NSSF ni siasa, wizi au kiwango duni cha uelewa kwa watendaji


F

fikirikwanza

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Messages
6,776
Likes
1,030
Points
280
F

fikirikwanza

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2012
6,776 1,030 280
Hii nchi imekuwa ya amani pengine sio amani bali utulivu kwa muda sasa, kwa maaana mtanzania sio mtu wa kung'ang'ania jambo hata kama linagusa maisha yake ya kila siku. Ipo mifano mingi yakiwemo kodi kubwa kwenye bidhaa na ushuru, mishahara nk. Matumizi mabaya ya madaraka kwa waliokabdhiwa dhamana sasa limekuwa janga kubwa kwa taifa. Ukweli kwamba karibu serikali yote iko lege lege hakumaninishi huu udhaifu ni halali kwa kila mtu na taasisi za serikali.

NSSF: Chombo kilichoanzishwa kwa sheria ya bunge sasa ni mwiba kwa wanachama wake na wananchi kwa ujumla:
1. Kupata mafao imekuwa kazi ngumu kuliko kutafuta pesa na kuhakikisha unachangia kupitia makato kwenye mishahara yako

2. Baada ya kufanya mchakato wa kumlipa mtu chake kuwa mgumu na wenye harufu ya rushwa, wakaja na kali kuliko eti hakuna kuchukua fedha yako mpaka umri wa kustaafu (wanajua kila MTz atafikisha umri huo, hivyo asubiri), hizi ni siasa, wizi au akili ndogo??? watendaji wa NSSF mtajipambanua vipi juu ya hili??

3. Baada ya wananchi kuja juu tamko la kipuuzi la kuzuia fao la kujitoa likafutwa, malipo ya kujitoa yakaanza tena.Mchezo mpya ukabuniwa, lazima uwe mjinga kidogo ili kufanikisha wizi na udanganyifu. Hesabu zitakosewa tena kwa alimia 80% wa wananchama ili kuleta tafurani wakati wa malipo.

4. Wataandaa hesabu feki, hata kama wanaona kuna hela imebaki kwenye akaunti yako, hawatauliza utalipwa sehemu ya pesa yako, iliyobaki wanasubiria iwapo utafuatalia au la, je kama hujui namna ya kufuatilia unafanyaje? kama hujui mahesabu wanafanyikaje unafanyaje? wanabakisha fedha hizo kwa madhumuni gani? HUU ni wizi au makosa ya kibinadamu? watendaji WAKUBWA WANAELEWA HILI AU LA? hawaifahamu ofisi wanayoiongoza?

5. Ili kufanikisha matakwa yao, mawasiliano ya simu-simu zao kila ukipiga zinatumika laini zaidi ya 20, email-ama hawajasoma vya kutosha hawajui kutumia au ni kiburi cha kuharalisha mambo yako, matatizo mengi kuliko majibu mara email haijafika-mara wakikujibu zinabounce ili mradi majibu yawe ya mdomo kuandika hawataki, dunia ya leo mtu anaomba aandikiwe barua itumwe kwa posta? hao ndo NSSF.

6. WANAWEKEZA MICHANGO YA WATEJA MPAKA MTEJA ANAINGIA HASARA, je uwekezaji unaomwingiza hasara mteja ni kwa faida ya nani? KAMA hutoi riba au unatoa 1-2% per annum, bila kujadili kiasi cha fedha mtu anacho inakuwaje? benki zenyewe wanatoa hadi 15% kutokana na wingi wa fedha, NSSF 1-2% kweli hii? kwa nini unawekeza hadi mteja hapati haki yake? tunawekeza hela ya mteja au ziada?? yaani baada ya mteja kupata hela yake kujumlisha faida angalau 5-10% per year; zinazobaki kweli ni ziada zinawekezwa; Ina maana mteja wa leo anaibiwa ili sijui wa lini aje kufaidi. AKILI NI NDOGO, serikali haijaagiza hivyo, WATENDAJI WA NSSF lazima muuonesha kuwa akili mnazo na mnaweza kuzitumia kwa manufaa ya wanachama wote; sio ili mradi mipango hata kama ni mibovu

TUNACHANGISHWA KWA LAZIMA NA KUZUNGUSHWA KUPEWA MICHANGO YETU HADI LINI? Kila kona tatizo ni hilo hilo, Kwani lazima mtu hangaishwe kabla ya kuchukua michango yetu??? KWA HALI HII RUSHWA ITAKUWA KUBWA NDANI YA NSSF, Vyombo vimulike suala hili.

Nawasilisha
 
S

SILENT GUNNER

Member
Joined
Jan 23, 2012
Messages
22
Likes
0
Points
0
S

SILENT GUNNER

Member
Joined Jan 23, 2012
22 0 0
Inasikitisha sana kuona usumbufu huu kwani mi pia imenichukua miezi saba mpaka nane kupata card mpya yani smartcard, mpaka nilivogomba sana ndio kaka mmoja akaamua kuprint, otherwise kila ukienda kabla hata hajakusikiliza vizuri anakupiga tarehe mwei au miezi miwili, hapa ubungo kuna dada anaitwa haika ndio anakela sanq japo inaonekana kalibu wote wanatabia moja. Utakuta wanapiba stori tu hana hawajali. Nilituma email hawajibu nilipoomba kuonana na ngazi za juu ndio wakaonekanq kujali japo kidogo. Wanakela sana mi naona kuchqngia ie optional
 
Capt Tamar

Capt Tamar

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2011
Messages
9,029
Likes
7,091
Points
280
Capt Tamar

Capt Tamar

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2011
9,029 7,091 280
Utaambiwa mara ngapi???Serikali(wanasiasa) ilimpumbaza Dr dau na kusomba hela kwenye mfuko huo,ili kutimiza baadhi ya ahadi lukuki walizotoa kwa wananchi,fedha hizo zilitolewa kama mkopo ila cha kuhuzunisha ni kuwa serikali imekwama kurudisha fedha hizo,na ili kuweka mambo sawa kwa upande wa shirika na kupunguza idadi ya wadai,serikali ilikubaliana na nssf na mashirika mengine kuunda sheria itakayozuia watu kuleta madai yao hadi hali ya kiuchumi ya shirika ipate ahueni,likaja wazo la miaka 60 ndipo udai chako,hilo limeshindikana,na bado hali ya shirika si nzuri,hivyo lazima lijiendeshe kiujanja ujanja ili liweze ku survive,rushwa nayo imepata parking hapo.
 
Anko Sam

Anko Sam

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2010
Messages
3,212
Likes
25
Points
135
Anko Sam

Anko Sam

JF-Expert Member
Joined Jun 30, 2010
3,212 25 135
CCM imemfanya Rama Dau kuwa ni mfadhili wake, utakuta jambo ambalo ni wajibu wa Serikali kulitekeleza kwa kutumia Budget yake, utakuta Dau ana mwaga pesa za wanachama hovyo hovyo ili kujikomba kwa aliye mteua. Kila sehemu utamkuta anatoa hela za wanachama.

Kama JK aliachiwa na Ben Nkapa hazina imetuna mpaka basi, deni la Taifa lilikuwa around Tsh. 4 Trillion, akanza kuzigawa kama Mamilioni ya JK alifikiri haziwezi kwisha. Alipozimaliza akaanza kukopa mapaka deni la Taifa Tsh. 22Trillioni na hatujui zimekwenda wapi! Akaona hali mbaya sasa amegeukia wateule wake waokoe jahazi, huyu Dau ndo amekuwa legelege kabisa, mara wanazuia michango ya watu na sasa wanawazungusha wanachama!

Rama Dau tunza pesa za wanachama na si kila kitu umkubalie mweshimiwa! Mkatalie la sivyo mtakuja juta wenyewe wakiamua kuzifuta!
 
M

MzalendoHalisi

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2007
Messages
3,908
Likes
184
Points
160
M

MzalendoHalisi

JF-Expert Member
Joined Jun 24, 2007
3,908 184 160
Juzi Dau nilimwona Morocco wakati wa Taifa Stars!

hivi ile pesa alitoa kwenye salary yake au ni hizo pesa za wanachama?

Nahitaji ufafanuzi!
 
K

kamkoda

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2012
Messages
395
Likes
5
Points
35
K

kamkoda

JF-Expert Member
Joined Sep 20, 2012
395 5 35
Nssf wanahitaji mageuzi makubwa sana hata huo mtego wa kuhamasisha watu waanzishe saccoss ni story tu ya abunuwasi, hela ya mtu tena yake mwenyewe halafu umkopesha akurudishie na faida mbona mnafika mbali jamani wekeni ATM MACHINE WATU TUCHUKUE FEDHA ZETU WANAVYOFANYA HUKO DUNUANI SIVYO MNAVYOFANYA
 
J

johnmashilatu

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2010
Messages
560
Likes
292
Points
80
J

johnmashilatu

JF-Expert Member
Joined Sep 16, 2010
560 292 80
Aaaaghhh, nafikiri headline haijakaa vizuri sana. lakini yote kwa yote NSSF ni usumbufu, kero, rushwa, kusimangwa n.k... nchi hii mambo yanakwenda ndivyo sivyo.

Ukienda NSSF utafikiri unakaribia kuingia Rumande ya polisi, kambi ya JWTZ au unataka kuingia gerezani. ofisi ina walinzi wenye mabunduki makubwa yanayobebwa sijui kwa lengo la kumtisha nani.

ukienda ofisi za NSSF mwanza, wale walinzi pale mapokezi hawana lugha nzuri, hasa yule mzee mfupi, utaulizwa maswali kana kwamba umeingia hapo kufanya uhalifu.

ukiingia upande wa kusihoto ambako wananchama wana-process madai yao huko ndio janga. watu wan kaa zaidi ya saa sita bila kupata huduma! kitu kimoja wanaochosahau wafanyakazi wa ofisi hizo ni kuwa wako pale kwa ajili ya wananchama, sio wao wako kwa ajili ya wanachama!. kuwaoana wanachama kama rai wa daraja la tatu kama ilivyokuwa enzi za ukoloni ndio jadi ya ofisi hiyo. huduma mbovu.

kuna watu wanafuatilia madai yo kwa zaidi ya miezi sita bila kuambulia chochote, wanapigwa danadana usiombe. kunatengenezwa mazingira ya kutoa chochote ili uweze kupata haki yako! umekwwenda na barua yako ya kumaliza mkataba wako inabainika ina kasoro na kuambiwa nenda kafanye marekebisho. unarudi baada ya saa moja wanasema umegushi! wanaishi wapi hawa wasiofahamu zama za sasa za teknolojia inavyorahisisha mambo!, kwanini nifunge safari ya kwenda mtwara wakati inawezekana nikapiga simu huko( mtwara) na wakanitumia barua nyingie ndani ya dakika 10?

Nimeshuhudia kuwa wafanyakazi hwajali muda wa wateja wao. labda kwa sababu wanadai mafao( kwa wanaofanya hivyo) haiwezekani mtu afuatilie mafao yake kwa zaidi ya miezi mitatu, hata kama ameacha hiyo iliyompelekea kupata hayo mafao bado ana mambo mengine ya kufanya na hata kama ni kupumzika basi asichaguliwe kwamba aende kupumzika NSSF

jambo la Msingi hebu kuweni wazi. waelezeni wateja au ikiwezekana bandikeni kwenye mbao zenu, kwamba mteja aliyekamilisha taratibu zote anapaswa kulipwa ndani ya kipindi gani, ili watu wajue wanaweza kuchukua hatua gani baada ya muda huo

wakubwa wa NSSF mwanza, kwanini mnafanya kazi kwa mazoea? haiwezekani siku oja mkahamishia dawati lenu hata kwa saa moja hapo eneo ambako wanachama wanadai mafao yao?

Au hamwezi kununua "line" ya simu ya mkononi ambayo itakuwa inakaa ofisini na namba zake kuzibandika kila mahali ili kupokea hoja za mnaodai kuwahudumia?
 
Silly

Silly

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
534
Likes
41
Points
45
Silly

Silly

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2010
534 41 45
Tumeizoea Tanzania yetu ya - kubali yaishe - hata kama hayaishi tunakubali tu. Ifike mahali tuwajibishane tu hata kama ni ndugu au jamaa yako, otherwise hii ya kubebana tutaona mengi sana.
 
Ulukolokwitanga

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2010
Messages
8,416
Likes
3,937
Points
280
Ulukolokwitanga

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Joined Sep 18, 2010
8,416 3,937 280
Mhmh, mi sichangii kitu hapa nisije nikaonekana MDINI bure....
 
mkomatembo

mkomatembo

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2011
Messages
1,478
Likes
529
Points
280
Age
61
mkomatembo

mkomatembo

JF-Expert Member
Joined Dec 17, 2011
1,478 529 280
Juzi Dau nilimwona Morocco wakati wa Taifa Stars!

hivi ile pesa alitoa kwenye salary yake au ni hizo pesa za wanachama?

Nahitaji ufafanuzi!
Wewe unasema morocco, afadhali hiyo morrocco, kuna yale mashindano ya juzi juzi hapa ya kombe la nssf linatusaidia nini sisi wachangiaji?
 
F

fikirikwanza

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Messages
6,776
Likes
1,030
Points
280
F

fikirikwanza

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2012
6,776 1,030 280
Tuungane kupinga wizi huo, Tuungane kudai haki ya kusikilizwa na kupewa michango yetu tunapoihitaji kwa faida inayokubalika. UNYONGE SASA BASI!!!! sio kukopeshwa pesa yetu wenyewe
 
M

MzalendoHalisi

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2007
Messages
3,908
Likes
184
Points
160
M

MzalendoHalisi

JF-Expert Member
Joined Jun 24, 2007
3,908 184 160
Kama hamjui mkubwa pale huwezi pata kazi!

Ndo maana utendaji mbovu!
 
A

adobe

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2009
Messages
1,897
Likes
505
Points
280
A

adobe

JF-Expert Member
Joined May 6, 2009
1,897 505 280
Ukitaka kujua nssf nenda ubungo.niliuwa pale siku chache zilizopita hakuna cooperation kati ya uongozi na staff.meneja aliweza kuongea mambo ya hovyo na staf wake pamoja na kuvaa suti alidharaulika sana.pamoja na kuzunguka kuangalia staf wanavyofanya kazi lakini lugha zake si nzuri.so kuanzia meneja hadi staf wana lugha za hovyo.
 
mirisho pm

mirisho pm

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2012
Messages
2,875
Likes
4,882
Points
280
mirisho pm

mirisho pm

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2012
2,875 4,882 280
me nshajitoaga huko.... waah! nasubir tu muda nikapachimbe, hata sh 5 yangu hailiki na haya majitu ya hovyo sana.
 
K

kulyanganga

Member
Joined
Nov 13, 2012
Messages
61
Likes
0
Points
0
K

kulyanganga

Member
Joined Nov 13, 2012
61 0 0
nadhani umekurupuka kuandika mawazo yako mabovu, suala kusitisha mafao halijaanza NSSF bali kama haujui kuna mdhibiti anaitwa SSRA, waajiri pamoja na Bunge , usumbufu wa mafao unatokana na sisi wenyewe wanachama taarifa zetu kutozikumbuka wakati wakufungua mafao pia ningekuomba ndugu yangu uwe unaudhuria semina mbalimbali za mifuko ya hifadhi ya jamii pia haukatazwi kuomba vipeperushi, vitabu sheria ya mifuko husika ili kuzifahamu watu wengi wenye mawazo mafupi kama wewe mifuko hii wanafanaisha na bank, ndugu yangu kama ulikosa kazi sio kwa urasimu haukutimiza vigezo! ACHA IENDELEE KUONGOZA, IWEKEZE KWA MANUFAA YAKO NA HATA UKIENDA KUCHUKUA MAFAO YAKO UTAPEWA ULICHOCHANGIA NA INTEREST JUU.
 
M

MPadmire

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
3,132
Likes
1,577
Points
280
Age
51
M

MPadmire

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
3,132 1,577 280
NSSF inahusu hasa wafanyakazi sekta binafsi na VYama vya wafanyakazi vimekuwa legevu sana, Why?......

Je kwa nini wafanyakazi wanalalamika tu bila kuchukua hatua..... Piga viongozi chini, weka Viongozi wa muda, piga migomo na Maandamano. nashangaa hata wamachinga mtwara wanawashinda wafanyakazi walioenda shule kidogo Mhh.

FAO la kujitoa je lipo ama NSSF waliwapiga changa la macho?????

Je ongezeko la Mshahara sekta binafsi litatekelezwa????

Tafakari, chukua hatua...
 
F

fikirikwanza

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Messages
6,776
Likes
1,030
Points
280
F

fikirikwanza

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2012
6,776 1,030 280
Ukitaka kujua nssf nenda ubungo.niliuwa pale siku chache zilizopita hakuna cooperation kati ya uongozi na staff.meneja aliweza kuongea mambo ya hovyo na staf wake pamoja na kuvaa suti alidharaulika sana.pamoja na kuzunguka kuangalia staf wanavyofanya kazi lakini lugha zake si nzuri.so kuanzia meneja hadi staf wana lugha za hovyo.
UBUNGO/Kinondoni ndo imekuwa gumzo, kuanzia chief manager hadi wapokea fomu, pamulikwe UBUNGO
 
F

fikirikwanza

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Messages
6,776
Likes
1,030
Points
280
F

fikirikwanza

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2012
6,776 1,030 280
Katika hali ya kawaida inawezekanaje chombo cha umma na serikali kama NSSF kuwa na sera na mipango, utaratibu mbovu? Kwa nini kila mwanachama wa NSSF analamika inapofika kuchukua mafao yake? Je ni lazima nyie ndo muendeshe NSSF hata baada ya kushibdwa kuiendesha?? Je sio VYEMA KUKAA NYIE KUKAA PEMBENI AKILI MPYA ZIFANYE KAZI? Je na Kutoka NSSF mnasubiri maandamano ya wananchama? Kama hamtaki kutoka, basi pigeni kazi kwa akili na weledi.
 

Forum statistics

Threads 1,273,872
Members 490,535
Posts 30,494,155