...solutions ni very simple kill TANESCO monopoly,ruhusu fair play then create serious & independent regulatory body to enforce standards,safety,fairness etc,kwa sasa only TANESCO ndio anaweza kuuza umeme ile nchi hakuna mtu mwingine anaruhusiwa,no way serious investor ataweka billions zake on the line asubiri incompetent & corrupt TANESCO wamwambie namna ya kuuza umeme wake,hakuna cha NSSF wala serikali watatutoa gizani tukiendelea na sheria zetu,kill TANESCO monopoly then ruhusu fairplay is the only way.
Hivi hawa NSSF si warudi hatua chache tu nyuma kwanza waangalie ni nani anachangia huo mfuko (subscribers) na ana hali gani kimaisha na kimapato!!!!??? Inasikitisha, badala ya kujiingiza kwenye miradi yenye maswali mengi kama haya inayoweza kupelekea matatizo ya shirika huko mbeleni (tunaona serikari yenyewe ilivyo kosa mwelekeo kwa kujiingiza huko) na badala yake hicho kilichopo kwanza waweke subsidies (kama gawio vile) angalau 20% ya faida kwa wanachama. Maana nasikia wanasema wana akiba ya miaka 40 (40 years!!!???) wakati zaidi ya 70% wa wanachama wake (wachangiaji) hawana hata uhakika wa saving ya mwaka mmoja! Tutaona mengiNyie subirini tu...
Upande wangu sikutaka ku-deal na hili la Kiwira kwani tulipoanzisha ile kampeni ya kuirudisha Kiwira mikononi mwa Watanzania hatukuambiwa tunawaonea watu. Lakini sasa inaonekana wameamua kufanya wanavyotaka kufanya kwa sababu wanaweza.
400b kwa 300mw sio mpango mzuri wa muda mrefu ukichukulia kuwa ni makaa ya mawe!na uje huo umeme kwani mgao unaumiza sana uchumi.mipango ya muda mrefu ndiio itatoa ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hili
Hivi karibuni pamekuwepo Shinikizo la NSSF kutaka kuwekeza kwenye mradi wa Kiwira. Swali ninalojiuliza NSSF wana expertise gani katika masuala ya uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe? Swali la msingi ninalojiuliza je NSSF wanaye strategic partner mwenye ujuzi na uzoefu wa uendeshaji wa miradi ya aina hii? Kwa mujibu wa taarifa za kwenye media haionekani kama wanaye partner wa aina hiyo unless kama ni siri.
Uzoefu, unaonyesha Pension Funds zote duniani, huwa haziwekezi kwenye miradi mkubwa as lead investor. Mara nyingi Pension Funds zinawekeza kwenye miradi iliyo viable, na yenye wawekezaji wengine wenye uzoefu na aina ya shughuli inayofanyika. Wajibu wa Pension Funds ni ku identify miradi ambao ROI (Return of Investment) sio ya kutilia mashaka na risk iliiyo very minimal….kwani wanawekeza jasho la mfanyakazi ambaye analitegemea katika maisha yake ya baada ya kustaafu. Hivyo, NSSF ilipowekeza kwa kununua hisa za NMB zilizouzwa kwenye soko la Hisa nchini, au kwenye Unit Trust of Tanzania au miradi mingine yoyote iliyo lucrative kama vile TWIGA CEMENT, ilikuwa ni sahihi kabisa etc. Kwani tunajua microfinance industry inakua nchini; na tunajua harakati za ujenzi zinazidi kupanuka nchini hivyo demand ya cement kwa miaka mingi ijayo itakuwepo.
Uwekezaji kwenye miradi ya umeme ni very risky na ROI ni ya muda mrefu na endapo mipango thabiti nay a kueleweka haipo, inaweza kuwa mradi wa hasara kubwa. Hivyo idea ya NSSF kuwekeza as LEAD AND SOLE INVESTOR, ni wazo BAYA. Mtu yeyote anayelipigia debe wazo la aina hii….lazima atakuwa ana maslahi binafsi nyuma yake na sio maslahi ya PENSIONERS wanao contribute kwenye mfuko wao.
Isitoshe, NSSF wana track record ya kuchangamkia miradi mbalimbali as AS LEAD INVESTOR wakati hawana technical expertise katika eneo husika , matokeo yake mpaka leo miradi hiyo haija take-off. Chukulia mfano wa MRADI WA DARAJA LA KIGAMBONI…mpaka leo mwaka wa 5, bado upo kwenye makaratasi…na mpaka sasa wamekwishabadilisha Consultants mara mbili….na bado mradi haujulikani utaanza lini. Vivyo hivyo, NSSF hao hao….tokea miaka 4 iliyopita walisema wanawekeza kwenye mradi wa Hospitali (at least mradi huu walikuwa na strategic partner-Appollo Hospitals ya India); lakini kwakuwa wao ndio walikuwa LEAD INVESTOR, mpaka leo mradi huo hauja take-off; na majuzi wakati wa power crisis waliongelea mradi wa umeme wa dharura….mpaka leo (pamoja na udharura) hakuna lolote lililokwishafanyika.
Rai yangu kwa NSSF, waachane na papara za kuwekeza kila mahala simply b'se potfolio yao ni kubwa….hizo ni fedha za wafanyakazi…….wawe makini sana na maeneo wanayowekeza….sio leo wanarukia kununua majenereta ya umeme, kesho mchuchuma, kesho kutwa tutaambiwa wanataka kujenga airport……miradi hii haina tija kwa wanachama wenye mfuko wao.
For once, waweze kwenye miradi ambayo wananchama wake wanaweza kunufaika hata kabla ya kustaafu kama vile ujenzi wa low cost housing ambazo wanachama wake wanaweza kukopeshwa na kukatwa pole pole….walau wawe na security ya makazi…