NSSF ichunguzwe na TAKUKURU na Wizara ya Fedha kuhusu harufu ya ufisadi na rushwa

kishegheni

Member
Mar 6, 2012
17
75
NSSF imeteua Kampuni binafsi ya PROPER CONSULT kusimamia majengo yake na kuwataka wapangaji kufanya malipo kwenye Akaunti binafsi ya Kampuni hiyo iliyoko CRDB kinyume maelekezo ya Serikali kuwa malipo yote ya Serikali yafanyike kwa kutumia Control Number ili pesa zote ziingie Serikalini.

Hapa kuna harufu ya ufisadi.

1) NSSF wameteua kampuni kusimamia majengo bila kufuata Sheria ya manunuzi ya umma ya kupata hii Kampuni, hivyo kuna dalili ya rushwa.

2) NSSF wamekuwa kila mwaka wanatenga kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya matengenezo ya nyumba zake na zinatumika lakini matengenezo hayafanywi ndani wala nje, wapangaji wanaambiwa wafanye matengenezo wenyewe. Swali ni kuwa hizo pesa za matengenezo zinatumika kufanyia nini kama sio ufisadi.

Shirika hili la umma linapaswa kuchunguzwa na Takukuru na wizara ya Fedha kuhusu ufisadi huu na harufu ya rushwa.
 

REJESHO HURU

JF-Expert Member
Mar 6, 2014
3,016
2,000
Yani Serikali ijichunguze nakusihi tu tarehe 28 October 2020 usifanye makosa kura yako muhimu sana.
 

dyuteromaikota

JF-Expert Member
Apr 30, 2013
4,589
2,000
Hera za nssf hazipaswi kuingia serikalini maana ni hera za wanachama na sio za serikali. Kama kuna matumizi mabaya hapo sawa wahusika wawajibishwe.
 

saulejerry

New Member
Sep 30, 2015
1
45
Taarifa hizi ni za upotoshaji na hazina ukweli wowote. Hii ni kwa kuwa kampuni za usimamizi majengo zinafanya kazi za Property & Facilities Management kwa mujibu wa sheria za nchi yetu na uteuzi wake kusimamia baadhi ya majengo ya NSSF umefanyika kwa mujibu wa sheria za manunuzi ya UMMA (PPA) na si kama ilivyoelezwa kwenye ukurasa huu kwa lengo la upotoshaji.

Kampuni hii inafanya usimamizi wa baadhi ya majengo( investment properties) za NSSF( mfuko ) na mojawapo ya kazi za Property and Facilities Manager ni kuhakikisha kuwa wapangaji wote wanapanga na kukaa kwenye nyumba za Mfuko kwa kufuata taratibu na sheria za nchi yetu. Pia, wapangaji wanatakiwa kulipa kodi kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa kmkataba.

Kodi zote za pango la nyumba zinalipwa kwa kutumia control number kwenda kwenye akaunti ya NSSF. Pamoja na ulipaji wa kodi ya pango, wapangaji pia wanatakiwa kulipia gharama za huduma mbalimbali katika jengo (service charge) kwa lengo la kuhakikisha huduma hizo kama maji, umeme, huduma za lifti, usafi nk zinapatikana.

Pesa hizi zinakusanywa na Property Manager kwa niaba ya NSSF kupitia kwenye akaunti ya service charge kuhakikisha huduma hizi zinapatikana kwa haraka. Malipo ya huduma ni tofauti na malipo ya pango la nyumba (Rent).

Matumizi ya fedha hizi za huduma yana kaguliwa na wakaguzi (Auditor) wa ndani na nje ya Mfuko na report inawekwa wazi kwa Mfuko na wapangaji pia.

Tunawaomba wananchi wazipuuze taarifa hizi kwa kuwa hazina ukweli wowote
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom