November 2007 Inflation Rate Slightly Increases

Mtoto wa Mkulima

JF-Expert Member
Apr 12, 2007
681
126
November 2007 Inflation Rate Slightly Increases
Inflation rate for November 2007 has slightly gone up. According to the National Consumer Price Index (NCPI), inflation rate for November 2007 is 7.3 percent in comparison with the figures for November the previous year. The November 2007 inflation rate has gone up by 0.2 percentage points when compared with November 2007 inflation figure, which was 7.1 percent as measured on a year - to - year basis.

MFUMUKO WA BEI WA MWEZI NOVEMBA 2007 UMEONGEZEKA KIDOGO
Mfumuko wa bei wa mwezi Novemba 2007 umeongezeka kidogo. Matokeo ya fahirisi ya bei ya Taifa (National Consumer Price Index), mfumuko wa bei wa mwezi Novemba 2007 ni asilimia 7.3 ukilinganishwa na fahirisi ya bei za mwezi Novemba mwaka 2006. Mfumuko wa bei unaopimwa kwa kigezo cha mwaka hadi mwaka, umeongezeka kutoka asilimia 7.1 mwezi Oktoba 2007 mpaka asilimia 7.3 mwezi Novemba 2007.

Mfumuko wa bei unaopimwa kwa kigezo cha mwezi hadi mwezi (Oktoba hadi Novemba 2007), umeongezeka kwa asilimia 1.1. Fahirisi za bei zimeongezeka kutoka 139.2 mwezi Oktoba hadi 140.7 mwezi Novemba 2007. Baadhi ya bei za vyakula na visivyo vyakula vimepanda. Kuongezeka kidogo kwa mfumuko wa bei kumechangiwa zaidi na kupanda kwa bei za vinywaji laini, maji ya chupa na konyagi. Vyakula ambavyo bei zake zimepanda ni mchele, mahindi ya kusaga, unga wa mahindi, unga wa ngano, mkate, tambi, mihogo, viazi, ndizi za kupika, mboga za majani, nyama, mafuta ya kupikia na nazi. Bei za bidhaa nyingine zilizopanda ni nguo za aina mbali mbali, samani (furniture), mafuta ya nywele, baisikeli, betri ya gari, na miamvuli. Hata hivyo, bei za brashi ya kusugulia sakafu, mabeseni ya maji, radio na luninga (TV) zimeshuka. Mchanganuo wa Fahirisi za Bei za Taifa za mwezi Oktoba 2007 ni kama ifuatavyo:-

http://www.nbs.go.tz/CPI/CPI112007_Kiswahili.htm

Jamani hii ni hatari sana kuona hebu angalieni trend ya bei ya vitu muhimu kama chakula inavyokwenda juu ni balaa, nishat na maji nayi wawekezaji gani watakuja wekeza wakati garama ya uzalishaji inapanda? vinywaji navyo nisoo

Wazee wachumi wetu wa JFsijui nyie mnasemaje
 
Back
Top Bottom