Noti bandia sio jambo geni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Noti bandia sio jambo geni?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dingswayo, Mar 11, 2011.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Naona mkurugenzi wa BOT hapa anasema noti bandia sio jambo geni. Suala ni kuwa zimeingizwa juzi juzi tu hapa na kumekuwa na forgeries nyingi sana. Ni jinsi gani tatizo hili litatatuliwa? Hii ndio tunataka kusikia.
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  wish ningekuwa sniper, ningewatungua hawa wote wanaotetea sera mbovu wizi ufisadi
   
 3. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Sio mara ya kwanza kwa Watanzania kuwa no noti. Tumezaliwa tumezikuta. Mbona hizi mpya za sasa zimezidi kuwa forged, na kwa nini sasa?
   
 4. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  Kwa uwazi kabisa, utaratibu wa kutengeneza noti huwa na usiri mkubwa, yaani katika kuchakata makaratasi yenyewe! Sasa ili siri ya noti ivuje, aidha mchapishaji wa hizo avujishe(kwa makampuni ya Ulaya sidhani), ama wenye kuzitaka hizo noti(BoT katika kesi hii) wavujishe mchakato wa utengenezaji wake kwa maharamia. Ukitazama filamu hii ya noti mpya ilikuwa na mizengwe kibao: Mara ya kwanza gazeti moja lilitoa uwezekano wa BoT kuchapisha noti hizo, sikumbuki kama benki ilithibitisha au kukanusha. Noti zilipoingia kukawa na tetesi kuwa kiasi fulani kimeibwa pale JKNIA, halafu zikachelewa kuingia mzungukoni, hata ikadhaniwa kuwa zile bandia zimeuwahi mzunguko. Mwisho wa picha nikasikia ati BoT wamepanga kuziondoa noti mpya kwenye mzunguko mara ifikapo mwezi wa nne. Eh, nimesahau kuwa hizi noti ndio zile ambazo Gavana Ndullu alizifia mpaka basi, kuwa ni vigumu kughushika! Aaaaaaagh.....
   
Loading...