Now Tuweke balance Bungeni: Chama kuwa na 80% ya seats Wananchi ni losers! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Now Tuweke balance Bungeni: Chama kuwa na 80% ya seats Wananchi ni losers!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwanaukweli, Sep 5, 2010.

 1. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2010
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Wakati wa chama kimoja, wabunge wote walitoka chama kimoja na hivyo haikuwa issue katika mijadala kwa kuwa chama ndo kilikuwa kimeshika hatamu, na chama na serikali ilikuwa ni system hiyo hiyo.

  Tangu kuanzishwa kwa Demokrasia ya Vyama vingi, michango ya wabunge katika mijadala, hasa wa chama tawala imekuwa inalazimika kuchagua moja kati ya mawili katika hoja zilizo nyingi. Moja, ni ama kuongea ukweli kuhusu masuala yaliyo na maslahi ya wananchi: kama kufichua matumizi mabaya ya vyeo vya watendaji wa serikali; Mbili, ni ama kunyamaza kwa kuzingatia maslahi ya kisiasa ya chama chao.

  Hii ilijidhihirisha wazi pale hoja za mikataba ya madini zilipoletwa bungeni, na hoja za sakata la Richmond, EPA, Twin Tower, Rada na nyingine nyingi. Hapa ndipo kwa mara ya kwanza wananchi walianza kuona kuwa Wapinzani maana yake SI WAPINGA MAENDELEO, bali ni watetezi wa wananchi. Wabunge wa upinzani wakaanza kupendwa na wananchi: hasa watetezi wa wananchi: Mh. Zitto Kabwe na Mh. Dr. W. Slaa na wengineo. Hapa pia ndio tuliona mawaziri na wabunge wa CCM wakizomewa na wananchi kwa kuwa wananchi waliona kuwa maslahi yao yameachwa.

  CCM pia imekuwa ikitumia "adhabu" kwa wananchi wanaochagua wapinzani ya kuwanyima huduma za jamii, huku wakiendelea kukusanya kodi za wananchi hao bila aibu wala kusutwa na dhamiri. Wananchi nao si wajinga wanaona hayo, wameyaona na wamepokea ujumbe!

  Katika kampeni hizi zinazoendelea, ningetamani nione bunge linalokuwa kama la Kenya: Bunge ambalo hakuna chama kimoja kilicho na viti zaidi ya 50%.

  Nadhani tukifika huko ndo tunaweza kurudi kule: KUJADILI HOJA KWA MASLAHI YA WANANCHI, NA SI KWA MVUTO WA KISIASA. Hapa mshindi ni mwananchi. Serikali iliyoko madarakani pia italiheshimu bunge; kwani bunge litakuwa makini kuona yote yanayotendeka serikalini na KUKOSOA na KUELEKEZA kila inapofaa.

  Wananchi ni juu yetu kuona hili na kuacha ushabiki usiotusaidia wa Chama fulani.

  Tena mtu akikupa rushwa Sh. 5000 kakudharau sana huyo, kataa kununuliwa utu wako kwa vocha ya simu.

  Haya tuone kama tumeamka.

  Wana JF mnasemaje???
   
 2. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2010
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Wabunge wengi wa chama kimoja bungeni wanatusaidia nini? I mean wananchi wa kawaida.
   
 3. l

  logician mkuu JF-Expert Member

  #3
  Nov 18, 2014
  Joined: Jun 2, 2014
  Messages: 795
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hata kwenye bunge la katiba tumeona hasara ya kujaza chama kimoja bungeni.

  Wananchi tunachukua hatua.

  Tunawashukuru UKAWA kuunganisha nguvu zenu.
   
Loading...