Elections 2010 [NOT OFFICIAL]: JJ Mnyika: Tumeshinda kwa zaidi ya kura 20,000

wana jf mpaka sasa mambo yana kuwa na utata, kiravu kaenda ubungo , manyika according to primary election kutoka kata zote anaongoza kwa kura zaid ya elfu 20, wakawaambia tume wahesabu kwa kutumia excel,wakina mnyika walienda na laptop sita, wasimamiz wa kituo wakasema hawawezi kuzitumia, kwahiyo wamepeleka laptop kutoka makao makuu nec, ndio wameanza kuhesabu,..

kuhesabu kata hata mia ni dk chache to tena na kwa kichwa,ok utaratibu unataka excel ila ,1

100+100=200 excel ikichakachuliwa ikasema 10000?
 
Shukrani, karibu ndoto yangu inatimia ningekikosa hiki kichwa bungeni ningesikitika sana, ni kijana aliyeitumikia Chadema kwa moyo wote na wote tumeshuhudia. Mdee alimaliza aliposema mbunge mmoja wa Chadema ni sawa na wabunge 20 wa CCM. Hongereni sana huko bungeni sijui kama patatosha.

Mbunge mmoja wa Chadema ni zaidi ya Wabunge 50 wa CCM. Ukweli ndio huo.
 
haki ya nani vile,sasa roho imetulia
sababu ilitolewa hasa nini kilichofanya wachelewe?
kura zikoje ebu tupe tulale

Kawe tunasubiri
mtaamini kila udaku...mi niliongea nae kwa simu, ngoma bado mbichi!
 
kwa hiyo hawa ndio wanafidia kukosekana slaa bungeni!!! Na hasara nyingine ni atakaposhindwa urais na dalili zinaonyesha!!!!!
ngoja nikupe siri usiyoijua, kwa matokeo ya sasa, kila kiongozi wa ccm anahjihisi analawitiwa....chadema wametoa kichapo tulichokuwa tunakihitaji
 
Kuna kichwa toka Musoma kinaitwa Vicent Nyerere yaani hakurupuki kuongea ana data za kila anachoongea.Sijui huko bungeni itakuaje,nataka wakose 2/3 ya wabunge ili kuwe na mabadiliko ya katiba
 
Inavyoonekana nchi hii haiwezi kukombolewa bila wananchi kugangamala. Hii style itupatie funzo kubwa sana kwa chaguzi zijazo.
 
Huyu maji marefu ni profesa wa nini? Mwenye taarifa naomba msaada.

Profesa Maji Marefu ni Mganga wa Kienyeji, darasa halijui=mbumbu, yeye na Shekhe Yahya ni sawasawa. Kama nayeye amekuwa mbunge basi ni balaa bunge litalipuka kwa uchawi huko.
Kwa kifupi ni Profesa wa kujiita mwenyewe kwa kufanya mambo ya nguvu za kiza. Binafasi siamini kama amekuwa mbunge,
 
Hamna mwenye figures basi ni bora kusubiri kupata official matokeo yanayosubiriwa
 
kwa hiyo hawa ndio wanafidia kukosekana slaa bungeni!!! Na hasara nyingine ni atakaposhindwa urais na dalili zinaonyesha!!!!!

Kwa wizi wa CCM hilo lawezekana, ila hata mtoto mdogo anajua Kikwete analazamisha urais huku akijua uwezo huo hana.

Its just a matter of time sasa hivi macity karibu yote ambako ndio kwenye maendeleo na watu wenye upeo mkubwa,wamechangua upinzani, CCM wameshinda sehemu ambazo watu bado wanauchapa wa pono.

Hao wanaouchapa sasa hivi baadae watajiuliza mbona wenzetu walioendelea wanachagua upinzani? Hilo swali tu ni ufunguo wa mabadiliko yao.

Tusubiri.
 
na wamtangaze na halima mdee ili aende akapumzike sasa, hajalala tangu juzi, kama walifikiri atakuwa legelege kwa uchovu ili wachakachue wamekwisha.

Wanawababaisha na vimilioni vyao vya wizi. Hivi takukuru wako wapi? Na Kibaha Mjini CCM wanamshawishi kijana wa Chadema wampe vimilion kama 40,000,000 ambazo hazina value kabisa kama ushindi wa Chadema ulivyo.
 
Hivi uteuzi wa wabunge wa kuteuliwa lazima wawe wanawake tu maana mie napendekeza kama Dr wa ukweli akishindwa ateuliwe kama mbunmge akawachachafye mafisadi
 
Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba kijana Mnyika ni Mbunge wa Ubungo kuanzia leo. Ameshinda kwa kishindo na watu wote wamelipuka kwa shangwe. Pale Loyola kwa sasa hapakaliki!!

Werrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaawerrrrrrraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Sugu kwa pembeni bila kumsahau mzee wa kiraracha, najaribu kupiga picha bungeni Mrema akibishana na prof. Maji marefu kazi ipo.
hivi kuna mtu anajua nini maana ya kile chuo cha Mwalimu Nyerere Magogoni.? maana tunachagua tu viongozi sababu ya ushabiki, sasa hawa mnaowashabikia mfano Sugu, Kalapina, Maji marefu na wengine wengi wataenda kufanya nini bungeni.? wengine shuleni walikuwa vilaza, km kweli tunataka kuwa na mapinduzi ya ukweli lazima tuwaandae viongozi wetu lasivyo tutakuwa tunaruka mkojo tunakanyaga mavi.
 
Profesa Maji Marefu ni Mganga wa Kienyeji, darasa halijui=mbumbu, yeye na Shekhe Yahya ni sawasawa. Kama nayeye amekuwa mbunge basi ni balaa bunge litalipuka kwa uchawi huko.
Kwa kifupi ni Profesa wa kujiita mwenyewe kwa kufanya mambo ya nguvu za kiza. Binafasi siamini kama amekuwa mbunge,

:glasses-nerdy:lazima waipate fresh bungeni uchawi umeingia
 
izi TV zetu vilaza sana,wako wapi sasa kutangaza?
Hizi siyo tv ni video ambayo hadi ukaweke mkanda kwenye deki hakuna cha live wala nini.
wanatutangazia yale tunayoyajua tayari. Yaani hatuna tv kabisa, NEC CCM, Vyombo vya habari sawa tu
 
Utendaji kazi uko hoi hivyo hivyo sehemu nyingi. Wamezoea. Hupati huduma ati mtu kenda kunywa chai ama hakuna hata sababu za maana zinazotokea wakati watu wanasubiri huduma. Aibu kabisa kufanya hayo hayo hata kwenye suala nyeti kama kutoa matokea. Watu wamezunguka vituo kutaka matokeo yatangazwe, ati wahusika wanakwenda kunywa chai!!!!!! Huu uozo mwisho wake lini??????
 
Back
Top Bottom