NSSF: Kilio kilichokosa ufumbuzi. Wanyonge hunyongwa kimya kimya nchi ikijifanya haioni, sababu ni jambo linalogusa tabaka la waliotengwa na mfumo

concrete jungle

New Member
Dec 11, 2019
4
1
Habarini wakuu,

Ninaandika waraka huu nikiwa na maumivu makuu moyoni juu ya mahangaiko na misukosuko tunayopitia waathirika tuliopoteza ajira zetu katika kipindi hiki kigumu na kuamua kufungua madai ili kupata stahiki zetu NSSF tukiamini ndo hazina yetu iliyosalia itakayotukwamua katika kipindi hiki kigumu.

Bahati mbaya tumekutana na rungu zito lililokosa mtetezi kila mmoja akihisi alimuhusu kwa sababu bado yupo kazini.

Imekuwa ni kasumba mtu kuzungushwa miezi zaidi ya sita mpaka miaka bila kuona hata senti moja wafanyakazi wa NSSF wamegeuka miungu watu wanajibu wanavyojisikia kwa jeuri kubwa hasa hasa hizi ofisi za Dar Kinondoni na Ilala Boma.

Sijajua kwa mikoani lakini hali ni mbaya Tanzania nzima usiombe ukose ajira katika kipindi hiki cha awamu ya tano hakuna atayekujali AMANA YAKO ITAGEUKA SHUBIRI YAKO watoto, mke familia kwa ujumla italala njaa.

Maradhi, vifo na misukosuko yote ya kifamilia ambayo ingeweza kutatuliwa na akiba yako lakini wazandiki wameing'ang'ania na hawajali juu ya hilo wakiendelea kukurusha miezi mitatu mitatu mbele bila huruma wala kukufikiria.

Wengine utoka mbali kwa nauli za mikopo kuja kwenye ahadi ya wazandiki ahadi ya wanyori ahadi isiyokoma wala kutekelezeka masikini ya Mungu mnyonge huyu anapofika huambulia ahadi mpya isiyopungua miezi mitatu kuendelea na kule mkoani anaporudi hajui atalipa vipi ile fedha aliyokopa inatia huruma ndani ya nchi ya uzao wa mama na baba yako mabibi na mababu zako.

Ingekuwa vyema serikali ingekuwa wazi juu ya hili kwamba hakuna pesa hizo ili watu wajiandae kisaikolojia watu wamekubali ata wapewe hyo 33.3% ya mshahara wa mwisho lakini nao imekuwa kizungumkuti sasa mnataka waibe ili familia ile hali ya kuwa wana pesa zao halali?

tuwe na ofu ya Mungu juu ya hili hata kama tumeshika mpini siku moja tutafutika katika dunia hii ilojaa udhalimu usababishdwao na mababilon tuweke sheria zenye usawa na si kandamizi kwa tabaka la chini.

Kwa watu wasio na sauti wala kwa kusemea wakasikika wanasiasa wao huchukua chao mara tu wanapoitimisha muhula kwanini isiwe kwa matabaka yote?

Kuna watu walikuwa wameahidiwa mwezi wa 9, wa 9 wamerushwa wa 12 wa 12 wamerushwa wa 3 what the non sense of it?

AMANA YAKO INAGEUKA SHUBIRI YAKO tusikubali hili tushirikiane kwa pamoja hatuijui kesho yetu hata kama upo ndani ya ajira paza sauti kwa wanaopitia magumu aya ili kesho tusiendelee kumlea mdudu huyu bedui kwa formula ya divide and punish them no one will hear their voice because they are few.

MWISHO NAOMBA MWENYE NAMBA YA BRANCH MANAGER NSSF TEMEKE PAMOJA NA NAMBA YA WAZIRI JENISTA MHAGAMA AZIRELEASE HAPA KWA MSAADA ZAIDI AHSANTE.
 
Mkuu acha kunitonesha maumivu, miaka kadhaa nyuma ilibidi niache hela zangu huko. Sheria ya hovyo eti ukiacha kazi hupewi hela yako mpaka ufukuzwe. Nonsense.

Nakuomba usitegemee sana huko unajitafutia matatizo. Chukulia Hilo Kama gonjwa lisilo na Dawa jiandae kuishi nalo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unachosema ni sahihi lakin tusi-quit kiraisi zipo njia za kupambana haki haipotei inacheleweshwa tu.
 
Hawa watu ni wababaishaji sana lakini mimi ntazaa nao tu, niko nnje ya ajira mwaka wa pili nakimbizana nao ile pesa ni yangu na wala siwaombi mkopo NTAZAA NAO NA WATANILIPA TU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa watu ni wababaishaji sana lakini mimi ntazaa nao tu, niko nnje ya ajira mwaka wa pili nakimbizana nao ile pesa ni yangu na wala siwaombi mkopo NTAZAA NAO NA WATANILIPA TU

Sent using Jamii Forums mobile app
Duuh! Mwaka wa pili unafuatilia? Mbona wengine wanasema ukijaza fomu ya madai hata miezi miwili haiishi unapokea mzigo wako?
 
Wakati Fulani tatizo linakuwa lipo kwa Mwajiri kwa kutopeleka michango.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni tatzo dogo sana hilo. Kwa ujumla NSSF ni janga na hizi kanuni zao pamoja na utendaji wao wa ujivuni ipo siku isiyo na jina watakujajikuta sehem mbaya sana. Maana wapo mitaani na wanaowafanyia ujivuni tena kweny hela zao wamekata tamaa. Ogopa aliekata tamaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom