NSSF kusitisha huduma ya matibabu ya mwanachama kutoka Shirika binafsi baada ya kustaafu haiingii akilini

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,580
4,262
Kwenye maadhimisho ya Mei Mosi nilisikia kitu cha ajabu sana kwenye risala ambacho naamini Muheshimiwa Rais hakukisikia vizuri kwani hakukitolea maoni yake.

Hivi inaingia akilini eti mfanyakazi wa shirika binafsi (Private) aliyekuwa anachangia michango yake kikamilifu huko NHIF akistaafu husitishiwa huduma ya matibabu yeye na mwezi wake?

Namaanisha tofauti na mfanyakazi wa uma (Public sector) ambaye huduma huendelea kwa yeye na mweza wake?

Natamani kupata ufafanuzi wa hili au pengine kuwekwe vigezo vyenye uhalisia tofauti na hapo, huu ni ubaguzi ambao unastahili kukemewa kwani kubahatika kupata nafasi chache za ajira Serikalini isiwe kigezo cha kututenganisha!

( Samahani) naomba kichwa cha habari kisomeke NHIF na sio NSSF)
 
Kuhusu matibabu,kubali makato ya bima ya afya ya Taifa (NHIF),utapata huduma za matibabu wewe na mwenza wako baada ya kustaafu.
 
Back
Top Bottom