Noti mpya ya shilingi elfu hamsini na laki moja inahitajika kwa Tanzania

kabila01

JF-Expert Member
Apr 21, 2009
4,048
2,000
Ndugu wana jamii nimeamua kuleta hii topic kwenu baada ya kuangalia kwa kina tatizo la mrundikano wa watu hasa kwenye ma benki yetu hapa nchini.
Siku moja nilikua benk ya NBC pale makambako Iringa na foleni ilikua ina watu kama 15 tu lakini ilinichukua masaa mawili kufika kwa cashier na ma cashier walikua watatu. Kilichotokea ni kwamba kila aliekua anaenda pale dirishani alikua na mzigo wa hela ambao ulikua unamfanya Teller atumia hata dk 15 kuhesabu
Pia saizi mtu kua na laki 5 na kuendelea za matumizi ya kawaida ni kawaida tu kwa watanzania. uwekaji wake unakua mgumu sana hasa tunapokua matembezini na kwenye shughuli zingine.
Serikali inashindwa kukubali tu kua thamani ya fedha katika nchi yetu imeshuka sana hivyo ni muhimu wakachapisha noti mpya za shilingi elfu hamsini na laki moja kutuondolea usumbufu
 

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,951
2,000
Dah mkuu unataka utupeleke kwa baba yako Zaire na Zimbabwe?

Wakichapisha noti hizo za 100,000/= shilingi yetu itakuwa jehenamu hapa penyewe inapumulia mashine
 

Makindi N

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
1,067
1,250
That's an elementary thinking. Hiyo Makambako yenyewe unaweza usile chakula au kosa maji ya chupa ya 1000/= au 200/= kisa una note ya 10,000/= na hawana change. Yaani unamaanisha anaelipwa mshahara wa laki wawe wanapewa note moja tu?
 

TUKUTUKU

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
11,775
2,000
Nakubaliana na wewe kuwa kuna tatizo kama hilo,lakini naona wewe umelikuza sana (you have extremely exaggerated the issue).Bank tellers siku hizi wanatumia mashine kuhesabu fedha,kwa kutumia dakika 15 basi hizo fedha ni nyingi sana na kwa matumizi ya kawaida kutumia laki tano ni nyingi mno labda kama kuna kitu unataka kununua tofauti na matumizi ya kawaida kwa vile chakula na mavazi!hata hivyo hoja yako bado ina uzito furani,mimi nakubaliana na wewe kuanzishwa kwa sarafu ya elfu hamsini,lakini sio laki moja!!
 

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,694
2,000
Ni kweli kwa jinsi hali ilivyo tunahitaji noti ya 50,000 na 100,000 maana kubeba pesa sasa imekuwa issue. Hata huyu mchangiaji mwingine alivyosema ukienda kupata huduma counter shida kweli. Wahudumu uchukua muda mwingi kuhesabu pesa unayopeleka. Kwa deposits za siku hizi mtu kudepost 100,000,000 kwa mtu mmoja si ajabu!. Ebu fikiri unahitaji 500,000 toka ATM itakuwaje?
 

De Javu

JF-Expert Member
May 5, 2010
265
0
Kuchapisha noti za kima kikubwa kama ulivyoeleza kutasaidai kupunguza usumbufu lakini kwa upande mwengine kuna madhara makubwa zaidi, moja ambalo si nchi hii tu bali nchi nyingi wanapiga vita utengenezaji wa noti za bandia, fikiria umebambikiwa noti-feki ya laki? Vilevile ufanikishaji wa biashara haramu unakua rahisi kufanya malipo ya pesa nyingi bila ya matatizo. Kwa watu wa kawaida pia inakua vigumi pale unapofanya malipo, kwa mfano umelipwa hiyo noti ya laki unahitaji kulipa nauli ya daladala au kununua soda hapo ndio ugumu unapokuja utaanza kuzunguka kila kona kutafuta chenji. La msingi ni Serikali kuharakisha miundo mbinu ya kibenki ili watu wengi zaidi waweze kutumia malipo kwa kadi kama nchi za dunia ya kwanza na kuepuka kubeba rundo la pesa. Kwa upande wa mabenki, wanaweza kuondoa hizo foleni kwa kuweka mashine ambazo zinapokea na kuweka pesa badala ya binaadamu kwa haraka zaidi na ufanisi mkubwa.
 

BRUCE LEE

JF-Expert Member
Dec 11, 2010
2,097
2,000
kwanza kwanini pesa yetu inazidi kushuka thamani? Kama kweli tuna wachumi wazuri huu ndio wakati kukomaa na kubuni mbinu za kuhakikisha pesa yetu inakua na thamani na kama vipi wazifutilie hata noti za elf 10,zibaki za buku5,mbona rwanda na kenya wameweza?kwanini sisi tushindwe??j
 

Da Pretty

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
3,047
2,000
hujapita wilaya za mikoa ya Lindi,mtwara na Ruvuma. utazunguka na 10,000 yako bila kupata huduma,hiyo noti ya elfu 50 si itakua balaa!
 

BRUCE LEE

JF-Expert Member
Dec 11, 2010
2,097
2,000
kwanza kwanini pesa yetu inazidi kushuka thamani? Kama kweli tuna wachumi wazuri huu ndio wa kukomaa na kubuni mbinu za kuhakikisha pesa yetu inakua na thamani na kama wasifutilie hata noti za elf 10,zibaki za buku5,mbona rwanda na kenya wameweza?kwanini sisi tushindwe??
 

kivato

Member
Nov 20, 2010
18
45
Katika dawa sio kuanzia noti mpya,
ila kuna haja ya benki zetu kuongeza muda wa kufanya kazi. kwa mfano benki inakuwa wazi hadi saa tano usiku ambapo utapata huduma zote za kibenki. pia benki zetu kufanya kazi muda kwenye siku za jumamosi na jumapili. Maana benki zingine zinafungwa saa tisa mchana, hii inachangia sana foleni na mambo aliyayasema ndugu yetu.
 

Utingo

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
7,785
2,000
Ni kweli kwa jinsi hali ilivyo tunahitaji noti ya 50,000 na 100,000 maana kubeba pesa sasa imekuwa issue. Hata huyu mchangiaji mwingine alivyosema ukienda kupata huduma counter shida kweli. Wahudumu uchukua muda mwingi kuhesabu pesa unayopeleka. Kwa deposits za siku hizi mtu kudepost 100,000,000 kwa mtu mmoja si ajabu!. Ebu fikiri unahitaji 500,000 toka ATM itakuwaje?

kabla ya kukubaliana naye, jaribu kwenda vijijini na noti ya sh elfu 10,000 kisha omba change uonge shughuli yake ilivyo pevu kuipata. Tatizo ni huduma mbovu za kibenki zilizopo hapa nchini.
 

Mchili

JF-Expert Member
Aug 19, 2009
725
195
Tatizo tunanang'ania mno kufanya transaction kwa cash. Tujifunze kutumia huduma kidogo iliyopo ya kielectronic kama MPESA, Tembo card, cheque nk badala ya kubeba lundo la hela kila unapofanya manunuzi. Kuchapisha noti za dhamani kubwa tutakua tunahatarisha kuelekea waliko Zimbabwe.
 

Little John

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
215
170
Hata mimi nakubaliana na hoja ya kuwana noti ya Tshs. 50,000 & 100,000, naomba tusiwe na negative mind sikuzote, tukiona glass ya maji ipo nusu tujifunze kusema "the glass is half full" rather than saying "the glass is half empty", kwanini nasema hivyo, watu wanafikiria haraka sana jinsi ya kuitumia hiyo hela kununua vitu na je change inakuwaje, je vijijini itakuwaje, kwanini hatujafikiria kwamba itakuwa rahisi sana sana jinsi ya kupunguza counting transactions na ubebaji wa hela.
Ni habari ya kuaminika kabisa kwamba kuna noti ya US $ 5,000 na 10,000 ambayo kwa haraka haraka hiyo nia amount kubwa kupita kwenye mikono ya kawaida ni wale matajiri sana wenye uwezo wa kuimiliki hiyo, hivyo kuwa na Tshs. 50,000 na 100,000 sio ajabu sana. Mimi nafikiri ni jinsi ya BOT kuweka utaratibu wa mzunguko wa hiyo hela na mengineyo, other wise I think its ok.
 

HansMaja

Senior Member
Nov 9, 2010
102
250
Mimi nakubaliana na waliosema juhudi zinahitajika kulinda thamani ya shilingi na sio kuchapisha minoti ya 50,000/- au 100,000/-. Serikali inatakiwa ihakishe export inaongezeka kwa hali juu. Hii ni njia muhimu ya kuifanya sarafu ya nchi iwe imara. Wazo lingine ninalokubaliana nalo ni kuanzisha mtindo wa electronic economy...yaani kutumia mfumo wa wa card kufanya transaction kama ilivyo huku kwenye nchi zilizoendelea. Cash economy yaani kutembea na minoti imepitwa na wakati
 

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,528
2,000
Duh, umasikini unatufanya tufikirie kuchapa noti ya thamani kubwa na si kuimarisha uchumi na kuongeza thamani ya Sarafu yetu na hivyo kuondokana na kuchapisha makaratasi yenye tarakimu nyingi.

Mchili kasema, tunahitaji msukumo na undava kutoka Serikalini wa kuhakikisha kuwa watu wanatumia viplastiki au hundi na hivyo kupunguza mzunguko wa fedha na uchapishaji ambao unashusha thamani ya sarafu!
 

MaMkwe

JF-Expert Member
Sep 5, 2007
284
0
Ndugu wana jamii nimeamua kuleta hii topic kwenu baada ya kuangalia kwa kina tatizo la mrundikano wa watu hasa kwenye ma benki yetu hapa nchini.
Siku moja nilikua benk ya NBC pale makambako Iringa na foleni ilikua ina watu kama 15 tu lakini ilinichukua masaa mawili kufika kwa cashier na ma cashier walikua watatu. Kilichotokea ni kwamba kila aliekua anaenda pale dirishani alikua na mzigo wa hela ambao ulikua unamfanya Teller atumia hata dk 15 kuhesabu
Pia saizi mtu kua na laki 5 na kuendelea za matumizi ya kawaida ni kawaida tu kwa watanzania. uwekaji wake unakua mgumu sana hasa tunapokua matembezini na kwenye shughuli zingine.
Serikali inashindwa kukubali tu kua thamani ya fedha katika nchi yetu imeshuka sana hivyo ni muhimu wakachapisha noti mpya za shilingi elfu hamsini na laki moja kutuondolea usumbufu

Taarifa nilizonazo ni kwamba BOT inakusudia kuondoa noti za sh elfu tano na elf kumi sokoni na kurudisha noti za sh 5, 10, na 20 na kutoa noti ya sh 50.
 

Kigogo

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
20,523
2,000
rais hana akili unategemea nini??noti ya 100,000/=?kazi ipo ..EU noti kubwa ni euro 500 na nchi kama holland hawakubali kufanya transaction madukani na minoti ya euro 500 ni 50 na 100 tu ..hapa mkwere anaona raha kuwa na minoti ya 100,000/=
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom