NSSF wadhamini na kujitangaza. Je, wapo kwenye ushindani na nani kibiashara?

themagnificient

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
965
3,277
Ukiona kampuni inalipa matangazo na kufanya udhamini kwenye matamasha makubwa basi jua inafanya hivyo kimkakati hasa kubrand bidhaa zao na kuzidi kujiongezea wateja ndio maana wanaingia garama kubwa kulipa matangazo na kufanya udhamini ili kujitangaza

Sasa kwa hapa Tz NSSF ni kama haina mshindani maana Seriakali ilishaunganisha mifuko yote wakaacha miwili tu yaani ukiwa sekta binafsi utake usitake NSSF itakukuhusu tu, mean hawaepukiki ina maana hawana sababu ya kuchota pesa tena za wanachama na kwenda kulipia matamasha or matangazo

Ni muda muafaka NSSF wachunguzwe isije ikawa huu uchochoro wa kufanya udhamini kulpia matangazo.kwa garama kubwa ni mradi wa upigaji sababu wanachoma pesa ingali nssf hawana upinzani wowote
 
Wahenga walisema "usilolijua nisawa na usiku wa giza"

NSSF imepanua wigo nasasa wanachama wanaweza kutoka katika sekta isiyo rasmi yaani wajasiriamali katika nyanja zote,
Katika huu uchangiaji wa hiari, huyu mjasiriamali anaweza kunufaika na pensheni ya uzeeni kama alivyo mfanyakazi anaepelekewa michango yake na muajiri wake.
Hivyo kuwafikia lazima promotion na matangazo ya kutosha.
Huwezi ukakaa ofisini tu kutegemea mamantilie au bodaboda aache shughuli zake aje kujiunga kabla hujamuelimisha vya kutosha huko nje.
 
Back
Top Bottom