Notification feki;kombe ,mwema,msika nani karuhusu traffic walipwe barabarani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Notification feki;kombe ,mwema,msika nani karuhusu traffic walipwe barabarani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jan 18, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,219
  Likes Received: 5,617
  Trophy Points: 280
  Wanandugu kama mlivyoona mwenangu alietangulia leo kulikuwa na swala muhimu sana kuonyeshwa wazi kwa traffica wakilamba "dombwa" ama rushwa
  kamanda msika ameonyeshwa kukasirika sana sana
  lakini kuna mambo mengi yanaityajika kufanyika kwenye jeshi la polisi ama traffic
  notification
  kumekuwa na swala la matraffic kupewa dhamana za kuandika notification na hata kulazimisha kulipa hapo hapo,na mwisho kuishia kupelekwa "vituo bubu vya polisi" ama vigari vyao wanapaki pembeni unaelekea huko,labda kwa mwingine unaweza kufurahi nalipa polisi leo hii naweka hili wazi shangazi yangu leo kawalipua awakuamini,hapa kawe kona kuna maaskari wanapaki pale kona ya kuingilia kawe,wanakuwa na vigari vyao vibovu vimechoka nahisi vitakuwa vya watu wamechukua pale central walipoona mtu kaachilia mbali.......
  Sasa huyu mama traffic mmoja akamkamata akamdai makosa ya alfu sitini,..akamwamabaia ampe 20,000 akasema ana ,akasema ataenda kulipa,yule mama akamlazimisha alipe pale kwenye gari akakataa alikuwa ameshaandika na notifcation uwezi amini alipoona ailipwi pale akaishia kuomba hata hiyo kumi mama akamwambia sina naitaji risiti nikalipe traffic akasema nenda usirudie tena kwa kuwa mwanamke mwenzangu,...najiuliza ile notofication aliyoandika anajibu nini kwa kuichana
  nimefika mijini mtummoja akatupa wanacheza na mkuu wa kituo husika,zile nyingi feki akikwambia kalipie kituo fulani,ujue mzee ana nusu mwisho wa siku traffic aliekamata ana[ewa nusu inayobaki mkuu wa kituo na mwandikishaji,....
  Hii rushwa aishi kama unawapa vitega uchumi vya kunzia walipwe kwenye magari jamani???????????????
   
 2. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,796
  Likes Received: 20,746
  Trophy Points: 280
  ni ngumu sana kuzuia rushwa kwa hawa polisi wetu wa barabarani,hata wakuu wa vituo/IGP na mabosi wote wakiwa wakali hawawezi kuzuia rushwa ya polisi,system nzima ya polisi imekaa ki-rushwa,igp na mabosi wengine wa polisi wako ofisini huku barabarani watacontrol vipi hawa yangeyange??ukichukulia mfano nchi za wenzetu wanausalama wana walkie talk ambazo hazizimwi, na kila anachoongea either na mwenzie au mtuhumiwa kinasikika na kurekodiwa makao makuu,kama hawa yangeyange wangelazimishwa kuwa na radio call zao on full time wangekuwa wanasikika wakati wwanaongea na mtu waliemkamata hivyo hata ukiomba rushwa unasikika na unarekodiwa,vilevile magari yao ni mabovu na hayafai kwa kazi ya polisi,gari za polisi za wenzetu ni kama kituo cha polisi kinachotembea,data base ya magari,leseni,insurance,crime record,chochote polisi anachotaka kujua kuhusu wewe anakipata kutoka kwenye computer ya gari yake,in fact polisi kabla ya kukusimamisha anakuwa anajua kila kitu kuhusu wewe na gari yako kama uko clean au la,mazingira ya polisi wetu yamekaa kirushwa na ni ngumu sana rushwa kuisha mpaka system ya polisi ibadilishwe kuwa ya kisasa na kuziba mianya ya rushwa.
   
 3. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #3
  Jan 19, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Ni makosa kuwalipa traffic barabarani. Hakuna aliyeruhusu hivyo isipokuwa Daniel Arap Moi,architect wa KANU kushindwa katika elections.
   
 4. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mishahara midogo Polisi jamani, sitetei rushwa ila waanze kulipwa vizuri kwanza na makazi yao yaboreshwe, wana hali ngumu sana hawa watu jamani.narudia sitetei wala kuipenda rushwa ila serikali iangalie wapi pakuanzia
   
 5. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Sasa hivi wanakomalia stika za fire extinguisher kwa nini askari wa fire and rescue services wasikague wenyewe? na traffic ndo wamekomalia hapo?
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mi juzi j2 jamaa alinidaka nimepakia mtoto alikula buku 2 asubuhi asubuhi ndo nilikuwa naenda kunywa supu hawa jamaa mmmh!
   
 7. Single D

  Single D JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2010
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 459
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hata round about ya BP kurasini napo wana notification feki.
  Mrema aliwahi kusema rushwa haitaisha hadi mitume wafufuke tena.
   
 8. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  wapo kila kona siyo kawe nenda kunduchi pale utakuta wamepark gari zao vichakani kila mmoja ana kitabu nenda chalinze wako porini wamejificha kibaya zaidi na boss utamkuta yupo pale ndo mkusanyaji mkuu,mfumo mzima wa police umeoza ni vigumu kumaliza rushwa police kwa sababu hata viongozi wa juu wanashiriki,dawa ya rushwa police ni kubalisha mfumo uliopo ambao ni wa mwaka 49 na kuingiza mfumo wa kisasa
   
 9. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2010
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hii ni Breaking News au? kwa sababu inajuulikana kuwa mlo wa Polisi usalama barabarani uko kwa madereva.
   
 10. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  Hapa sasa hivi nnapoandika habari hii nipo ndani ya bus la Hood na ninmshuhudia police traffic akichukua rushwa ya book mbili kutoka kwa konda. Hapa ni nje kidogo ya mji wa mfindi na kwa macho yangu kwa leo tu ni kama traffic wa tano tokea Tunduma nashuhudia wakichukua rushwa ya elfu moja na elfu mbili. NAPENDEKEZA RUSHWA NDANI YA JESHI LA POLICE ITANGAZWE KUWA JANGA LA KITAIFA
   
 11. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #11
  Jan 19, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  jamani rushwa kuisha ni kazi tukianzia na police wenyewe mshahara anaolipwa nikanakambwa anaambia zingine kajazie barabarani coz ni kiduchu.
  pili ni ss wenyewe madereva na wamiliki akuna aliyetayari kuandikiwa kosa or makosa wakati unajua kosa moja ni 20,000 utabembeleza wee utaanzia buku mbili hadi tano mwisho 10,000 ukiangalia unaona bora utoe ata kumi userve mda siku ziende
   
 12. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Off Topic - Hiyo buluu nimeipenda Jf mobile!
   
 13. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #13
  Jan 19, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Hawa jamaa ni kama viroboto, hawashibi, hawaachi. wanafia kwenye mlo.
   
 14. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #14
  Apr 2, 2015
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,548
  Likes Received: 1,593
  Trophy Points: 280
  haya yanafanywa kimazoea ...
   
Loading...