JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,112
- 3,536
Jamiifporums bwana! nimekuwa memba wa JF kwa muda mrefu ila rasmi nilijiunga mwaka 2012. Nimejifunza mambo sana kupitia forum hii.Kuna watu humu wanataka mafanikio ya Nchi kiuchumi na kijamii lakini wachache sana wanao jua tutafikaje huko!! Na ndio maana nikawaza hivi ni nani anaweza kuwaridhisha members wa jamiiforums?kuna baadhi ya watu kwao hakuna jema hata lingefanywa na nani na kwa malengo gani,they will always criticize.
Zamani wengi tulikuwa tunalalamika kuhusu ujenzi holela hususan jiji la Dar,lakini leo hii ubomoaji wa nyumba zilizo jengwa mabondeni na maeneo yasiyo ruhusiwa kisheria tayari watu wameanza ooh serikali imekurupuka na mbaya zaidi bila kuonesha au kupendekeza wangekuwa wao wangefanyaje? UKITAKA KUINGIA PEPONI SHARTI UFE!! Na ili jiji hili siku moja lipendeze, ni sharti ubomoaji ufanyike kwanza na ndio mpangilio mzuri uje!!
vivyo hivyo tulikuwa tunakubaliana kwa sehemu kubwa tu humu kuwa mtu sahihi kuwa waziri wa elimu ni Prof Ndalichako, lakini kuna wengine wasio na subira tayari wamesha sema hata yeye ndio walewale!!Hapo ndio najiuliza hata wewe ukiingia ofisini leo utaweza kufanya mabadiliko makubwa siku moja?
Wengine wameenda mbali kwa kusema kweli kasi aliyo anza nayo mheshimiwa magufuli ni nguvu ya soda tu kwasababu watu walio chota fedha kupitia Bank ya Stanibic hawajakamatwa! kweli? waziri akifanya jambo ooh anataka kuuza sura ITV! Kuwa kiongozi siyo mchezo! ni sawa na kuongoza watu wengine wanataka jua ilihali wengine wanataka mvua wakati huohuo.
wapeni muda viongozi wetu wafanyekazi na ndio kwanza hata siku 100 ofisini hazija fika.Kazi iliyo fanywa na mheshimiwa Magufuli siyo mchezo. ni watu wachache sana duniani wanaweza kufanya haya hasa ukizingatia anatoka katika chama kilicho choka na ndicho kilikuwa kinakumbatia maovu.Na ndio maana nikafikia uamuzi kwamba NO BODY CAN BE EVERYTHING TO EVERY BODY! Viongozi wetu someni Jf, chukueni yaliyo mazuri tuachieni yanayo udhi wengine huwa tuna andika kuondoa frustrations !!