NSSF ipo taabani kifedha

Gulwa

JF-Expert Member
Jun 16, 2008
9,729
14,740
Nimepata taarifa kutoka kwa mtu wa ndani ya nssf kuwa hali ya mfuko huo kifedha ni mbaya sana kiasi cha kushindwa kulipa makandarasi wengi, na baadhi ya miradi hasa ya ujenzi kukwama.

Sababu kubwa inayotajwa kusababisha hali hiyo ni:

1.Serikali kukopa hela nyingi kutoka kwenye mfuko bila kurudisha.

2.Ufisadi mkubwa unaofanywa na viongozi waandamizi wa mfuko ambao wengi wamejilibikizia mali nyingi sana zilizopatikana kwa njia haramu.

Sisi wachangiaji tunazidi kuwa maskini, watu walipewa dhamana ya kutunza michango yetu wanakosa uaminifu.

 
Wabunge wa upinzani tunaomba muihoji serikali Bungeni kuhusu hili, wabunge wa CCM hawawezi hata kama wanaumia.

Mpaka sasa serikali imekopa kiasi gani NSSF?

Katika bajeti ya mwaka huu 2015/16 serikali imetenga kisai gani kupunguza deni la NSSF?

Liquidity ya mfuko wa NSSF iko je mpaka sasa? i.e. Uwezo wa kulipa mafao kwa wafanyakazi NOT assets.
 
Katika hii mada ya NSSF,jamani mtu akitaka kujitoa ambaye alikuwa voluntary inakuwaje na malipo huchukua muda gani? Tafadhalini wakuu
 
Lazima wafilisike tu. Huo wanaoita uwekezaji ni ufisadi tu. nyumba ambayo wangenunua kwa sh. milioni 60 Temeke wanainunua milioni 300. Unategemea nini?
 
Mama wee kaakiba kangu ka miaka 3 nssf kanapotea hivihivi?...ebu mtujuze vizuri wajameni
 
Gulwa

Mkuu umesahau sababu nyingine, Waziri wa ujenzi kuwaingiza mkenge kwenda kujenga daraja la Kigamboni (White Elephant) litakalo hudumia wakazi wasiozidi 150,000 kwa siku. Kweli hawa viongozi wetu balaa.
 
Last edited by a moderator:
GULWA
issue yako ilizungumziwa na mbunge wa chadema anaitwa Mhe.Cecilia Paresso akioji kuhusu huo mfuko ya kwamba serikali imeufilisi na kwamba serikali inatishia uhai wa shirika sasa kwa habari hii unathibitisha kutoka kwa wausika ndani kuwa nikweli hali ni mbaya.

TUMAINI MAKENE labda anaweza kuturudhishia ule uzi wa Mhe.Paresso kuhusu NSSF
 
Suala hili ingawaje mtoa mada hana reliable source ya habari yake lakini halina budi kufanyiwa uchunguzi haraka sana kuokoa fedha za michango ya wanachama wa mfuko huu,si la kupuuzwa abadani,linajirudia rudia sana,inawezekana kuna ukweli ndani yake
 
Alafu bado kuna watanzania wana imani na watangaza nia wa CCM!!

Siuji tumelogwa,tumelaniwa sipati majibu!!
 
Suala hili ingawaje mtoa mada hana reliable source ya habari yake lakini halina budi kufanyiwa uchunguzi haraka sana kuokoa fedha za michango ya wanachama wa mfuko huu,si la kupuuzwa abadani,linajirudia rudia sana,inawezekana kuna ukweli ndani yake

Mkuu nimepata kutoka reliable source ila siwezi kutaja hapa kwa sababu zinazoleweka
 
Alafu bado kuna watanzania wana imani na watangaza nia wa CCM!!

Siuji tumelogwa,tumelaniwa sipati majibu!!

Mwambieni Mbowe arudishe mkopo wa NSSF ambao amepanga kuwatapeli. Watu aina ya Mbowe ndio hao hao wanaoshiriki kuikwamisha mifuko yetu ya kijamii.
 
Mwezi wa September mwaka jana inasemekana hawa jamaa walikuwa hawana pesa kabisa,walishindwa kulipa wanachama wao mafao, hali ilikuwa tete sasa Ramo Dau ni lazima abananishwe kwenye hili, na hatatoka salama pale.
 
Sijawahi kuvutiwa na hotuba za wanaccm lakini juzi nilimpenda Mh. Sumaye kwa kiasi fulani alivyokuwa akielezea sakata la NBC. Alisema kuwa wao walitumia taarifa za regulator na sio taarifa za CEO wa NBC, akatoa mfano kuwa hata leo ukimuita CEO wa ATC atakwambia 'wanatengeneza faida' mpaka akija external auditor ndio utajua kuwa pale hakuna shirika.
Suala la NSSF ni gumu na naamini muda sio mrefu tutajua kuwa hakuna kitu bali madeni tu yanayozidi hata thamani ya majengo wanayomiliki. Hiyo itajulikana pale akija external auditor kama lilivyokuwa sakata la BoT na EPA against kampuni huru ya mahesabu.
 
Kimkopo cha Mbowe cha 76m. Ambacho kila akilipa anabadilishiwa hesabu hakiwezi kuwa sababu ya mfuko kufilisika.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom