Noti mpya ni Ufisadi mwingine? Nani awajibike?

M-pesa

JF-Expert Member
Sep 4, 2011
602
151
Wanajamvi,
Kumbukumbu zangu zinaonesha ni miezi tisa sasa tangu noti mpya ziingizwe kwenye mfumo wetu wa kifedha. Imebaki miezi michache mwaka uishe, lakini bado naziona noti za zamani bado zimezagaa mitaani.
Kuna kipindi nakamata noti za zamani tu, tena kutoka kwenye taasisi za kifedha. Nilitegemea taasisi kama benki ingesaidia kuziondosha hizi za zamani kwa kuwapatia wateja wao zile mpya kupitia ATM machines au Kaunta zao.
Wakuu, naomba wenye kufahamu ni muda gani labda hizi noti za zamani zitakwisha atujuze. Je, ni mwaka mmoja, miwili au haifahamiki au hata kukisia ni ngumu?

Nawasilisha!
 
hizo zitaisha taratibu through transaction benk kuu haiwez kukusanya zote kwa mara moja na haraka but nahc kutokana na kutengeza pesa mupya ni gharama so wanatoa toa kwa awamu wakati wanakusanya za zamani mdogomdogo na ndomana unaziona bado za zagaa!
 
Kumbuka hili lilifanyika baada tu ya uchaguzi. Athari zake ni nini?
 
hizo zitaisha taratibu through transaction benk kuu haiwez kukusanya zote kwa mara moja na haraka but nahc kutokana na kutengeza pesa mupya ni gharama so wanatoa toa kwa awamu wakati wanakusanya za zamani mdogomdogo na ndomana unaziona bado za zagaa!

mbona bado zinatolewa mpya za zamani?
B.o.t wakiri kwamba walichemsha
 
Hadi JK atakapomaliza U-Rais wake, na atakaeingia ku-stabilize uchumi.... Wazitoe kwa uchumi wa serikali ya Kikwete?
 
Ndugu wana JF majuzi kati nimestushwa kuona Noti ambazo zinatakiwa zipotee kwenye mzunguko wa sasa zikiwa mpya yaani kitu kinyukri zinangaa na harufu ile yake ambayo ukiinusha lazima upige chafya... chyaaaa!!

Sasa sielewi why zinatoka wapi au Benki kuu wanaendelea kuzifyaua tena kwa kasi maana jinsi Dollar ya kimarekani inavyozidi kwenda juu hadi kwa statics ikifika Dec Dollar Moja ya Kimarekani itafika 2000 au 2200 BOT wakiendelea na kamchezo kao usioeleweka Sababu ya Kuchapisha Noti Mpya za Zamani na Noti Mpya za Sasa.

Hivi Bunge huwa halishilikishwi kutoa uamuzi wa kuchapisha noti Mpya? yaani Wakiishiwa Pesa dawa ni Kuchapisha tu Hii imekaa Fresh kama Zaire ya Mabutu..

Mkaguzi wa Hesabu sijawahi msikia akitoa Neno kuhusu ukaguzi nawasiwasi Noti Mpya zimechapishwa kwa sababu maalum ya Kisiasa.

Naombeni kujua mwenye ufahamu zaidi na hili linatitatiza sana sababu sioni umuhimu wa Kutumia Pesa Za Aina Mbili Tofauti kwa Muda Mrefu sana
 
waondoe manoti mabovu yaliyopewa jina feki la noti mpya. Hayana hata quality ya kuwa noti ya nchi hii. Watuachie noti zetu za ukweli kabisaa!
 
Nchi yenye viongozi wahuni wasiojali raia weke siku zote mambo yao hubaki ya kihuni. Ebu angalia minoti waliyotuletea jinsi ilivyo feki noti kama ya mia tano ikipitia kwenye mzunguko kwa siku chache inapoteza hata sura yake inachakaa kama kwamba imetumika miaka mingi. Watanzania tufike mahali tukatae ushenzi huu tunaofanyiwa na viongozi wasio wazalendo, viongozi ambao wapo kwa ajili ya matumbo yao.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
mimi kinachonitisha ni kasi ambayo shilingi yetu inapoteza thamani.hili ilitakiwa liwe addressed kama janga la kitaifa otherwise watanzania wa kawaida hawataweza kuishi ktk ardhi yao
 
Nchi yenye viongozi wahuni wasiojali raia weke siku zote mambo yao hubaki ya kihuni. Ebu angalia minoti waliyotuletea jinsi ilivyo feki noti kama ya mia tano ikipitia kwenye mzunguko kwa siku chache inapoteza hata sura yake inachakaa kama kwamba imetumika miaka mingi. Watanzania tufike mahali tukatae ushenzi huu tunaofanyiwa na viongozi wasio wazalendo, viongozi ambao wapo kwa ajili ya matumbo yao.
Yaani mimi bado nakumbuka Profesa Ndullu alivokuwa anatetea noti hizi...hivi BoT hakuna wataalamu wa noti? Kama mtu wa kawaida mtaani na mapema kabisa anaweza kujua noti hazina ubora wale wataalamu wetu wanalipya kwa kazi ipi? Hizi noti ni aibu kubwa na unaweza kuta nio pesa nyingi 'imeplipwa' kuzitengeza lakini sehemu ya fedha hizo kuishia mifukoni mwa 'wazalendo' wachache.
 
NAOMBA MNISAIDIE NYIE WANAUCHUMI WA JF, hivi hili jambo halina athari kwa kushuka kwa thamani ya shilingi? au ndio mbinu mpya ya chama kilichoshika dola kujikusanyia fedha za kampeni 2015?
 
jamani mm sio mtaalamu wa uchumi bt i have an idea. Inakuwaje serikali ya tanzania inaongozwa na noti mbili mpaka sasa.yan kuna elfu kumi mpya na yazamani. kuna mia tano mpya na zamani. Navyoelewa noti ikiwa introduce kwenye mzungunguko wa fedha uwa inachikua miezi 6 tuu mpaka ya zamani ina dissolve.jee nia ya kuintroduce ilikuwa ni nn?i fail to understand. Yan inaboa sana kwenye waleti kuna ela kubwa nyingine ndogo. Wanao jua uchumi or what happened embu tusaidiane hapa.
 
Wamegundua waliyo introduce iko chini ya viwango na haifai.......kwa kifupi jamaa alikuja na idea kwa ajili ya kutunisha kaji- account kake Uswiss
 
poor economic knowledge, poor management, poor leadership, ufisadi and being a leader without any vision for your country
 
Noti mpya zina kiwango bomu sana, zinachakaa upesi, hata kama serikali inasema zina ubora. They are poo indeed, kama walivyo poor kule uppstairs viongozi wenyewe walioleta noti hizo
 
Noti mpya zina kiwango bomu sana, zinachakaa upesi, hata kama serikali inasema zina ubora. They are poo indeed, kama walivyo poor kule uppstairs viongozi wenyewe walioleta noti hizo

si suala la uchakavu, hawana mikakati ya kuinua uchumi wa nchi, hazina imekauka, mishahara unalipaje....dawa ni kuchapisha noti mpya...ingekuwa mishahara inalipwa kwa fedha za kigeni tungeona mziki wake.
 
Quality ya Noti ni mbaya sana,na hamna mtu aliyewajibishwa kwa kupitisha madudu haya ktk dawati lake. pia inawezekana lilikuwa zoezi la kukamilisha uchaguzi.

hapo ndio tuelewe uongozi wetu wa nchi hautaki kuwajibisha watumishi wake ktk Taasisi
 
Back
Top Bottom