Ngaliba Dume
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,710
- 3,669
Ni week ya sasa Wajawazito katika ofisi mbalimbali za jiji la Dar es Salaam hawapati huduma,iwe Ubungo au Ilala kwa wakazi wa Dar es Salaam.
Inaenda karibu week ya pili sasa kwa wajawazito ukienda kwenye ofisi za NSSF kwa ajili ya Fao la Ujauzito ni kero tupu,sababu mara mtandao unasumbua mara hatupokei hizo form.
Kitengo cha Huduma kwa Wateja Ofisi za NSSF Ubungo Plaza ni ovyo na aibu tupu.Unaenda unamkuta mwanamke badala ya kumuhudumia mwanamke mwenzake aliye katika matazamio kwa upole na ukarimu,inakuwa ni lugha ya ukali na ghadhabu.
Mtu mfanyakazi,anachangia pesa zake lakini ni usumbufu mtupu.Lugha wanayotoa wahudumu ambao walipaswa kutoa lugha nzuri na ya staha ni kinyume chake,watu wapo ofisini kama wamelazimishwa.
Ifikie mahali wahudumu katika hizi ofisi watambue kuwa wapo hapo si kwa ajili yao na hawalipwi mishahara sababu wanakaa tu,bali ni kwasababu wanahudumia wateja ambao ndio wafanyakazi wanaochangia pesa hizo.
Kila unapooenda unakutana na lugha za "mtandao hakuna,hatujui utarudi lini" au "Forms za fao la uzazi hatupokei kwa sasa,jinsi ya kujaza kaulize huko walikokuambia kuwa tunatoa fao la uzazi".
NSSF kama wadau wa wafanyakazi wanatakiwa kuwajali wateja wao,kutoa huduma nzuri na kuwa na lugha nzuri kwa wateja.
NSSF shughulikieni tatizo la hicho mnachoita "mtandao" ili watu wapate huduma kwa wakati,wapeni semina wafanyakazi(hasa tawi la Ubungo kwa Dsm) namna ya kuongea na kuhudumia watu.Wawe na lugha nzuri kwa wateja.
Mfanyakazi mshahara mdogo na bado manyanyaso kwa NSSF makubwaaa,mtatuua walimu kwa stress jamani