dhi62
Member
- Sep 29, 2013
- 28
- 14
Wadau,
Kama tunavyofahamu Tanzania ni nchi isiyoongozwa kwa misingi ya dini fulani japokuwa wanaoutuongoza wana dini. Kwangu mimi naona ni jambo jema endapo hatutaangalia dini zetu ili tupate au kutoa huduma mbalimbali za kijamii. Ni hivi majuzi mfuko wa jamii ya watanzania wote NSSF imetangaza nafasi lukuki za kazi lakini zimo tuhuma ambazo zinatolewa na watu wanaodai ni wafanyakazi na wenginesio wafanyakazi kuwa NSSF kuna udini eti kama hauna 'sigda' haupati kazi au kama wewe si Abubakari au Hamisi haupati kazi. Tuhuma hizi ni mbaya na kubwa kwa mfuko unaoitwa wa jamii. Eti ili wakuajiri si kwamba umefaulu interview bali kwa majina na dini yako. Ni jambo linalohitaji ufafanuzi na ushahidi wa kutosha aidha kukubali au kukataa kuwa kuna udini au hakuna maana litaleta mpasuko kwa taifa. Moto wa dini ni rahisi kuuanzisha na kuuchochea lakini ni ngumu kuumaliza. Kesho tutaskia na PPF kuna 'UDINI' Keshokutwa tutaskia mahakamani kuna udini na mwisho itakuwa ni jeshi na ikulu kuna udini huku mamlaka zikiwa kimya.
ushahidi wangu kwa meta Uzi huu:
inaweza kuwa kweli au la ila tambua kuwa no one will bother replaying your baseless accusations. njoo na figures here how many employees there? how many are Muslims and how many are non? how many applied for jobs in respective vacancies, how many were Muslims and how many were not? who got the chance with their religions in percentages? hapo utakuwa umeeleza kisomi and you'll make sound logic.