NSSF chakula ya mafisadi: Dk. Dau acha usaniii, Watanzania tutakushukia kwa maandamano! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NSSF chakula ya mafisadi: Dk. Dau acha usaniii, Watanzania tutakushukia kwa maandamano!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MPadmire, Oct 26, 2012.

 1. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Dk. Ramadhani Dau ni msanii, anaongea utafikiri yuko Marekani.Eti ILO iliweka standard ya malengo ya mafao. Tanzania ajira ni maghumashi, sekta binafsi ni mbovuu..... unyanyasaji na ajira za mashakaaa.

  Fao la kujitoa kwa NSSF ni lazima kwa private sector.

  Kwanza Serikali kupitia wizara ya kazi ni Butu... Imeshindwa yafuatayo

  A - Kusimamia ongezeko la mshahara kwa private sector lilitolewa kati ya mwaka 2008...

  B- TUCTA nayo mbumbumbu

  C- Makampuni binafsi yameiweka serikali mfukoni, makampuni yanachangia kampeni za Thiciem. Kwa hiyo makampuni binafsi ni kandamizi, saa yoyote mfanyakazi anatimuliwa kazini, jeee asubiri mafao hadi afikishe miaka 55. Atalipaje kodi ya nyumba ama kula nini achilia mbali kuugua wakati hana mshaharaa??? .... Fao la mafao kwa NSSF ni lazima, ni hela zetu. .... Wewe Dr. Ramadhani Dau usichezee hela zetu.... Tunaungana wafanyakazi na hela zetu utatoa ku.dada.deki.

  D- Sasa inakuwaje wafanye mabadiliko kwa PPF na sio kwa NSSF> Hapa kuna jambo. Kuna njama na wiziiiiiiii.
   
 2. Endangered

  Endangered JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 929
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu MPadmire, hayo mabadiliko kwa PPF ni yapiu hayo, naanza kuhisi kizunguzungu mbona.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. m

  mdunya JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 7, 2012
  Messages: 765
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kitaeleweka tu! We need our money.
   
 4. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Dau ni mjasililamali anayejenga majengo ya bei mbaya na kudai ni ya walalahoi. Ama kweli Bongo hata mtu awe na PhD ni upuuzi kwa walio wengi aina ya Dau.
   
 5. K

  Kifarutz JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2012
  Joined: Aug 7, 2012
  Messages: 1,694
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Plan A ni kuwatuma wabunge bungeni kwenda kutengua huu uozo in the coming parliamentary sessions. Hiki ni kipindi muhimu kwani tutawajua wabunge wepi ni wasaliti. Wakishindwa kuitengua hii taka mwili then kifuatacho kiwe ni mgomo usio dhaifu nchi nzima ambao kikomo chake ni kurejeshwa kwa fao letu. Halafu wale wabunge wasaliti tuwashughulikie in 2015 election. Ni ujinga kwa serikali kung'ang'ana na hela ambazo siyo zake. Hii serikali ni ma.vi kabisa..!
   
 6. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2012
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Duh! hivi watanzania mlikuwa bado hamjui usanii ulioko NSSF? Kufanya mabadiliko ya sheria hii ni mpaka CCM itoke madarani maana NSSF inaibeba miradi mingi ya serikali na CCM hivyo si lahisi sana wabunge wa CCM kufanya maamuzi hayo.
   
 7. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Watanzania ni wanyonge, jamani hata wafanyakazi angalau wamesoma nao wanakuwa waoga. Au kwa nini tunakosa umoja na mshikamano tutetee haki zetu.

  Nani ambaye hajapata zile message za watoto wa vigogo katika chaguzi za Chaoo. Je kwa nini tena tusihamasishane kwa sms tena na tukapata mafao yetu ya kujitoa.
   
 8. a

  adolay JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,567
  Likes Received: 3,026
  Trophy Points: 280
  Kinachoendelea NSSF na kwingineko, ni UFISADI uliokomaa ukapevuka na kupevuka kisha kuvuka hata mipaka ya kuudhibiti uchu na urafi wa fedha za maskini wachache watanzania kwa visingizo visivoingia akilini, wakiwaacha watanzania sehemu kubwa bila msaada wowote kwenye umri huo nazaidi wakifa kwa njaa, kukosa matibabu na malazi hafifu. Hii sio huruma ila ni ujambazi wa mchana kweupe.

  inawezekana huko kwa wenzetu kwasababu wametengeneza mazingira mazuri inapotokea mwanachama kakosa ajira, hapa kwetu haiwezekani kabisa.Hakuna mazingira yaliyoandaliwa kumfanya mwanachama aishi kwa amani/matumaini akipata huduma za lazima hasa baada ya kuacha au kuachishwa kazi akiwa na umri chini ya miaka 55.

  Huyu Dau nilimtazama mara mbilimbili wakati akisema anasimamia sheria uso wake ulionesha dharau, kejeri na kiburi ndani yak. Hana aibu hata huruma ni fisadi fulani vile.

  1. Sina kazi, watoto wangu wamerudishwa nyumbani kutoka shule hawajalipa ada, Dau na serikali yake wanasimamia sheria ipi? sheria! watoto wao wanasoma, wangu wanasubili kuwa vibaka nyumbani? je hayo mafao yanafaidagani basi kwangu nafamilia yangu?


  2. Ni vipi nitaendelea kusubili hiyo miaaka 55 itimie sina mtaji, wala mradi wowote kuniwezesha kuishi kwa matumaini kufika huko? watalipa kwa kaburi langu, maana kufa ni lazima sina cha kunifanya niendelee kuishi bila kula wala afya bora . hapa kwetu siku hizi afya bora inapaikana nje ya inchi hususani India.


  3. Tuna wakulima na wasio nakazi zaidi ya 70%, hawa tunawaona kila siku wakizeeka wakiuguwa na kufa. serikali inatoa mafao gani kwa vikongwe endapo msingi ni kuwafanya waishi bila kutaabika? Je sera hapa ni kuhami matatizo ya uzeeni au kutuibia mafao yetu. (Ningekubaliana na sheria hiyo endapo kundi hilo la wakulima wangekuwa wanapewa chochote)

  4. Dau kama yeye ameshiba na anaakiba yakutosha, asitupangie lini tuchukuwe mafao yetu sisi wenye njaa na ambao kila siku inapokucha ni afadhari ya jana, Dau ni mnafiki maana anajuwafika serikali imeufilisi mfuko wake! alikuwa wapi kutueleza haya hapo kabla? na ilikuwaje walilipa hapo kabla hii sheria waliweka pembeni kwa misingi gani kama sio mazingira yetu kiuwezo shirika kushindwa kukidhi baadhi ya mahitaji ya msingi kwa wanachama wake?


  Tuwasubuiri wabunge waingie mkenge wa huyu pumbavuu Dau, tutaonana huku mitaani, adhabu ya kubaka na kuiba akiba zetu sio tu zitawatowa katika viti vyao vya ubunge, lakini kila mwanachama mpenda haki wa hii mifuko lazima tulipize visasi kwa wabunge vya aina yoyote ile, iwe ni kwa kutumia silaha au sumu vyovyote vile watakuja kuomba kura 2015. haiwezekani wao (wabunge) baada ya miaka yao mitano pale bungeni wanachukuwa mafao yao kwanini nawao wasisubili at 55 au zaidi???
   
 9. D

  Do santos JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2012
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 470
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  hapa hakuna hoja kuna chuki binafsi dhidi Dr Dau,ni chuki dhidi ya mafanikio yake.Jiulize kabla ya kulaumu hiko unacholalamikia yeye ndo amekiweka/amekitunga au la?
  Tatizo jf siku hizi ni mkumbo kwa kwenda mbele.Mtu mmoja akilaumu wengine nao wanaiga bila ya kujua yupo sahihi au la.Hakuna yoyote anayeweza kuandamana ni kelele tu.Wenye kuandamana wanajulikana
   
 10. a

  adolay JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,567
  Likes Received: 3,026
  Trophy Points: 280
  Mkuu chuki gani?

  1. Hivi anaezuia fedha ya mwingine ni sisi au yeye na serikali yake? nani mwenye roho ya korosho hapo?

  2. Mshahara wake na marupurupu yake si anapata kweni tumeongelea hayo? na kama sio ni chuki gani unayoongelea wewe?

  3. kama anahuruma na maisha yetu tukifikia uzeeni tupe mkakati wa serikali kwa wasio na mishahara hususani wakulima maana na wao wanachangia katika pato na maendelo ya taifa? uzeeni serikali inawasaidiaje?

  4. kama niwewe inakuwaje unapokuwa na fedha yako imedhibitiwa NSSF na hakuna namna yoyote ya kukuwezesha kuishi wakati huna kazi kwa maana ya malazi, chakula nk tupe matazamo wako mkuu ukizingatia ulinganifu wa chuki zetu kwa huyo mpuuzi Dau. ndo kusema mtu afe na akifa nini faida ya akiba yake?
   
 11. G

  Gulwa JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2012
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 2,786
  Likes Received: 1,963
  Trophy Points: 280
  Dr Dau kwa wasiomjua ni miongoni mwa mabilionea wa kurisha hapa nchuini. Amekuwa waklala wa ccm ktk kuchukua michango kutoka kwa makandarasi mbalimbali wakati wa uchaguzi, amejinufaisha kwa pesa za miradi mbalimbali ya ujenzi ya nssf, kuna mhandisi wa nssf aliye karibu naye sana amejenga hotel yenye thamani ya mabilioni maeneo ya makumbusho. ningewweza kumwaga wizio mkubwa alioshiriki klwenye miradi kama vile jengo la bunge, udom, mafuta house, ubungo plaza............
   
 12. Ryaro wa Ryaro

  Ryaro wa Ryaro JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 2,663
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Ni Mwenye Phd FEKI tu ndiye anayeweza kuunga mkono swala la Kutojitoa kwenye mifuko hii ya SSRA, Jamani siku Bunge lilkishindwa kutupa kutusaidia kuondoa sheria hii Kandamizi ndo siku tuamue Kupamabana KUFA NA KUZIKWA.
  Haiwezi kuingia akilini kuwa mwanachama uchukue fedha pale tu anapofikisha miaka 60. Kwanza Life span ya mtanzania ni chine ya miaka 50. Je hiyo 60 ni wapi na wapi?
  Je wale wasiokuwa na kazi ambao ni zaidi ya 75% nani atawatunza wakizeeka?
  Watanzania wenzangu ni MUDA mwafaka wa KUFIA haki yetu kwani hata kuishi Hakutakuwa na Faida kama pesa yako hautaitumia eti kuna mtu anakujali sana ukiwa mzee.
  Tupewe pesa yetu tufanye ujasiliamali (Entrepreneurship) na ni hizi fedha ndo mtaji wetu.
  Ngoja tuwasubiri na kwa kuwa wameonyesha Lobbying za hao wakina DAU muda si mrefu zitajulikana mbivu na mbichi.
  NYIE CHUKUENI FEDHA BENKI KUU, EPA, sijui DEEP GREEN lakini hizi zetu MTATUA ili MZILE MZILE Tukiwa TUMELALA MAUTI.
   
 13. T

  Trueman Member

  #13
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 11, 2012
  Messages: 88
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sasa km anapinga fao la kujitoa mkataba wa ajira ukiisha inakuaje atang'ang'ania hela zako? Ni Dr wa nini huyu
   
 14. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Matter of time tu, lazima hela zetu tuchukue otherwise watoe option tuamishe pesa zet ziende gepf, dr dau umedandia treni kwa mbele sqga la fao la kujitoa analijua utouh... dr dau na jeikei mmefilisi mifuko ya hifadhi, lazima tutagawana majengo ya nssf yote tunayajua tutaanza kuyalipua moja moja.
   
 15. a

  adolay JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,567
  Likes Received: 3,026
  Trophy Points: 280

  Hawa ndo wasomi wetu, wanaotanguliza ubinafsi na kukalia PHD zao.

  Kesha pewa zake na serikali kwenye mikataba feki na mikopo ya kuendesha ccm na analeta ukilaza na unafiki wake kwetu.

  Tuna wapuuzi wengi wa aina hii wanaokwenda kwa kuburuzwa kwa kamba ya serikali ya ccm na kuweka pembeni elimu zao.

  Huyu DAU ni Fisadi tu kama mafisadi wengine, atueleze mikakati yake kwa wasionacho kama wakulima yeye na serikali yake wanampango gani? Je serikali inabagua? kama sio ubaguzi wakulima hawazeeki? kama wanazeeka na hakuna mkakati wowote kwanini tusiamini wanatuibia mchana kweupe?
   
 16. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Kweli hawa CCM aliyeshiba hamjali mwenye njaa. Nani awaachie hela yake kwa miaka 30 halafu aje kupata mafao ya Shs 50,000 kwa mwezi kama wanazopata wazee wetu kwa sasa. This is bulshit, nashangaa Zitto na kamati yake wameishia kuchekacheka tu badala ya kumbana huyu bazazi Dau kuhusu hela zetu. Mashinikizo yote ya kuzuia mafao ni njama za Dau baada ya kushindwa kuisimamia NSSF yake.
   
 17. Ushimen

  Ushimen JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 24, 2012
  Messages: 12,837
  Likes Received: 12,822
  Trophy Points: 280
  kaka ukosahihi, lakini kinacho nishangaza sisi watingaji wa migodini tunaongea saana pasipo kuchukua hatua. TUKIUNGANA TUNAWEZA, Tuchukuwe hatua na maamuzi magumu.
   
 18. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Hii serikali ya mafisadi wanapima upepo, wakiona tunalegea tu imekula kwetu. Tuanze sasa kujenga mshikamano na mkakati. Maandamano makubwa na migomooo
   
 19. Anthonio

  Anthonio JF-Expert Member

  #19
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 26, 2012
  Messages: 202
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Shida ya viongozi wetu, wanapotaka kujinufaisha na kutunyonya mfano mzuri kwao ni Ulaya na mashirika ya kimataifa. Dk akitaka kuondoa fao la kujitoa aishauri serikali ifute sheria ya ajira ya muda mfupi.
   
 20. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #20
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Thread yako umechukulia kama vile kila mtu ni mfanyanyakazi.

  Ni asilimia ngapi ya Watanzania ambao ni wafanyakazi?

  Unasema wabunge wasaliti tuwashughulikie in 2015 as if hii ni nchi ya wafanyakazi.

  Kama kawaida hayo mabadiliko yatapitshwa na bunge.

  Na hakuna mfanyakazi hata mmoja ambaye atagoma.

  Ndiyo ukweli wenyewe japokuwa unauma.
   
Loading...