NSSF jirekebisheni; Sio busara kuchelewesha malipo kwa muda mrefu

pole sana ndugu, ni kweli unacho kilalamikia, ila tatizo sio mifuko bali watendaji walio pewa dhamana ya kuendesha na kusimamia mifuko hiyo.

Sio NSSF tu bali hata PSPF kuna matatizo makubwa, kuna baadhi ya watendaji wana chezea na kuchelewesha haki za watu.,

wanachama wana nyanyasika na kuzungusha kama vile wamekuwa ombaomba!!!! kumbe ni haki yao.

Waziri mwenye dhamana na mifuko hii ya hifadhi ya jamii anapaswa kufuatilia kero hizi za mara kwa mara na kuzitolea ufumbuzi wa kudumu.
Wanachama wachangiaji wanapaswa wafurahie akiba walio iweka sio kujutia!!!!
 
Nashukuru sifikirii kuajiriwa tena, ila nilisema endapo ningeajiriwa nikaambiwa akiba yangu inapelekwa NSSF wallahi naacha kazi. Nini hiyo ya Dar? Matusi yapo NSSF Dodoma tena yupo mama special kwa kujibu hovyo na kuchamba watu ati anasema "sisi (NSSF) tunawapa msaada tu" hivi huyu mama anaakili kweli? NSSF tambueni huo sio msaada ni makato ya lazima kutoka katika mishahara yetu sio msaada kutoka kwenu, hebu mpelekeni huyu mwanamke semina ya maadili angalau ajue jinsi ya kuhudumia wanachama wao, huyu mama atakuwa ni kabila fulani wale ambao wanaongea hawamezi mate, usiombe ukakutana na mdomo wa yule mama huli siku nzima. NSSF Dodoma jirekebisheni na anaye wachafua hasa ni huyu mama, idara zipo nyingi muhamisheni pale hafai. Halafu najiuliza kwani nyie NSSF nani kawaloga? Mbona mlikuwa na Huduma nzuri tu. Si bure kuna sababu
 
Back
Top Bottom