Nssf ieleze wananchi sababu kutojenga daraja la kigamboni

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
1,195
Ndugu zangu,

naamini wote mmefuatilia kwenye vyombo vya habari jinsi Dr. Magufuli na Dr. Harrison walivyoanza kazi jana Jumapili, siku moja tu baada ya kuapishwa. Katika magazeti ya leo, ujenzi wa daraja la Kigamboni ni mojawapo ya vipaumbele vya makamanda hawa wawili. Dr. Magufuli anadai maelezo kutoka NSSF ya kutojenga daraja la Kigamboni hadi leo na kama hawawezi waseme hivyo ili yeye akope pesa BoT na kulijenga.

Mimi siyo msekaji wa Dr. Magufuli wala wizara ha ujenzi. Lakini naomba nitumie taarifa zilizo wazi kwa jamii (public) kuonesha ni kwa nini Magufuli anataka maelezo kutoka NSSF.

Ujenzi wa daraja la Kigamboni uko kwenye Ilani za Uchaguzi za CCM za mwaka 2000 na mwaka 2005. Sina nakala ya Ilani ya 2000 lakini ukirejea ukurasa wa 54 wa Ilani ya 2005 utaona hii ahadi. Lakini Hansard ya Bunge ya tarehe 3 Agosti 2007 inawakumbusha Wabunge na Watanzania kwamba ahadi ya ujenzi wa daraja hili ilikuwepo hata kabla ya Ilani ya 2000. Bahati mbaya Mbunge aliyetamka haya maneno hakutaja mwaka hasa ambao ahadi hii ilianzishwa na CCM.

Hansard mbali mbali za 2006 na 2007 zinaonesha Wabunge, hasa wa Dar es Salaam (Zungu na Msomi) wakiulizia maendeleo ya ujenzi huu mara kwa mara. Kila mara wanajibiwa majibu ambayo hasa hayana mshiko.

Lakini tarehe 3 Agosti 2007 Wabunge hawa wakiungwa mkono na wenzao wengi walitia pressure kubwa na serikali ililazimika kujibu kikamilifu.

Kwamba NSSF ilianza upembuzi yakinifu 2003 uliogarimu dola za kimarekani 20,000, ambazo zililipwa kwa Howard Humfrey. Mwaka 2004 wakafanya upembuzi wa kina kwa garama ya dola 230,000. Kisha serikali ikasema kwa kuwa CCM imeliweka daraja hili tena kwenye Ilani yake ya 2005, basi ni lazima litajengwa na mchakato umefika mahali pazuri.

Awali Hansard ya 1 Agosti 2007, Waziri wa Kazi Ajira na Maendeleo ya Vijana alijibu swali Bungeni kwamba daraja litajengwa kwa sababu tayari Waraka wa Baraza la Mawaziri umeshatayarishwa. Kwamba waraka huo umeshapita kwenye ngazi ya Sekretariati ya Baraza la Mawaziri. Kinachosubiriwa ni Waraka huo ufike kwenye Baraza la Mawaziri na ambalo kama likiridhika litamshauri Rais aagize kuanza ujenzi wa daraja hilo la Kigambani. Waziri alisisitiza kwamba daraja hili litajengwa kabla ya 2010, kama ilivyoahidiwa kwenye Ilani ya CCM ya 2005.

Mheshimiwa Zungu aliibana serikali zaidi ieleze gharama za hili daraja na kama ni kitu ambacho serikali kweli imeshindwa kujenga. Alijibiwa tarehe 3 Agosti 2007 kwamba garama za kujenga daraja la Kigamboni ni Euro millioni 45 ambazo ni sawa na Shilingi billioni 91. Pia akaarifiwa kwamba Euro milioni 22.5 zitatolewa kama msaada na serikali ya Uholanzi.

Baadaye NSSF walitoa Tangazo kwene magazeti wakialika makampuni binafsi yenye nia ya kuingia ubia na NSSF katika ujenzi wa daraja la Kigamboni. Baada ya hili tangazo (bado nalitafuta nitaweka tarehe yake hapa) sijaweza kupata taarifa zaidi kuhusu mchakato wa ujenzi wa daraja hili. NSSF hawakuweka bayana ni makampuni mangapi na uwezo wao walioomba ubia huo. Serikali pia haijazungumzia tena na pengine Wabunge pia hawaja uliza tena kwani kwenye Hansard sijaweza kupata taarifa yoyote.

Ni kwa sababu hizi hapa juu naamini kwamba NSSF wana maelezo kwa nini daraja hili halijajengwa. Pia ni kutokana na Dr. Magufuli kuwataka wajieleze natamani kuamini kwamba pengine serikali ilikwisha kabidhi ujenzi wa daraja hili kwa NSSF.

Kama NSSF hawahusiki, watueleze nani alikwamisha huu mradi. Kama kuna ufisadi ulijipenyeza, tunaomba Dr. Magufuli na kamanda wake msaidizi Dr. Harrison waweke mambo hadharani ili iwe rahisi kwao kulishuhulikia tatizo hili.

Nimalizie kwa kuwatahadharisha hawa makamanda wawili (Dr. Magufuli na Dr. Harrison) kwamba kama walitoa hii kauli kama mtaji tu wa kutafuta cheap popularity ya kuanzia kazi, kuna watu wanafuatilia, na tutalifuatilia kwa nguvu zetu zote. Lakini itoshe kuwahakikishia kwamba tunawaunga mkono katika hatua hii ya awali.
 
Kinyambiss

JF-Expert Member
Dec 2, 2007
1,374
1,225
Ujenzi unaanza Feb 2011. Magufuli aache kutafuta cheap popularity. Its not even under his mandate
 
Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
1,195
Ujenzi unaanza Feb 2011. Magufuli aache kutafuta cheap popularity. Its not even under his mandate

Mkuu, tunashukuru kwa taarifa za muda wa kuanza ujenzi wa daraja la Kigamboni. Tunaomba tafadhali tuarifu zaidi;

1. Kwa kuwa Feb ni miezi miwili tu ijayo, ni maandalizi gani ambayo tayari imeshafanyika hadi sasa?

2. Nini kilichelewesha kuanza ujenzi wa daraja hili?

3. Ni garama kiasi gani zitagarimu ujenzi wa daraja hili hadi kupitika?

4. Pesa zinatolewa na nani?

5. Kampuni gani iliyopewa tenda ya kujenga daraja hili?

6. Je, unaweza kutupatia ramani ya daraja hilo?
 
Dedii

Member
Aug 16, 2010
76
70
Duh kweli bongo is bongo, yaani miaka yote tumeishi kwa tabu kigamboni eti kwa sbb 91 bilion!! ina maana lowasa anapesa kushinda serikal? amewezaje kuanzisha ujenzi wa 70 b, ilihali alikuwa muajiliwa wa hiyo sirikali iliyoshindwa ujenzi wa daraja la 91b kwa miaka 49. hongereni sirikal.
 
haya ndiyo maswali ya kujiuliza. kwamba sababu ilikuwa ni kukosekana pesa au nia? mchakato haukufika mwisho kwa sababu gani?
 
Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
1,195
Hali ilivyokuwa Ferry Kigamboni tarehe 29 November 2010 siku moja tu baada ya Dr. Magufuli kutoa kauli kwamba NSSF wajieleze kwa nini daraja la Kigamboni halijajengwa

kigamboni ferry 058.jpg kigamboni ferry 034.jpg kigamboni ferry 064.jpg
 
The Finest

JF-Expert Member
Jul 14, 2010
21,617
1,225
Ujenzi unaanza Feb 2011. Magufuli aache kutafuta cheap popularity. Its not even under his mandate

Ndio wabongo tulivyo ukitaka kufanya kazi na kujua kitu kinaendaje unaambiwa cheap popularity na hiyo Feb 2011 unayosema i doubt pia
 
The Finest

JF-Expert Member
Jul 14, 2010
21,617
1,225
Ujenzi unaanza Feb 2011. Magufuli aache kutafuta cheap popularity. Its not even under his mandate

Mkuu, tunashukuru kwa taarifa za muda wa kuanza ujenzi wa daraja la Kigamboni. Tunaomba tafadhali tuarifu zaidi;

1. Kwa kuwa Feb ni miezi miwili tu ijayo, ni maandalizi gani ambayo tayari imeshafanyika hadi sasa?

2. Nini kilichelewesha kuanza ujenzi wa daraja hili?

3. Ni garama kiasi gani zitagarimu ujenzi wa daraja hili hadi kupitika?

4. Pesa zinatolewa na nani?

5. Kampuni gani iliyopewa tenda ya kujenga daraja hili?

6. Je, unaweza kutupatia ramani ya daraja hilo?

Mkuu naomba utujibie hayo maswali hapo juu since unajua ujenzi utaanza Feb 2011 na majibu ya hayo maswali utakuwa nayo i guess.
 
.

Jamani tunaomba majibu ya haya maswali, na kwa nini NSSF hawajamjibu Magufuli?
 
Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
1,195
Jamani mbona hatujasikia majibu ya nssf kuhusu hili daraja? Je, magufuli alikuwa anatisha nyau au amekutana na kisiki?
 
TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
22,598
2,000
Ujenzi unaanza Feb 2011. Magufuli aache kutafuta cheap popularity. Its not even under his mandate
wewe una matatizo makubwa sana ya uelewa...

Ujenzi umechelewa for more than 6 years and then you come with disco lights to talk of feb 2011 ati ni kutafuta cheap ppopularity?? i think you are the one looking for cheap popularity

ungekua unaishi kigamboni usingesema hayo

Hivi unajua kwamba hata signature zilishapitishwa lakini anko wako akabana?
 
TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
22,598
2,000
Mkuu, tunashukuru kwa taarifa za muda wa kuanza ujenzi wa daraja la Kigamboni. Tunaomba tafadhali tuarifu zaidi;

1. Kwa kuwa Feb ni miezi miwili tu ijayo, ni maandalizi gani ambayo tayari imeshafanyika hadi sasa?

2. Nini kilichelewesha kuanza ujenzi wa daraja hili?

3. Ni garama kiasi gani zitagarimu ujenzi wa daraja hili hadi kupitika?

4. Pesa zinatolewa na nani?

5. Kampuni gani iliyopewa tenda ya kujenga daraja hili?

6. Je, unaweza kutupatia ramani ya daraja hilo?

Mkuu naomba utujibie hayo maswali hapo juu since unajua ujenzi utaanza Feb 2011 na majibu ya hayo maswali utakuwa nayo i guess.
kazin.. achana na kinyambiss, ni uvuvuzela tupu unakisumbua

we kula bia yako mkuu... wako wengi hao

ati wanaanza ujenzi wakati hata eneo halijawa paved
 
TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
22,598
2,000
FYI by 2005 hii pesa ya dowans ingeweza kujenga madaraja matatu ya kigamboni
 
BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,521
2,000
hakuna deal zuri la kifisadi kama kununua au kurepea kivuko!hapo jamaa wa tamesa hupata pesa ya kutakata!ndio maana vivuko hununuliwa haraka sana!daraja ni permanent solution na nchi inapenda solutions za kula pesa tuu mara kwa mara!daraja kigamboni sahau mpaka ccm itoke madarakani
 
Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
1,195
FYI by 2005 hii pesa ya dowans ingeweza kujenga madaraja matatu ya kigamboni

pesa zetu halali wanafisadi halafu wanatutia kwenye madeni zaidi kwa kutafuta wawekezaji kuleta maendeleo. hivi kwa nini serikali hung'ang'ania madarakani kama kweli nchi ni maskini? priority is never wananchi.
 
Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
1,195
hakuna deal zuri la kifisadi kama kununua au kurepea kivuko!hapo jamaa wa tamesa hupata pesa ya kutakata!ndio maana vivuko hununuliwa haraka sana!daraja ni permanent solution na nchi inapenda solutions za kula pesa tuu mara kwa mara!daraja kigamboni sahau mpaka ccm itoke madarakani

makes sense, tutawatoa tu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom