wanajamvi wenzangu, hapa tzie tunayo mifuko kadhaa ya hifadhi za jamii nssf ikiwa mojawapo. Nawapongeza sana wafanyakazi mpaka mkurugenzi wake kwa weledi wao na kasi yao ya kuwekeza katika nchi yetu. Mimi kama mtanzania wa kawaida ninafurahia sana kuanzia ujenzi wa hostel za mabibo, sua, ujenzi wa nyumba za bei rahisi kinyerezi, ujenzi wa majengo mengi mengi kama vitega uchumi. Kiukweli nawapongeza sana.
Hayo yote tisa na sasa wameamua kujikita kwenye ujenzi wa daraja la kigamboni ambalo litapunguza kero ya vivuko kwa wakazi wa dar es salaam.
Funga kazi ambayo imenivutia zaidi ni kuamua kuwekeza kwenye uzalishaji wa nishati ya umeme ili kuwaondolea watanzania adha wanayoipata... Sina cha kuwapa ila nawaomba wachape kazi isije ikawa tembo akisifiwa........
Wito wangu kwenu kama mtanzania mwenzenu, naomba sana sasa mvuke mipaka, msijifungie hapa hapa, msiige mabenki yetu wala viwanda vyetu au niseme utamaduni wetu wa uoga nendeni nje ya mipaka muwekeze na muitangaze nchi yetu. Mungu wabariki nssf