Gurudumu
JF-Expert Member
- Feb 5, 2008
- 2,349
- 261
Ndugu zangu,
naamini wote mmefuatilia kwenye vyombo vya habari jinsi Dr. Magufuli na Dr. Harrison walivyoanza kazi jana Jumapili, siku moja tu baada ya kuapishwa. Katika magazeti ya leo, ujenzi wa daraja la Kigamboni ni mojawapo ya vipaumbele vya makamanda hawa wawili. Dr. Magufuli anadai maelezo kutoka NSSF ya kutojenga daraja la Kigamboni hadi leo na kama hawawezi waseme hivyo ili yeye akope pesa BoT na kulijenga.
Mimi siyo msekaji wa Dr. Magufuli wala wizara ha ujenzi. Lakini naomba nitumie taarifa zilizo wazi kwa jamii (public) kuonesha ni kwa nini Magufuli anataka maelezo kutoka NSSF.
Ujenzi wa daraja la Kigamboni uko kwenye Ilani za Uchaguzi za CCM za mwaka 2000 na mwaka 2005. Sina nakala ya Ilani ya 2000 lakini ukirejea ukurasa wa 54 wa Ilani ya 2005 utaona hii ahadi. Lakini Hansard ya Bunge ya tarehe 3 Agosti 2007 inawakumbusha Wabunge na Watanzania kwamba ahadi ya ujenzi wa daraja hili ilikuwepo hata kabla ya Ilani ya 2000. Bahati mbaya Mbunge aliyetamka haya maneno hakutaja mwaka hasa ambao ahadi hii ilianzishwa na CCM.
Hansard mbali mbali za 2006 na 2007 zinaonesha Wabunge, hasa wa Dar es Salaam (Zungu na Msomi) wakiulizia maendeleo ya ujenzi huu mara kwa mara. Kila mara wanajibiwa majibu ambayo hasa hayana mshiko.
Lakini tarehe 3 Agosti 2007 Wabunge hawa wakiungwa mkono na wenzao wengi walitia pressure kubwa na serikali ililazimika kujibu kikamilifu.
Kwamba NSSF ilianza upembuzi yakinifu 2003 uliogarimu dola za kimarekani 20,000, ambazo zililipwa kwa Howard Humfrey. Mwaka 2004 wakafanya upembuzi wa kina kwa garama ya dola 230,000. Kisha serikali ikasema kwa kuwa CCM imeliweka daraja hili tena kwenye Ilani yake ya 2005, basi ni lazima litajengwa na mchakato umefika mahali pazuri.
Awali Hansard ya 1 Agosti 2007, Waziri wa Kazi Ajira na Maendeleo ya Vijana alijibu swali Bungeni kwamba daraja litajengwa kwa sababu tayari Waraka wa Baraza la Mawaziri umeshatayarishwa. Kwamba waraka huo umeshapita kwenye ngazi ya Sekretariati ya Baraza la Mawaziri. Kinachosubiriwa ni Waraka huo ufike kwenye Baraza la Mawaziri na ambalo kama likiridhika litamshauri Rais aagize kuanza ujenzi wa daraja hilo la Kigambani. Waziri alisisitiza kwamba daraja hili litajengwa kabla ya 2010, kama ilivyoahidiwa kwenye Ilani ya CCM ya 2005.
Mheshimiwa Zungu aliibana serikali zaidi ieleze gharama za hili daraja na kama ni kitu ambacho serikali kweli imeshindwa kujenga. Alijibiwa tarehe 3 Agosti 2007 kwamba garama za kujenga daraja la Kigamboni ni Euro millioni 45 ambazo ni sawa na Shilingi billioni 91. Pia akaarifiwa kwamba Euro milioni 22.5 zitatolewa kama msaada na serikali ya Uholanzi.
Baadaye NSSF walitoa Tangazo kwene magazeti wakialika makampuni binafsi yenye nia ya kuingia ubia na NSSF katika ujenzi wa daraja la Kigamboni. Baada ya hili tangazo (bado nalitafuta nitaweka tarehe yake hapa) sijaweza kupata taarifa zaidi kuhusu mchakato wa ujenzi wa daraja hili. NSSF hawakuweka bayana ni makampuni mangapi na uwezo wao walioomba ubia huo. Serikali pia haijazungumzia tena na pengine Wabunge pia hawaja uliza tena kwani kwenye Hansard sijaweza kupata taarifa yoyote.
Ni kwa sababu hizi hapa juu naamini kwamba NSSF wana maelezo kwa nini daraja hili halijajengwa. Pia ni kutokana na Dr. Magufuli kuwataka wajieleze natamani kuamini kwamba pengine serikali ilikwisha kabidhi ujenzi wa daraja hili kwa NSSF.
Kama NSSF hawahusiki, watueleze nani alikwamisha huu mradi. Kama kuna ufisadi ulijipenyeza, tunaomba Dr. Magufuli na kamanda wake msaidizi Dr. Harrison waweke mambo hadharani ili iwe rahisi kwao kulishuhulikia tatizo hili.
Nimalizie kwa kuwatahadharisha hawa makamanda wawili (Dr. Magufuli na Dr. Harrison) kwamba kama walitoa hii kauli kama mtaji tu wa kutafuta cheap popularity ya kuanzia kazi, kuna watu wanafuatilia, na tutalifuatilia kwa nguvu zetu zote. Lakini itoshe kuwahakikishia kwamba tunawaunga mkono katika hatua hii ya awali.