwa ni watu wengi kughushi nyaraka za kuacha kazi, kulipa michango bila wanachama kupata faida na walio wengi kukosa pensheni baada ya kufikisha umri wa kustaafu.

Hivi huyu Prof ni Mtanzania? Anafahamu maisha wanayoishi watu baada ya kukosa kazi ama kustaafu? soma habari yote hapa chini ambayo imeandikwa na gazeti la NIPASHE leo na inapatikana IPPMEDIA.COM

NSSF waja na hoja tatu fao la kujitoa
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Profesa Godius Kahyarara aliiambia Nipashe katika mahojiano maalum hivi karibuni kuwa utekelezaji wa utaratibu wa fao la kujitoa umekuwa na athari kwa wanachama wanapofikia umri wa kustaafu.

Serikali ilikuwa inapanga kuwasilisha muswada wa sheria ya zuio la fao la kujitoa wakati wa vikao vya bunge vinavyoendelea mjini Dodoma ingawa mpango huo unadaiwa umeahirishwa.

Miongoni mwa mapendekezo yaliyomo kwenye muswada huo ni kuondolewa kwa kipengele cha fao la kujitoa na kupendekeza fao la kutokuwa na ajira kwa mwanachama aliyeachishwa kazi.

Hata hivyo, jambo hilo limepata upinzani kutoka kwa wadau mbalimbali na mwishoni mwa wiki iliyopita, vyama vya wafanyakazi na asasi za kiraia walitoa tamko la kupinga kuondolewa kwa kipengele cha fao la kujitoa.

Profesa Kahyarara alifafanua mwanachama akiacha au kufukuzwa kazi anapaswa kutafuta nyingine au kuendelea kuchangia kwa kutumia vyanzo vingine kwa ajili ya maisha ya uzeeni na siyo kujitoa kwenye mfuko.

“Mfano mifuko ya wenzetu wa Zanzibar, Kenya na Uganda haina utaratibu wa fao la kujitoa,” alisema Profesa Kahyarara.

Profesa Kahyarara alibainisha sababu tatu zinazofanya uwepo ulazima wa kuondoa kipengele cha fao la kujitoa kwenye sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii.

Alitaja mambo hayo matatu kuwa ni watu wengi kughushi nyaraka za kuacha kazi, kulipa michango bila wanachama kupata faida na walio wengi kukosa pensheni baada ya kufikisha umri wa kustaafu.

TATIZO LA KUGHUSHI
Bila kutaja takwimu, Profesa Kahyarara alisema kasi ya wanachama wanaoacha kazi au kufukuzwa kutaka kujitoa kwenye mifuko hiyo ni kubwa.

Profesa Kahyarara, hata hivyo, amesema shirika hilo limegundua watu wengi wanaghushi nyaraka ili wapewe michango yao.

“Wanatumia nyaraka za kughushi ili kudanganya wamefikisha umri wa kustaafu, wamefukuzwa au kuacha kazi,” alisema Profesa Kahyarara.

Profesa Kahyarara alisema wamekamata watu wengi waliofanya uhalifu huo na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

MICHANGO BILA YA FAIDA
Akizungumzia athari nyingine ya fao la kujitoa, Profesa Kahyarara alisema kwa kitendo cha kuchukua michango mapema kimesababisha wanachama kukosa faida.

“Utaratibu wa mfuko pale unapomlipa mwanachama wake mafao yake basi anatakiwa alipwe na faida akiwa amefikisha umri wa kustaafu,” alifafanua Profesa Kahyarara.

Profesa Kahyarara alieleza kuwa wanachama wengi wa NSSF wamejikuta wakipoteza haki ya kupata faida kwa kitendo chao cha kuchukua michango yao mapema kabla ya kufikisha umri wa kustaafu.

ATHARI KWA WASTAAFU
Profesa Kahyarara alisema watu wengi hawajui wanapojitoa kwenye mifuko hiyo wanaathiri maisha yao kwa kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya kusaidia wanapozeeka au kupata ajali.

“Tungependa watu waweke fedha na wazichukue pale watakapofikisha umri wa miaka 55 au kama wamechangia miaka 15 mfululizo ili waishi maisha mazuri,” alisema Profesa Kahyarara.
Profesa Kahyarara alisema kuwa pamoja na kulipa mafao, pale wanachama wake wanapofikisha umri wa kustaafu basi hulipwa pia pensheni ya kila mwezi.

Alisema shirika lake halina dhamira ya kushikilia fedha za wanachama wake bali wanataka zisaidie katika maisha ya uzeeni.

“Wananchi wanapaswa kuelewa kuwa lengo la mifuko ya hifadhi ya jamii ni kutunza fedha za kusaidia uzeeni, uzazi au kupata ulemavu,” alifafanua Profeda Kahyarara.
Profesa Kahyarara alionya sio jambo zuri pale mtu anapostaafu basi anakuwa tegemezi kwa jamii inayomzunguka.

“Mtu anapokosa pensheni matokeo yake anakuwa tegemezi kwa familia, lakini angekuwa na fedha za pensheni angeendelea kuishi kwa raha na
heshima,” alisema.

Hapa naona kama inatungwa agenda ili tusahau issue ya Vyeti. Nasema hivii sisi tunataka VYETIIIIIIIIIIIIIIIIII.
 
Mungu anawaona.

Acheni kututesa hivi na sisi pia ni binadamu.

Professor nnamuunga mkono.

Wacheni kutaka kutumbuwa ujanani, hayo mafao yatawafaa nyie wenyewe uzeeni au mkitangulia basi warithi wenu wana japo cha kujivunia.

Professor, kaza buti.
 
Ubaya wa nini? Kwani ni nini maana mafao ya uzeeni?

Unaleta mambo ya upinzani kwenye mafao ya uzeeni? Unafikiri wanaozeeka ni CCM tu?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
Stupid you-bibi kizee.
 
Ni Mkurugenzi mkuu wa NSSF prof. Godius Kahyarara. Sababu alizotoa za kuunga mkono fao la kujitoa kuondolewa zimenifanya nijiulize maswali mengi yasiyo na majibu. hapa chini nanukuu kwa ufupi (nyekundu).

Profesa Kahyarara alifafanua mwanachama akiacha au kufukuzwa kazi anapaswa kutafuta nyingine au kuendelea kuchangia kwa kutumia vyanzo vingine kwa ajili ya maisha ya uzeeni na siyo kujitoa kwenye mfuko.

“Mfano mifuko ya wenzetu wa Zanzibar, Kenya na Uganda haina utaratibu wa fao la kujitoa,” alisema Profesa Kahyarara.

Profesa Kahyarara alibainisha sababu tatu zinazofanya uwepo ulazima wa kuondoa kipengele cha fao la kujitoa kwenye sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii.

Alitaja mambo hayo matatu kuwa ni watu wengi kughushi nyaraka za kuacha kazi, kulipa michango bila wanachama kupata faida na walio wengi kukosa pensheni baada ya kufikisha umri wa kustaafu.

Hivi huyu Prof ni Mtanzania? Anafahamu maisha wanayoishi watu baada ya kukosa kazi ama kustaafu? soma habari yote hapa chini ambayo imeandikwa na gazeti la NIPASHE leo na inapatikana IPPMEDIA.COM

NSSF waja na hoja tatu fao la kujitoa
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Profesa Godius Kahyarara aliiambia Nipashe katika mahojiano maalum hivi karibuni kuwa utekelezaji wa utaratibu wa fao la kujitoa umekuwa na athari kwa wanachama wanapofikia umri wa kustaafu.

Serikali ilikuwa inapanga kuwasilisha muswada wa sheria ya zuio la fao la kujitoa wakati wa vikao vya bunge vinavyoendelea mjini Dodoma ingawa mpango huo unadaiwa umeahirishwa.

Miongoni mwa mapendekezo yaliyomo kwenye muswada huo ni kuondolewa kwa kipengele cha fao la kujitoa na kupendekeza fao la kutokuwa na ajira kwa mwanachama aliyeachishwa kazi.

Hata hivyo, jambo hilo limepata upinzani kutoka kwa wadau mbalimbali na mwishoni mwa wiki iliyopita, vyama vya wafanyakazi na asasi za kiraia walitoa tamko la kupinga kuondolewa kwa kipengele cha fao la kujitoa.

Profesa Kahyarara alifafanua mwanachama akiacha au kufukuzwa kazi anapaswa kutafuta nyingine au kuendelea kuchangia kwa kutumia vyanzo vingine kwa ajili ya maisha ya uzeeni na siyo kujitoa kwenye mfuko.

“Mfano mifuko ya wenzetu wa Zanzibar, Kenya na Uganda haina utaratibu wa fao la kujitoa,” alisema Profesa Kahyarara.

Profesa Kahyarara alibainisha sababu tatu zinazofanya uwepo ulazima wa kuondoa kipengele cha fao la kujitoa kwenye sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii.

Alitaja mambo hayo matatu kuwa ni watu wengi kughushi nyaraka za kuacha kazi, kulipa michango bila wanachama kupata faida na walio wengi kukosa pensheni baada ya kufikisha umri wa kustaafu.

TATIZO LA KUGHUSHI
Bila kutaja takwimu, Profesa Kahyarara alisema kasi ya wanachama wanaoacha kazi au kufukuzwa kutaka kujitoa kwenye mifuko hiyo ni kubwa.

Profesa Kahyarara, hata hivyo, amesema shirika hilo limegundua watu wengi wanaghushi nyaraka ili wapewe michango yao.

“Wanatumia nyaraka za kughushi ili kudanganya wamefikisha umri wa kustaafu, wamefukuzwa au kuacha kazi,” alisema Profesa Kahyarara.

Profesa Kahyarara alisema wamekamata watu wengi waliofanya uhalifu huo na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

MICHANGO BILA YA FAIDA
Akizungumzia athari nyingine ya fao la kujitoa, Profesa Kahyarara alisema kwa kitendo cha kuchukua michango mapema kimesababisha wanachama kukosa faida.

“Utaratibu wa mfuko pale unapomlipa mwanachama wake mafao yake basi anatakiwa alipwe na faida akiwa amefikisha umri wa kustaafu,” alifafanua Profesa Kahyarara.

Profesa Kahyarara alieleza kuwa wanachama wengi wa NSSF wamejikuta wakipoteza haki ya kupata faida kwa kitendo chao cha kuchukua michango yao mapema kabla ya kufikisha umri wa kustaafu.

ATHARI KWA WASTAAFU
Profesa Kahyarara alisema watu wengi hawajui wanapojitoa kwenye mifuko hiyo wanaathiri maisha yao kwa kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya kusaidia wanapozeeka au kupata ajali.

“Tungependa watu waweke fedha na wazichukue pale watakapofikisha umri wa miaka 55 au kama wamechangia miaka 15 mfululizo ili waishi maisha mazuri,” alisema Profesa Kahyarara.
Profesa Kahyarara alisema kuwa pamoja na kulipa mafao, pale wanachama wake wanapofikisha umri wa kustaafu basi hulipwa pia pensheni ya kila mwezi.

Alisema shirika lake halina dhamira ya kushikilia fedha za wanachama wake bali wanataka zisaidie katika maisha ya uzeeni.

“Wananchi wanapaswa kuelewa kuwa lengo la mifuko ya hifadhi ya jamii ni kutunza fedha za kusaidia uzeeni, uzazi au kupata ulemavu,” alifafanua Profeda Kahyarara.
Profesa Kahyarara alionya sio jambo zuri pale mtu anapostaafu basi anakuwa tegemezi kwa jamii inayomzunguka.

“Mtu anapokosa pensheni matokeo yake anakuwa tegemezi kwa familia, lakini angekuwa na fedha za pensheni angeendelea kuishi kwa raha na
heshima,” alisema.
Mshenzi huyo .asipangie watu maisha.mtu anapanga maisha yake mwenyewe.
 
Back
Top Bottom