Noti Bandia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Noti Bandia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mgoyangi, Mar 11, 2011.

 1. Mgoyangi

  Mgoyangi Senior Member

  #1
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Benki kuu ya Tanzania imekanusha uvumi unaosambazwa na watu wenye nia mbaya kwamba ina zoezi la kukusanya noti mpya kili kuziondoa katika mzunguko kwa madai kuwa ubora wake ni hafifu.
  Akiongea na Radio Free Afrika kwa njia ya simu kutoka Dar es salaam , Mkurugenzi wa Huduma za kibenki, Benki kuu ya Tanzania Bwana Emmanuel Boaz amesema habari hizo ni za kizushi na kwamba Benki hiyo haina mpango kama huo.
  Bwana Boaz amesema Bennki kuu inawahakikishia wananchi kwamba noti mpya zilizoingia kwenye mzunguko mapema mwaka huu ni bora na zinapaswa kuendelea kutumika sambamba na zile za zaman na kwamba wananchi wanapaswa kuendelea kuzipokea na kuzitumia pasipo shaka yoyote.
  Hata hiyo Mkurugenzi huyo wa huduma za kibenki amewataka wananchi kuendelea kuzichunguza kwa umakini kila wanapopokea noti hizo kuligana na alama ambazo zimekuwa zikitangazwa na benki hiyo kupitia vyombo vya habari.
  Hatua ya Benki kuu ya Tanzania kutoa ufafanuzi hiyo inafuatia kuwepo kwa kundi la matapeli ambalo linasambaza uvumi kuwa noti mpya zinakusanya kwa nia ya kuzibadilisha noti hizo kwa thamani ndogo na hivyo kujipatia kipato kisicho halali.
  Kulingana na maelezo ya Bwana Boaz, baadhi ya wananchi wamekuwa wakipiga simu na kutuma barua kutoka sehemu mbali mbali nchini wakilalamikia kuwepo kwa kundi la matapeli ambalo linasambaza
   
 2. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mi sijui watanzania ubora tunaupimaje...Noti inatoa rangi ka batiki iliolowekwa leo unasema noti bora?
   
 3. dedam

  dedam JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 846
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  gavana alishanena noti yote yote ile origina iwe pound,dollar lazima itoe rangi!! Ikisuguliwa
   
 4. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Nasikia ukitaka kujua noti feki ama halali, chunguza ubora wake. Zilizo bora zaidi siyo za Benk Kuu hizo ndiyo mzikatae. Dhuuu...!
   
 5. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  niliipenda sana ile noti ya 10,000 ya kwanza kabisa ile ya blue natamani niipate kama kumbukumbu
   
 6. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Inayotoa rangi ni feki mbuya. Mimi nimezijaribu kwa kuloweka hizo noti, halafu nikapiga pasi ikiwa katikati ya karatasi nyeupe. AISHIVYO BWANA, sikuona hata doa la rangi lenye nanometa moja!
   
Loading...