NSSF na nyumba za kuuza ni kwa faida ya Nani ?

Mnama

JF-Expert Member
Oct 13, 2010
2,665
2,127
Katika hali ya kusikitisha nyumba zilizojengwa na hili shirika kwa ajili ya kuwauzia wanachama wake ni kiinamacho cha ajabu,nyumba zenyewe chache halafu bado bei ghali kuanzia million 77 hadi 109 na bado wankusukumizia uenda ukachukue mkopo Commercial Bank of Africa (CBA) huku nako unakutana na uwizi mwingine maana ukipewa mkopo wa Million 100 riba 19.5 % p.a kwa miaka 20 mpaka umalize umelipa Million 450 na hapo rejesho la mwezi ni 1.8 millioni na inatakiwa iwe 45 % ya net pay.

Sasa huku ni kumsaidia mwanachama au kuzifaidisha Benki ? maana ni kama wamegeuka mawakala wa benki wa kujenga nyumba na kuisogezea benki ikutafune.kwa nini wakati hela zilizotumika kujenga hizo nyumba ni akiba zetu wanachama .

why not hirepurchase kama kweli wanataka wanachama wafaidi na wawe na moyo wa kujiwekea akiba ?
 
Back
Top Bottom