Noti za Plastiki Kuchukua Nafasi ya Noti za Karatasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Noti za Plastiki Kuchukua Nafasi ya Noti za Karatasi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Boflo, Mar 8, 2010.

 1. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,393
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Member's LoginUsernamePasswordNot a member? Sign Up
  Sign Out
  [​IMG] Noti za Plastiki Kuchukua Nafasi ya Noti za Karatasi
  [​IMG]
  Noti za plastiki zinavyoonekanaMonday, March 08, 2010 1:16 AM
  Kidogo kidogo noti za karatasi zinaanza kutoweka duniani na nafasi yake inachukuliwa na noti za plastiki, Kanada imekuwa nchi ya nane duniani kubadilisha pesa zake na kuanza kutumia noti za plastiki.Noti za karatasi kidogo kidogo zinaelekea kuwa historia na nafasi yake inachukuliwa na noti za plastiki ambazo hazipitishi maji hivyo hata ukizisahau kwenye nguo zako wakati wa kuzifua hazitapata madhara yoyote tofauti na noti za noti za karatasi ambazo huchanika kirahisi zinapolowa maji.

  Kanada inakuwa nchi ya nane duniani kubadilisha noti zake na kuanza kutumia noti za plastiki. Kanada itaanza kuziondoa noti za karatasi kidogo kidogo kuanzia mwishoni mwa mwaka ujao.

  Noti za plastiki zinatumia plastiki aina ya polymer biaxially-oriented polypropylene (BOPP) na zimeambatanishwa na vionjo vingine vya ulinzi ili kuzifanya noti hizo ziwe si rahisi kufojiwa.

  Noti za plastiki hazichaniki wala kuharibika kirahisi hivyo kuziokoa pesa za serikali zinazotumika kuchapisha noti mpya kila baada ya muda.

  Faida nyingine ya noti za plastiki ni kwamba hazibebi uchafu mwingi na bakteria kama zilivyo noti za karatasi. Mfano mzuri ni noti za dola ya Kimarekani asilimia kubwa ya noti hizo zina uchafu wa madawa ya kulevya kutokana na kutumiwa zaidi na wauzaji wa madawa ya kulevya.

  Australia ndio iliyokuwa nchi ya kwanza kutumia noti za plastiki. Ilianza kutumia noti hizo tangia mwaka 1992.

  Nchi zingine zinazotumia noti za plastiki ni Bermuda, Brunei, New Zealand, Papua New Guinea, Romania na Vietnam.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,231
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Ni hatua moja mbele anyway!
  But i think it will be a very temporary solution, coz we are soon going to e-money.
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 42,116
  Likes Received: 37,540
  Trophy Points: 280
  Bwabwa,
  kumbe wewe ni economist.
  Safi sana
   
 4. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,033
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Bwabwa kumbe sometimes unakuwa serious!! Good one.
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,640
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
  ni hatua nzuri sana !
   
 6. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #6
  Mar 8, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  okey , asante BWABWA.
  ILA NIMEWAHI KUONA PESA ZA Zambia, wana noti fulani hivi zina material ya plastic, ila zinapoanza kuisha zinatia hata kinyaa.
   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,936
  Likes Received: 384
  Trophy Points: 180
  sio eco- friend hizo-Plastic tena?
   
 8. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,851
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
   
 9. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,824
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Jimmy - e-money will take more that 20 years - tupo nyuma sana.
   
 10. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #10
  Mar 8, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Duu,hizo pesa za plastic si zinatupa hasara?zikianguka si zitavunjika?
   
 11. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,517
  Likes Received: 7,271
  Trophy Points: 280
  mkuu miaka 20 ni mbali sana, technologia inakimbia fast sana, ukikosa original basi MCHINA yupo,
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...