Nssf kuanza kukopesha wanachama wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nssf kuanza kukopesha wanachama wake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by shadhuly, Mar 19, 2011.

 1. s

  shadhuly Senior Member

  #1
  Mar 19, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 141
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  NSSF kuanza kukopesha fedha wanachama wake Send to a friend Saturday, 19 March 2011 11:33 0diggsdigg


  [​IMG] Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa NSSF,Abubakar Rajabu

  Lauden Mwambona, Mwanza
  MFUKO wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), unaandaa utaratibu wa kukopesha wanachama wake fedha ili waweze kuzitumia kwa shughuli za kupambana na umaskini.
  Akizungumza jijini Mwanza juzi, Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa mfuko huo, Abubakar Rajabu, alisema hivi sasa mipango inaendelea NSSF kuwasaidia wanachama wa mfuko kwa kuwakopesha fedha kama wanavyofanya kwa kampuni za uwekezaji nchini.

  Rajabu alisema mfuko huo kwa sasa umemteua mtalaamu wa kuangalia utaratibu mzuri wa kukopesha wanachama, ili waweze kufanya kazi za maendeleo na kwamba, mpango huo unaweza kuanza kutekelezwa kabla ya miaka mitatu ijayo.

  "NSSF itaanza kuwakopesha wanachama wake baada ya kukamilika kazi ya mtalaamu anayeangalia namna bora ya kutoa mikopo hiyo bila kuathiri mipango ya mfuko," alisema na kuongeza kuwa mpango huo unalenga kusaidia mapambano dhidi ya umaskini kwa wanachama.

  Kwa siku tatu, Mwenyekiti huyo akiwa na wajumbe wengine wa bodi ya wadhamini wa NSSF, walifanya ziara mikoa ya Kagera na Mwanza kwa kutembelea Kiwanda Sukari Kagera, ambacho kilipata mkopo wa dola 15 milioni za Marekani kutoka katika mfuko huo.

  Naye Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk Ramadhan Dau, alisema mfuko umejiwekea mipango ya kupitia upya viwango vya mafao kila baada ya miaka mitatu.

  Dk Dau alisema kupitia mpango huo, mwaka huu, mfuko uliongeza mafao na wale waliokuwa wakipata kiwango cha chini cha Sh52,000 sasa watakuwa wakipata Sh80,000 kwa mwezi. Kufuatia mabadiliko hayo wapo wastaafu ambao wanapata Sh5 milioni kwa mwezi.

  Alisema kwa utaratibu huo, NSSF itaendelea kuwajali wanachama kila baada ya miaka mitatu kwa kuongeza viwango suala ambalo limekubaliwa kimataifa.

  SOURCE MWANANCHI I9 MARCH 2011
   
 2. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Safi -- huu ni mpango mzuri sana.

  Inatakiwa wabunge sasa watie nguvu ili huu mpango uharakishwe.
   
 3. Enigma

  Enigma Senior Member

  #3
  Mar 19, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 108
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  I don't know what it is, but there is definitely something fishy about NSSF.

  SLIDINGROOF despair not, just an observation!
   
 4. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2011
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mpango huo umechelewa sana, mfuko ulikuwa unawafaidisha zaidi watu na makampuni yasiyokuwa wanachama!
   
 5. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mikopo ni mizuri tatizo hapa kwetu bongo ni riba zisizojali hali halisi!
   
Loading...