NSSF tawi la Kahama jirekebisheni,tendeni haki kutokana viapo vyenu vya kazi

thetallest

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2017
Messages
6,232
Points
2,000

thetallest

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2017
6,232 2,000
Kama kichwa cha habari kilivyojieleza,ofisi hii ina tuhuma nzito sana kuhusiana na Mafao ya wafanyakazi waliokua wa Acacia gold mine bulyanhulu,kahama ,shinyanga.

Mgodi ulifungwa ili yafanyike majadiliano ya kina, baina ya Acacia buly na serikali .hivyo ilipelekea wafanyakazi kuachishwa kazi.

Majadiliano ya Kina pia yalifanyika baina ya wawakilishi wa wafanyakazi na mifuko ya hifadhi ya jamii yote ikiwemo na NSSF.
Makubaliano yalifikiwa kwamba mifuko italipa mafao ndani ya mwezi mmoja baada ya mwanachama kufungua madai yake.
Ni miezi minne (4) sasa kuendelea ulipaji wa nssf ndio unaleta usumbufu,mifuko mingine hili walilimaliza mapema mno.

kinachoendelea kwa sasa nssf kahama ni wafanyakazi waliokua wa Acacia buly kuhonga watumishi wa nssf kahama ili wapate mafao yao kwa kile kinachosemekana pesa chache inapokewa nssf kahama toka hazina.

Hili linafanywa na baadhi ya wafanyakazi waliokua wa buly na watumishi baadhi wa ofisi hiyo.

Mfano ,utaratibu ni kwamba mtu aliefungua 7/11/2018 anatakiwa apate kabla ya mtu aliefungua 11/11/2018 ,cha ajabu kuna wanachama wamefungua madai mwezi wa12 lakini tayari wamekwisha lipwa,hii haikubaliki hata kidogo,
Michezo hii inafanyika kwa ustadi wa hali ya juu sana,
Naomba vyombo husika vya kisheria kufuatilia kero hii,

Hali hii imefanya waliokua wafanyakazi wa buly kuichukia serikali ya Magufuli kwamba imewaletea usumbufu, watoto wao mpaka sasa hawajaenda shule,wanamadeni,fedha za liba zinawaperekesha ile mbaya.

Ushauri wangu kwa watumishi wa nssf kahama, fanyeni kazi kwa weledi,fuateni utaratibu ",first in first out " isiwe "last in first out"
 

Forum statistics

Threads 1,381,210
Members 526,018
Posts 33,792,612
Top