Elections 2010 [NOT OFFICIAL]: JJ Mnyika: Tumeshinda kwa zaidi ya kura 20,000

ccm kama hamkuchaguliwa kwenye sanduku mkubalini kuwa wananchi tumewachoka..hamuelewi nini?
 
Kusoma hawawezi, hata kuangalia picha jamani!! CCM hamchomoki hapo Ubungo. kubalini tu.
 
Wanazidi kujiaibisha, na kwa taarifa yao jimbo la ubungo linaangaliwa kuliko hata matokeo ya uraisi
 
Jimbo la Ubungo hawawezi kushinda na CCM know it well. Ila wanataka focus ya watu ihamie Ubungo huko kwengine wafanye jinai walizopanga kuzipanga. Bahati mbaya wamechelewa, tathmini zao zilikuwa za uongo na hawakutarajia upinzani ulio tokea. Kwa hivyo hawakujiandaa kuiba kura! Sasa wanakumbuka shuka imeshakuwa asubuhi.

JK wa 2010 ni 10% ya yule wa 2005 kwa sababu ufisadi umemuangamiza. Hakuna kurudia kuhesabu kura popote. Wanataka wavuruge angalau uchaguzi urudiwe ili wafanye kile ambacho walisahau kukifanya kwenye huu uchaguzi. Hata hivyo ukweli ni kuwa organization ya CCM imeshakufa na hakuna wanachoweza kufanya effectively sasa hivi. Hata wizi wa kura hawawezi, watakamatika tu!

Tangazeni matokeo ya kura kama yalivyo kwenye vituo vya kupigia kura!!
 
Amini usiani umma umeongea sasa wamebaki vinywa wazi hatulali mpaka kieleweke :israel:
 
Kweli matendo yanaongea kwa sauti kuu kuliko hata maneno. Wana wa nchi wametenda kimya kimya kwenye masanduku ya kura lakini kishindo chake kwa hakika ni kizito, yeboyebo CHALI!
 
hahaaa kazi wanayo CCM...nasiki znz mkapa na mwinyi wako huko wanajaribu kuchakachua.....Bwawani watu lundo na kuna harufu ya vurugu maana wanasema hawatakubali...hahaaaa CCM bye bye..Sawa sawaaaaaa

Moto wameuwasha, counter ya nguvu.
 
Mkuu Pasco, naangalia tbc1 lakini wakati mtangazaji anajaribu kumuuliza msimamizi msaidizi-Ubungo kujibu hoja ya Mh. Mnyika kuchelewesha matokeo lakini ghafla wakaondoa kabla hajajibu swali hilo na kuonyesha mambo mengine.
MyTake:
Nina wasisima na Credibility ya TBC1 kwa maslahi ya TZ
Naomba usiwe na wasiwasi, bali uwe na uhakika kwamba, TBC ipo kwa ajili ya CCM na propaganda zake. Na tukiingia tu madarakani tunaanza na TIDO, hakika hatutamuacha. Asidhani aliyotutendea tumeyasahau, tunayakumbuka yote.
 
Sasa hivi ni saa tano na robo usiku kwa saa za Tanzania. Yaani matokeo ya ubungo HAYAJAJULIKANA tu? Kasulu, Ngara, Kibondo et la matokeo yapo hewani lakini mujini kabisa ati bado. CCM muogopeni mungu jamani!
 
Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba kijana Mnyika ni Mbunge wa Ubungo kuanzia leo. Ameshinda kwa kishindo na watu wote wamelipuka kwa shangwe. Pale Loyola kwa sasa hapakaliki!!
 
na wamtangaze na halima mdee ili aende akapumzike sasa, hajalala tangu juzi, kama walifikiri atakuwa legelege kwa uchovu ili wachakachue wamekwisha.
 
Shukrani, karibu ndoto yangu inatimia ningekikosa hiki kichwa bungeni ningesikitika sana, ni kijana aliyeitumikia Chadema kwa moyo wote na wote tumeshuhudia. Mdee alimaliza aliposema mbunge mmoja wa Chadema ni sawa na wabunge 20 wa CCM. Hongereni sana huko bungeni sijui kama patatosha.
 
Back
Top Bottom