NSSF versus PPF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NSSF versus PPF

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Tores, Jan 11, 2012.

 1. Tores

  Tores JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 425
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Wadau, kwa sasa nimerudi nyumbani TZ,baada ya kufanyakazi kwa muda mrefu nje ya nchi.....Na kwa bahati nzuri nimepata kazi katika kampuni ya utafiti wa madini kanda ya ziwa, maana mimi mwenyewe ni mtaalamu wa utafiti wa madini na mafuta.Mwajiri wangu ameniambia ni lazima kujiunga na shirika mojawapo kati ya PPF au NSSF.sasa nipo kwenye dilema..naomba msaada wenu wa kimawazo lipi shirika zuri........(huduma nzuri,masharti nafuu na faida nzuri kwa mwanachama) kati ya haya niliyoyataja?
   
 2. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,259
  Trophy Points: 280
  Ungemuuliza HR wa hapo ofisini kwako ungepata jibu. Lakini pia uki-google nssf, na ppf utapata web pages zao na kuangalia benefits to members. In a nutshell pamoja na benefits zingine, ppf wewe unakatwa 5% ya mshahara wakati ukiingia mpango wa nssf wewe utakatwa 10%.
   
 3. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,583
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
  Kaka nipo PPF, Natamani kuhama hata kesho kwenda NSSF.
  Jiunge na NSSF.
   
 4. T

  Topical JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  FYI,
  NSSF ina mafao mengi zaidi kuliko PPF; PPF huwezi kupata matibabu (health benefit) lakini NSSF utapata health benefit pamoja na maternity benefit kwa mkeo

  NSSF ina matawi mengi mkoani in case ukastaafu mikoani si lazima ufuate mafao hadi Dar unlike PPF..

  chungulia brochures za ppf na nssf ziko online linganisha mwenyewe
   
 5. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  vipi kuhusu kiinua mgongo aka pension? Je formula zao zinatofautianaje?
   
 6. Tores

  Tores JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 425
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Asante sana wadau kwa ushauri wenu mzuri,.....King'asti, Kipanga kampiga mkoloni na topical......ushauri wenu nitauzingatia accordingly!
   
 7. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #7
  Jan 12, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mbwembwe za NSSF zinawakimbiza. HIvi kama mkeo hazai au hashiki mimba what will you do? JAMANI MWEEEE, PPF is the best GO for it.
   
 8. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  makubwaa! Tuambie uzuri wa PPF sist carol.
   
 9. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,259
  Trophy Points: 280
  NSSF kupata hicho kibinua mgongo ni ndoto! Nilishawasusiaga pensheni yangu, manake unaifukuzia kama unafukuzia mchumba wa JF!
   
 10. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  hahahahahaha!! Unamfukuzia bamkwe humu?
   
 11. Didia

  Didia JF-Expert Member

  #11
  Jan 13, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 721
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  Kwa usala wa mafao yako hamia NSSF. hujusikia professor anayechangia PPF akistaafu cummulative pension yake anazidiwana mwlimu wa shule ya msingi?. PPF ukiacha kazi kupata hela yako utatembea mpaka usamehe. Tumepambana nao wabadili kanuni ya kukokotoa mafao hawataki. Kwa sasa kuna mamlaka ya udhibiti imeundwa inaitwa SSRA wako katika mchakato wa kuhuisha hizi kanuni za mifuko ya pension. Lakini hii itachukua mda. Nakushauli uende NSSF maana sijasikia ikilalamikiwa kama PPF.
   
 12. C

  Chief Lugina JF-Expert Member

  #12
  Dec 4, 2013
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 290
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa wanaojua kuhusu hii mifuko miwili ya jamii,ni mfuko upi bora hasa kwa mwaajiriwa mpya hasa PRIVATE SECTOR?
   
 13. k

  kwemwale Member

  #13
  Dec 4, 2013
  Joined: Mar 2, 2013
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bora nssf hasa kwa upande wa products zake yaani mafao au benefits.
   
 14. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #14
  Dec 4, 2013
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,281
  Likes Received: 4,286
  Trophy Points: 280
  Kuna mtu anayefahamu fomula ya kukokotoa mafao kati ya PPF na NSSF
   
 15. banambavu

  banambavu Member

  #15
  Dec 4, 2013
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 62
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  Wanakwambia siku kumi! Then ukienda wakwambia siku kumi tena! Mpaka sasa mwez wa tatu! Sielewiiiiiiiiiiiiiii!
   
 16. P

  Prince Hope JF-Expert Member

  #16
  Dec 4, 2013
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 2,167
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Hawako mbali na LAPF, wanawalea wajiiri wasiopeleka michango hat zaidi ya mwaka! Mwajiri akisema ana financial crisis tu, wala hawamsumbui!
   
 17. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #17
  Dec 4, 2013
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 199
  Trophy Points: 160
  vp fao la kujitoa nssf? nampango wa kuacha kazi na kuwa mjasiliamali kuanzia january mwakani...ntapata fao langu baada ya mda gani?
   
 18. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #18
  Dec 4, 2013
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  NSSF niBora zaidi. Kwa nini? Wana mafao mengi kama walivyoeleza watu hapo juu..ina network kubwa kuliko mfuko wowote mwingine..kuhusu kuchangia sasa hivi sheria inaruhusu mwanachama kukatwa 5% au 10%. So it is your choice.

  Nssf ina reserve ratio kubwa kuliko mfuko mwingine wowote mwingine afrika mashariki na kati...yaani hata watu wakiacha kuchangia leo 'as a worst case scenario' nssf inaweza kulipa mafao yake mfululizo kwa miaka 7. Lakihi pia ina actuarial surplus ya kuweza ku-usustain mpaka miaka 50 ijayo. (Wakati mfuko kama Pspf ina Aftuaria deficit hadi serikali imeamua kuikopa bn 50 kwa mwaka ili kulipa mafao....na haya ndiyo yanaelekea kwa LAPF na PPF)

  Pia sasa hivi NSSF inaelekea kuwa Certified na ISO 9001:2008 ili kuboresha huduma zake ambazo kwa sasa zinasua sua. Ila kwa ninavyoijua ISO..hqikupatii certification mpaka uchange kweli kweli. Na mimi nategemea positives.

  MWISHO: USidanganyike, mifuko mingine yooote inacopy na kupaste mambo ya NSSF. Kwa kifupi NSSF ni baba lao wengine wanafuata.
   
 19. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #19
  Dec 4, 2013
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Private or Public...NSSF Baba lao
   
 20. M

  Memory Senior Member

  #20
  Dec 5, 2013
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 108
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Mifuko yote inaharibiwa na Serikali na hakuna mfuko unaotoa mafao ya mhimu kama fao la kupoteza kazi. ukiajiriwa mwaka mmoja na ukapoteza kazi utasubiri ufikishe miaka 55 na hapo ndo utajuuta kuwajua NSSF watakaposema hawaoni michango yako wakati mwajiri kishasepa!! nasikia wanalazimisha kuipitisha sheria ya kukaa na pesa za watu hadi 55yrs.
   
Loading...