NSSF, NPF na mashirika kama haya Hayasaidii wadau

Nssf ni kama desi.....

Wizi mkubwa sana umefanyika, bad investment decisions(ie quality group plaza), wanategemea sana nyumba rent(one trick pony) = pension black hole est ths 59bilions.

Sasa hivi watu ambao wastaafu ni kidogo sana kulikoni wanaofanya kazi, wachangiaji ni wengi sana kwa hiyo pengo haliwezi kuonekana (deci).
Uchumi wa tz unakuwa above 5% na kazi nyingi zinatengenezwa, after 30 pengo litakuwa limekuwa kubwa sana na watu wengi ambao wanafanya kazi sasa hivi watakuwa wamestaafu

nssf inaweza isifike 30yrs kama tz ikipata majanga ya kiuchumi na growth kuwa below 3%

lete data na stats kusupport arguments zako
 
zing,

..hii forum iko under 24/7 surveillance ya NSSF PR officers.

..kuwa mwangalifu na mambo unayopost hapa kuhusu NSSF.
 
Wacha vitisho wewe wacha watu wamkome nyani ebo!

Kama hawana madudu, kwani data zina shida gani? yale yale ya siri za usalama wa Taifa.
 
Rwabugiri said:
Wacha vitisho wewe wacha watu wamkome nyani ebo!

Kama hawana madudu, kwani data zina shida gani? yale yale ya siri za usalama wa Taifa.

Rwabugiri,

..wewe kama unataka ku-test zali endelea.

..kuna PR officers wa NSSF hapa watakuchambua mpaka kijijini kwenu ulipotoka.
 
Mashirika kama NSSF, NPF na mengine kama hayo yanakusanya pesa wafanyakazi. Lakini kwa mshangao na masikitiko sioni mashirika haya kama yanasaidia wananachi zaidi ya kujinufaisha yenyewe .

Wafanyakazi mara baada ya kustaafu hawafaidiki kabisa na mashirika haya sababu pesa wanayopokea ni ndogo sana.sijui mtu anayepokea mshahara kama wa 300,000 kwa mwezi akistaafu atapata shilingi ngapi kwa mwezi. Naomba hili swali kwa wanajua watijibu.

Napendekeza wadau na serikali kwa ujumla tuwabane hawa NSSF wajenge nyumba mjini na mikoni na waziuze kwa bei nafuu kwa wafanyakazi. Badala ya kujenga maghorofa makubwa ya kupendezesha mji huku masiha ya wadau yakiwa hayabadiliki.

Miji mingi inayopendeza kama capetown na hata ulaya imepangika na inapendeza sababu mashirika kama haya ya NSSF hayatafuti miradi tu ya kupata faida haraka lakini yalenga kuinua maisha ya watu

NSSF ijenge nyumba kila mkoa za kuuzia wafanyakazi

Mdau NSSF na NPF ni kitu kimoja, Zamani ilikuwa inatwa National Provedent Fund (NPF) na baadae wakabadili mfumo wa mafao na kuita National Social Security Fund (NSSF)

NPF - Kupata mafao mpaka ustaafu miaka 55
NSSF - Kupata mafao sio lazima uwe umefikisha miaka ya kustaafu. Ni wakati wowote ule unapoamua kutofanya kazi.

Kwa bahati mbaya jinsi serikali yetu ilivyo ya kifisadi inakomba pesa kwenye mashirika hayo hayo, na kufanyia mambo ya kifisadi. pesa ambayo ni ya mfanyakazi mlala hoi kabisa unadhani kweli kuta kuwa hata na riba kwa ajili ya pesa zetu??
 
[/SIZE]

Rwabugiri,

..wewe kama unataka ku-test zali endelea.

..kuna PR officers wa NSSF hapa watakuchambua mpaka kijijini kwenu ulipotoka.

Hahaaa.. sasa mimi mtoto wa mkulima choka mbaya wanichambue nini?, watakuwa wamekosa la kufanya! (Hii ina nikumbusha siku moja mtu alikuwa akiongea habari za Kakobe pr., muumini wake akasema weee usiseme, kwani ukimsema tu anajua!)

Labda niwashauri tu kwamba badala ya kutumia muda wao kuchambua, na kudeal na watu wanao/watakao wasema na kumwaga data zao live, wautumie vyema kulitengeneza hilo shirika kwa kuweka schemes za kuwasaidia wanachama wao walala hoi. Nina hakika watakuwa wamesaidia pia kujenga na kutimiza ndoto ya maisha bora kwa walio wengi.
 
[I said:
Game Theory;500702]Unauliza maswali huku humo humo unatoa hoja zisizo na data

kwanza hebu elewa kila shirika linavyofanyakazi kisha njoo utuletee drawbacks zao ..lakini lete supporting data

hapo tunaweza kwenda mbali na mjadala huu otherwise itakuwa yale yale ya hadithi za kutafutana uchawi ambao haupo
[/I]

Supporting data? Refer article by The East African of June 8-14, 2009 titled "How Dar's connected buyers run rings around NSSF". Vilevile, ukipitia reports za CAG utaona madudu yanayofanywa na NSSF. Btw, hawa NSSF wanasifiwa kwa kazi wanayoifanya Dodoma U, lakini ninafikiri kama si kuwa na wasiwasi kuwa ile kazi ni substandard. Yale majengo yatapauka na kuchakaa ndani ya miaka michache tu. Na kwa tabia ya NSSF, nina kila sababu ya kuamini kuwa ile kazi ni overpriced!
 
wakuu ni kweli sina data lakini kwa kuangalia kuna wadau wamesema kule UDOM na mabibo mojawapo ya haya mashirika yafanya na yanaendlea kufanya mambo makubwa. Ninachomsema mimi ni

Nashukuru vile vile kuna wadau wengine wameniunga mkono. Bahati mbaya sina taaluma ya uhandishi na hivyo naweza kuteleza hapa na pale katika kujieleza. Lakini nadhani bahati nzuri kuna wengine wamenipata vizuri kwa maelezo hayo hayo.

Ninarudia kusema sio tu kwa NSSF ,michango ya wafanyakazi inayowekwa kwenye mashirika haya haitumiki katika miradi inayowasadia wachangiaji hao moja kwa moja. Nimetolea NSSF mfano sababu ya uelewa wangu mdogo nilionano lakini naamini ni hivyo hivyo kwenye mifuko mingi. ya pensheni.

Labda kweli wana miradi ya kuwasaidia watotot wa masikini lakini naomba nielimishwe ni miradi gani iliyopo ya kuwaisaidi wadau wa KCC.

Changamoto niliyotoa mimi ni kuw ahaya mashirika yangejikita kwenye ujenzi wa nyumba za makazi. Kwa kujenga nyumba za makazi na kuziuza. Kwa ngu mimi nadhani hii ndiyo miradi sahihi inayotakiwa kufanyw ana mashirika kama haya

Kila mtu hawezi kuwa na data ndo maana tunakuja sehemu kama hizi. sometime unaweza kujudge kitu kwa kuagalia OUTPUT yake ukilinganisha na INPUT kinayopta . Kwangu mimi si muhimu kujua PROCESSING. OUTPUT inayotoka kwenye haya mashirika haisadii kabisa wadau . Na output ya miradi kingi wanyofanya haiwasadii wadau zaidi ya kutafuta faida.

Hoja niliyolenga sio tu kwa NSSF nimelnga mifuko ya yote kwa ajili ya PENSION kuwa haina miradi kwa ajili ya wastaafu.

Tunaona miji ya wenzetu inapendeza kwa kuwa na nyumba zilizopangika na uniform sababu ya mashirika kama kwa kujenga nyumba wanazouziwa wadau.

Nasema tena sina data ila mwenye nazo ambaye a anaweza kunipa kuna mradi gani haya mashirika umewalenga moja kwa moja wachangiaji anieleweshe.
 
counting... 1..

Acha fujo mkuu. Point taken since we are home to great thinkers. It is unfairly unfair hawa NSSF, PPF, etc hawasaidii kabisa maisha ya wachangiaji wake hadi pale wanapokuwa off-market. Implication ni kuwa mtu atakuwa ameishi maisha ya taabu kwa ajili yao na kisha kuishi kwa matumaini baadaye. In real sense "live poor die rich" Ni wezi na ni pamoja na insurance - NIC. There is a need to survey them and if possible we should question their existence. Hata kama wewe unafanya kazi au ni stakeholder wa moja ya haya mashirika ukweli ni huo. Kukosewa swali hakumaanishi kukosewa kwa jibu.
 
Mimi hoja yangu bado ipo pale!!!mashirika yote hayo PPF,NSSF,LAPF,NHC na mengine yaungane yajenge housing scheme kubwa mijini hasa dar arusha mwanza ili kupunguza ukali wa bei zinazopaa za nyumba.....hasa dar...wajenge hata flat 100 kila flat iwe uwezo hata familia 25 au 30 phase 1 inatosha ninauhakika bei zitashuka sana tutakuwa nyumba bora,uhakika.....kuliko kuwapa wajanja wachache....
 
wakuu ni kweli sina data lakini kwa kuangalia kuna wadau wamesema kule UDOM na mabibo mojawapo ya haya mashirika yafanya na yanaendlea kufanya mambo makubwa. Ninachomsema mimi ni

Nashukuru vile vile kuna wadau wengine wameniunga mkono. Bahati mbaya sina taaluma ya uhandishi na hivyo naweza kuteleza hapa na pale katika kujieleza. Lakini nadhani bahati nzuri kuna wengine wamenipata vizuri kwa maelezo hayo hayo.

Ninarudia kusema sio tu kwa NSSF ,michango ya wafanyakazi inayowekwa kwenye mashirika haya haitumiki katika miradi inayowasadia wachangiaji hao moja kwa moja. Nimetolea NSSF mfano sababu ya uelewa wangu mdogo nilionano lakini naamini ni hivyo hivyo kwenye mifuko mingi. ya pensheni.

Labda kweli wana miradi ya kuwasaidia watotot wa masikini lakini naomba nielimishwe ni miradi gani iliyopo ya kuwaisaidi wadau wa KCC.

Changamoto niliyotoa mimi ni kuw ahaya mashirika yangejikita kwenye ujenzi wa nyumba za makazi. Kwa kujenga nyumba za makazi na kuziuza. Kwa ngu mimi nadhani hii ndiyo miradi sahihi inayotakiwa kufanyw ana mashirika kama haya

Kila mtu hawezi kuwa na data ndo maana tunakuja sehemu kama hizi. sometime unaweza kujudge kitu kwa kuagalia OUTPUT yake ukilinganisha na INPUT kinayopta . Kwangu mimi si muhimu kujua PROCESSING. OUTPUT inayotoka kwenye haya mashirika haisadii kabisa wadau . Na output ya miradi kingi wanyofanya haiwasadii wadau zaidi ya kutafuta faida.

Hoja niliyolenga sio tu kwa NSSF nimelnga mifuko ya yote kwa ajili ya PENSION kuwa haina miradi kwa ajili ya wastaafu.

Tunaona miji ya wenzetu inapendeza kwa kuwa na nyumba zilizopangika na uniform sababu ya mashirika kama kwa kujenga nyumba wanazouziwa wadau.

Nasema tena sina data ila mwenye nazo ambaye a anaweza kunipa kuna mradi gani haya mashirika umewalenga moja kwa moja wachangiaji anieleweshe.

Kazi kweli kweli

1) sasa kama unakiri huna DATA au mzee ES anita DATAZ

2) Umekiri uelewa wako ni mdogo

sasa nakupa ushauri wa bure, its never too late kupata dataz...ongea na GREAT THINKERS wa Jamii forums na wengineo watakupatia dataz...kisha zilete tuzichambue

Halafu kama uelewa wako ni mdogo nadhani itakuwa ngumu zaidi kujadialiana nawe chochote kile lakini si tatizo maana sitokufeed midijada unyambue kwani uelewa wako ni mdogo

pole sana
 
[/I]

Supporting data? Refer article by The East African of June 8-14, 2009 titled "How Dar’s connected buyers run rings around NSSF". Vilevile, ukipitia reports za CAG utaona madudu yanayofanywa na NSSF. Btw, hawa NSSF wanasifiwa kwa kazi wanayoifanya Dodoma U, lakini ninafikiri kama si kuwa na wasiwasi kuwa ile kazi ni substandard. Yale majengo yatapauka na kuchakaa ndani ya miaka michache tu. Na kwa tabia ya NSSF, nina kila sababu ya kuamini kuwa ile kazi ni overpriced!

Attempt yako bado imefeli...

Mjomba rudia tena kutafuta valid data kwa sababu hata hao East African hiyo story waliinyofoa kutoka kwenye CAG report ambayo yote ni void...au hukuona tangazo maalum lililotolewa na aliyetajwa kwenye hiyo news clip magazeniti wiki 3 zilizopita

Hivi unajua kama Ludovich Utoh yuko kwenye position mbaya baada ya kuandika hiyo ripoti ambayo ni vull and void?

narudia

Leteni credible data tujadili nakupa tena nafasi ya kufanya hivyo nami siendi kokote kule nitakwepo humu nakusubiri kwa hamu
 
Mimi hoja yangu bado ipo pale!!!mashirika yote hayo PPF,NSSF,LAPF,NHC na mengine yaungane yajenge housing scheme kubwa mijini hasa dar arusha mwanza ili kupunguza ukali wa bei zinazopaa za nyumba.....hasa dar...wajenge hata flat 100 kila flat iwe uwezo hata familia 25 au 30 phase 1 inatosha ninauhakika bei zitashuka sana tutakuwa nyumba bora,uhakika.....kuliko kuwapa wajanja wachache....

sasa wewe unaongea na mtu ambaye ukimuuliza mara ya mwisho kaenda kijijini kwao hajui sembuse kukanyaga ardhi ya Tanzania

kalaghabaho wee
 
Kwanza unajua kuna Pension funds ngapi Tanzania?

Je unaweza kutuonyesha performance zao zikoje?

Then nashangaa kichwa chakocha habari umesema NSSna PPF lakini lawama umeamua kuzimwaga NSSF lakini hukutia neno kuhusus PPF kulikoni?

Mimi niko tayari kujadiliana nawe kuhusu hili lakini liwe based on DATA and STATS kusupport arguments au unasemaje?

Mimi siko ndani ya mshirika hayo ila ni mdau. sijui performance zao zaidi ya kusikia wakijisifia kwenye vyombo vya habari na kuona maghorofa na majengo wanayojenga kwenye baadhi ya miji.

Pili inawezekana nimekosea lakini lengo langu ilikuwa kutoridhihswa na priority za miradi zinatolewa na haya mashirika. Nimetuma NSSF kama picha ila ninalenga mifuko yote ya pension naamin utendaji wao uko swa tu. Sijasikia hata j1 aumejenga nyumba za makazi ya wafanyakazi wa kawaida.

Kuhusu DATA na STATS sina kwa kweli ila ninaweza ku evaluate kitu kutokana na OUTPUT yake. Sijaridhishwa na OUTPUT yao. Na ninaona walipwaji pensio wengi. Lakini kwa upande mwingine nikisema sijaona mradi unawalenga moja kwa moja wa wafanyakazi hiyo ni DATA kama nimekosea nieleweshe. Statisctic ingawa sina ziko wazi . Mfano thamani ya pesa utakayopokea baada ya kustaafu itakuwa chini kwa hiyo mafao hayawezi kukusaidia kinachowez akumsadia mwanachi wa kawaida ni asset kama nyumba. Kama mimi labda nakatwa 30,000 kwa mwezi na muajiri wangu anakatwa 30,00 hizo ni 60,000 . Naamini nikija kustaafu 60,000 itakidhi mahitaji machache sana ulinganisha na sasa.
 
zing,

..hii forum iko under 24/7 surveillance ya NSSF PR officers.

..kuwa mwangalifu na mambo unayopost hapa kuhusu NSSF.

Ni vizuri kama iko under surveillance maana ninaamini dukudukua za wadau zitafanyiwa kazi .

labda uniambie niwe mwangalifu wapi. siridhishwi na utendaji wao ukizingatia na mimi ni pensioner mtarajiwa .kama wanasoma naomba waanzishe miradi ya kujenga hata nyumbza za vyumba viwili kwa wafanyakazi wa kawaida.
 
Mimi siko ndani ya mshirika hayo ila ni mdau. sijui performance zao zaidi ya kusikia wakijisifia kwenye vyombo vya habari na kuona maghorofa na majengo wanayojenga kwenye baadhi ya miji.

Pili inawezekana nimekosea lakini lengo langu ilikuwa kutoridhihswa na priority za miradi zinatolewa na haya mashirika. Nimetuma NSSF kama picha ila ninalenga mifuko yote ya pension naamin utendaji wao uko swa tu. Sijasikia hata j1 aumejenga nyumba za makazi ya wafanyakazi wa kawaida.

Kuhusu DATA na STATS sina kwa kweli ila ninaweza ku evaluate kitu kutokana na OUTPUT yake. Sijaridhishwa na OUTPUT yao. Na ninaona walipwaji pensio wengi. Lakini kwa upande mwingine nikisema sijaona mradi unawalenga moja kwa moja wa wafanyakazi hiyo ni DATA kama nimekosea nieleweshe. Statisctic ingawa sina ziko wazi . Mfano thamani ya pesa utakayopokea baada ya kustaafu itakuwa chini kwa hiyo mafao hayawezi kukusaidia kinachowez akumsadia mwanachi wa kawaida ni asset kama nyumba. Kama mimi labda nakatwa 30,000 kwa mwezi na muajiri wangu anakatwa 30,00 hizo ni 60,000 . Naamini nikija kustaafu 60,000 itakidhi mahitaji machache sana ulinganisha na sasa.

Sasa mkulu huna data huna chohcote ni vigumu kufanya argument na wewe au?
 
Kazi kweli kweli

1) sasa kama unakiri huna DATA au mzee ES anita DATAZ

2) Umekiri uelewa wako ni mdogo

sasa nakupa ushauri wa bure, its never too late kupata dataz...ongea na GREAT THINKERS wa Jamii forums na wengineo watakupatia dataz...kisha zilete tuzichambue

Halafu kama uelewa wako ni mdogo nadhani itakuwa ngumu zaidi kujadialiana nawe chochote kile lakini si tatizo maana sitokufeed midijada unyambue kwani uelewa wako ni mdogo

pole sana

Na ninaposea uelewa wangu ni mdogo haina maana sielewi mambo. ninaposema uelewa wangu ni mdogo ni sababu ni kiu ya kujua zaidi ya ninayoyajua. kila siku kunajambo jipya ninalijua . hakuna mtu perfect amabye kakamilika kila idara. Kama wewe umefikia kilele cha uelewa wako hongera sana

Pia kama wewe unadhani position uliyonayo ni ya kutoa elimu tu na unahisi you dont absorb any thing from the society and enviroment then ure a MASSIAH wich i can doubt 99.9%. Assure me of tha please so that i know u better

Kwa Kujua kitu kimoja au vyote yaani INPUT, PROCESS na OUTPUT ya system basi unaweza kujudge performance yao. Wewe kama una uelewa wa kila input , processing na output ya kila system hongera.

Kwa haya haya mashirika mi ninayapima kutokana na OUPUTyake. sijui kwa undani PROCESSING gani wanafanya lakini naelewa some INPUT. uiza walipwaji pensheni kiasi wanachopkea( OUTPUT) kama kinaendana kwa tahamni na kiasi walichoweka kipindi hicho.

Be infomred that nilichosema is not only DATA but is INFORMATION. Naomba nikupe pole ingawa najua itakuwa vigumu kuipokea. Katika machache unayotakiwa kujifunza na wewe ni we can achieve tha same thing through diffrent path and views.
 
nashauri kakusanye kwanza data kisha uje vizuri

bado hujajiandaa vya kutosha mzee

mimi niko bize na MoU ya Kanisa na Serikali
 
Mdau NSSF na NPF ni kitu kimoja, Zamani ilikuwa inatwa National Provedent Fund (NPF) na baadae wakabadili mfumo wa mafao na kuita National Social Security Fund (NSSF)

NPF - Kupata mafao mpaka ustaafu miaka 55
NSSF - Kupata mafao sio lazima uwe umefikisha miaka ya kustaafu. Ni wakati wowote ule unapoamua kutofanya kazi.

Kwa bahati mbaya jinsi serikali yetu ilivyo ya kifisadi inakomba pesa kwenye mashirika hayo hayo, na kufanyia mambo ya kifisadi. pesa ambayo ni ya mfanyakazi mlala hoi kabisa unadhani kweli kuta kuwa hata na riba kwa ajili ya pesa zetu??
Tuko pamoja.....Mimi nilitegemea mashirika kama haya ndiyo yang'e kuwa ya kwanza kukopesha wafanya kazi au wateja wao lakini leo hii hata kupata haki yako ni mbindi ukiacha kazi mpaka ukaipate pesa yako ni baada ya miezi sita unapigika hao ni (NSSF), mimi huwa najiuliza: Mfano NSSF nina Mil 3 wanaona ubaya gani kunikopesha mil 2 bila riba yoyote kwasababu nipesa yangu etiiiiiii. ukitaka uone music achaka kazi harafu jaribu kufatilia mafao yako...mara watakuambia pesa bado haijaingia kwenye system...system system kitu gani au huwa wanazifanyia biashara kwanza mpaka miezi 3--- ndiyo ziingizwe kwenye system...Mfano ukipata report ya NSSF leo utakuta imekomea records za january je hii miezi feb mpaka Jun iko wapi?, mimi nahisi kuna mjitu inafanya biaashara kwa pesa zetu..... Nimeshuhudia mtu anaacha kazi iliachukue NSSF na Mwingine akiomba aachishwe kazi ilipate PPF harafu akikabiziwa barua anaomba kazi ama pale pale au pengine akiulizwa kama alishajiunga na mashirika kama NSSF au NPF anakataa nakama alikuwa amejiunga NSSF basi atajiunga na PPF! kinachofata hapo ni ufisadi maana ataenda kuongea na daktari (anampa kitu kidogo) ili aandikiwe kwamba 'anatakiwa kufanyiwa upasua" ili tu apate mafao yake haraka..
 
Back
Top Bottom