Elections 2010 [NOT CONFIRMED]: Prof. Mlambiti (wa Uchumi SUA) naye ashinda Ulanga

MTWA

JF-Expert Member
Aug 5, 2009
1,166
166
Ni taarifa ninazopata sasa kutoka kwa mwenyeji wa Ulanga kuwa Professor Mkongwe wa Uchumi, na Mhadhiri wa vyuo vya Makerere na Sua ameshinda kwa kishido huko Ulanga.

Hii ni hazina kubwa sana kwa chadema kujenga misingi imara kwa mwaka 2015 na zaidi
Tafadhali tuwatumie kujijenga baada ya ushindi huu mkubwa katika historia ya Tanzania
 
Wabunge wengi wa chadema ni dalili ya ukombozi. Waliopo Butiama lazima wataona kaburi la Nyerere likitikisika ikiwa ni dalili ya furaha.
 
Prof Mlambiti mzee wa Agricultural economics amekuwa mpambanaji wa siku nyingi na waziwazi. Kama kweli basi kweli subira avuta heri. Peoples power
 
Bado natafuta data kamili lakini waliopo huko wanaweza pia kunisaidia.
Ila hizi tetesi ni kutoka reputable site ya mtu wa huko kuwa ni uhakika
 
Hatimaye Prof. kakamata jimbo! tutegemee mengi sana kutoka kwa huyu mtu, hana tofauti sana na Slaa
 
Hii ni hazina kubwa sana kwa chadema kujenga misingi imara kwa mwaka 2015 na zaidi
Tafadhali tuwatumie kujijenga baada ya ushindi huu mkubwa katika historia ya Tanzania

Sura ya baraza la mawaziri la Dr. Slaa linaanza kuchukua sura.............huyu professa wizara ya kilimo ndiyo itamfaa...........halinganishwi na "TYSON: hata siku moja..............kama ubabaishaji wa JK ulivyoonyesha.........
 
Ni taarifa ninazopata sasa kutoka kwa mwenyeji wa Ulanga kuwa Professor Mkongwe wa Uchumi, na Mhadhiri wa vyuo vya Makerere na Sua ameshinda kwa kishido huko Ulanga.

Hii ni hazina kubwa sana kwa chadema kujenga misingi imara kwa mwaka 2015 na zaidi
Tafadhali tuwatumie kujijenga baada ya ushindi huu mkubwa katika historia ya Tanzania

Nina furaha isiyo na kifani, sio tu kushinda CHADEMA bali huyu Prof. mkongwe wangu ninayemheshimu maana amenilea nikiwa nachukua BSc hapo SUA ni Prof makini sana mwenye kujali maslahi ya taifa na ni mpambanaji, infact, he deserves it!
 
Great news! The truth will always stand no matter how long it takes
 
no datz no right to write
Usijali sana tuahamasika sana na hawa watu wa mhimu sana kama Prof. wa ukweli kabisa kutoka katika roho ya uchumi!. Hatuna uhaba wa wasomi wa ukweli kutoka Chadema sasa.
 
Nina furaha isiyo na kifani, sio tu kushinda CHADEMA bali huyu Prof. mkongwe wangu ninayemheshimu maana amenilea nikiwa nachukua BSc hapo SUA ni Prof makini sana mwenye kujali maslahi ya taifa na ni mpambanaji, infact, he deserves it!
nakwambia kwa waliosoma uchumi Sua basi hakuna mtu asiyemkubali Professor.
Yule ni hazina kubwa sana tena iliyosahauliwa siku nyingi
Sipati picha ya hilo Bunge la mwaka huu.

Labda Chadema wenyewe ndo tushinde urais, au kama ccm, basi waache ubabaishaji la sivyo Dodoma patachimbika!!
 
nilisikia kwenye taarifa za uchaguzi ch10 japo ilikuwa almost 2400. Kama ni kweli basi prof Kahigi wa Bukombe na Mlambiti wakiwa BUNGENI naamini japo pengo la SLAA ni gumu kuzibika lakini NEW ÅND PROMISSING REVOLUTION IS BEFORE US.
 
Hivyo vichwa acheni viingie Mjengini Dr. Slaa mwenyewe si ataendelea na kazi huku nje!
lakini shughuli za hawa maprof si ndogo!
Huwa hawaruhusu ujinga upite kabisa

mwaka huu waziri akipewa lazima afikirie mara mbili
 
prof. Mlambiti wa chadema ndie mshindi na kinachosubiriwa ni nec ulanga kumtangaza, tarafa za malinyi na ngoheranga historically ndio ngome thabiti za ccm lakini 2010 wameamua kuchagua mtu na siyo chama, msingi wa taarifa yangu jamvini unategemea fact hizi.

tarafa za ngoheranga na malinyi zina kata tano katika hizo tano ccm wameshinda 4 na chadema 1 hiyo ni udiwani, kwenye ubunge kura 75 % zote zimeenda chadema, maana prof ameshinda almost 99 polling station za tarafa hizi isipokuwa vijiji vya ihowanja na mbalinyi. Hapa ameshinda sana kwa sababu ya majeraha ya kura za maoni hususani vijana waliojitokeza kumuangusha dkt.ngasongwa baada ya wao nao kuchakachuliwa na tabibu mponda kwa nguvu ya celina kombani na ccm wilaya wakaiasi ccm na kumpigia debe prof. Mlambiti, kosa lingine ni kitendo cha mgombea wa ccm tabibu hadji mponda ni kuitenga na kuidharirisha kambi ya ngasongwa ktk kampeni zake kwa imani kuwa yassin njayagha na simon ngonyani watamsaidia hali ikawa ni tofauti sana maana hao aliowategemea ndio waliotuma majeshi ya kummaliza. Alisituka kuitafuta shuka alfajiri kuwa jamaa wanammaliza tena baada ya ujio wa kingunge jimboni aliyeagiza wagombea wote ktk kura za maoni warudi jimboni na kumtaka dkt ngasongwa akaokoe jahazi, bahati mbaya dkt ngasongwa akiwa ktk safari ya kuitikia wito akapata ajali njiani na kumfanya kukosa sehemu kubwa ya kampeni za lala salama ingawaje ndio aliwaokoa madiwani wa ngoheranga, biro na ihowanja. Dakika za lala salama ccm waliliona tatizo na kuwataka njaygha na ngonyani wakasafishe sumu walioipanda jimboni kama wasemavyo waswahili siku ya kufa nyani vijana hao wakiwa ktk gari moja walipata ajali sehemu ileile ambayo dkt ngasongwa alipatwa na ajali na kujikuta wanarudi mjini ifakara kwa matibabu na kumuacha tabibi hadji mponda akipata sapoti toka kwa alhaj ngasongwa ili kuirejesha malinyi ccm.

tarafa ya mtimbira takwimu zaonyesha kuna kata 6 katika hizo chadema ameshinda mbili lakini kura za ubunge zimegawanyika 55% ccm na 45 chadema, hii imetokana na uzawa wa wagombea wote wawili, wote wanatoka tarafa hiyo na ni wapogoro vidabagha tabibu hadji mponda kwa mtimbira yeye ni mhamiaji lakini prof ni mzawa halisi wa mtimbira, kinachosumbua hapa ni wanamtimbira kuwekwa njia panda ila advantage imekwenda kwa prof.mlambiti na chadema, tarafa ya lupiro kuna kata tano chadema wamezinyakua 2, katika ubunge kura zimegawanyika kwa 55 chadema na ccm 45, hii imetokana na majeruhi wa kura za maoni ccm ndg njayagha ambaye ni mzaliwa wa lupiro kumuunga mkono prof.mlambiti .

mtaji mkubwa hapa ni kura za maoni ndani ya ccm, uongozi wa ccm mkoa na wilaya ulielekeza nguvu ya kumng'oa hasimu wao mkuu dkt ngasongwa wakiamini kuwa tatizo lao ulanga magh ni ngasongwa wakasahau kura jimboni humo ni za mtu si chama. Katibu wa ccm alikula 5m toka mgombea wa ccm anayeshindwa uchaguzi sasa na kijana ngonyani na mkiti alikula mzigo kwa wagombea wa udiwani karibu wote ++yassin njayagha.
kwa msingi huo prof.mlambiti ndio chaguo la ulanga magharibi 201-15.

ktk hali hii ccm ulanga 2012 inatakiwa ifanyiwe overhaul halisi kuelekea 2015,ccm tujipange upya 2015.
 
Back
Top Bottom