Norwegian oil and gas company "Equinor" ipo matatani kufungasha virago vyake

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,944
18,653
Norwegian oil and gas company Equinor inayofanya uzalishaji wa Gasi toka 2007 hapa Tanzania, sasa imeamua kupunguza uwekezaji wake Tanzania katika uzalishaji wa Gasi.

Ijumaa iliyopita, msemaji wa Equinor ASA’s Internation, bwana Erik Haaland, aliliambia gazeti la The citizeni kuwa, mradi wa uzalishaji gesi (Tanzania Liquefied Natural Gas LNG) umekuwa ukiendeshwa kwa hasara hivyo basi management imeamua kupunguza uwekezaji huku akitumia msemo wa kiuchumi kuwa ni " Reducing annual balance sheet value". Hii kwa maelezo mepesi ni kuwa, kampuni imeamua kupunguza madeni yake hivyo basi itabidi baadhi ya assets za kampuni ziuzwe kufidia meadeni.

Hata ivyo, serikali ya Tanzania imesistiza kuwa, haikuwa imefahamishwa juu ya hatua izo maana haikuwa imepata ufafanuzi rasmi kutoka kwenye management ya kampuni.

Hata hivyo huu mradi umekuwa katika mgogoro na serikali toka 2019. Huku wawekezaji wakitaka mradi usiendelee mpaka ionekane utaweza leta faida kiuchumi.

Donath Olomi ambaye ni Mbobezi wa mambo ya Uchumi na ni CEO wa Institute of Management and Entrepreneurship Development (IMED) alijaribu kueleza kuwa sababu kubwa ya uamuzi huo, inatokana na kushuka kwa bei ya Mafuta na Gas katika soko la dunia pamoja na Mazingira yasiyokuwa Rafiki katika uwekezaji hasa mabadiliko katika Production Sharing Agreements (PSAs) hapa Tanzanua.

Source: The citizen 31/1/21

lng-pix-data.jpg
 
Yaani sasa tumefikia hatua hii!

1. Hatulindi mazingira mazuri ya uwekezaji,

2. Soko la dunia huwa bei inapanda na kushuka na ni kawaida.

3. Tatizo lipo ndani ya utendaji wetu kama nchi, taasisi zetu zilinde wafanyabiashara na walipa kodi ili waendelee kuwepo,tumejisahau tunatoa matamko ya kisiasa kulinda wamachinga kwa vile ni wananchi wanyonge na kusahau kundi la wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji.

4. Sasa kama nchi malengo ya ukusanyaji mapato kupitia kodi na tozo tutaweza kuyafikia?!

5. Wizara ya viwanda na biashara ikae na wadau wengine kama wizara ya fedha, Kituo cha uwekezaji,chama cha wenye viwanda na wawe na utaratibu wa kukutana mara kwa mara kujadili na kutafuta suluhu ya changamoto zinazojitokeza. Serikali kukaa kimya sio ujanja!
 
Wafanyakazi wa umma au serikali na taasisi zake sio wabunifu, ubunifu wanaojuwa wao ni kufungia kwa kuzani wanamkomoa tajiri, ila kwenye kuomba increment wanaongoza
 
Inetegemea hayo mazingira mazuri wanayosema ni yapi isijekuwa tu wao wanataka wanufaike tu sisi tusipate chochote wakati mali ni yetu.

Kama vipi wasepe tu maana gesi sio maandazi useme yataoza.

Tunaweza subiri ufiki wakati muafaka au aje muwekezaji atayekubaliana na terms zetu.
 
Lakini tutumikie wakati uliopo kutengeneza mazingira ya kukuza na kujenga uchumi, kusubiri wakati ujao ni kukosa mbinu na maarifa ya kukabiliana na mazingira ya sasa!!
Tuamke,tuwe wa kwa kwanza kujua na kubaini mbinu za kuwazidi na kufanikishi mipango ya kukuza na kuimarisha uchumi kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo!!!
 
Yaani sasa tumefikia hatua hii!

1. Hatulindi mazingira mazuri ya uwekezaji,

2. Soko la dunia huwa bei inapanda na kushuka na ni kawaida.

3. Tatizo lipo ndani ya utendaji wetu kama nchi, taasisi zetu zilinde wafanyabiashara na walipa kodi ili waendelee kuwepo,tumejisahau tunatoa matamko ya kisiasa kulinda wamachinga kwa vile ni wananchi wanyonge na kusahau kundi la wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji.

4. Sasa kama nchi malengo ya ukusanyaji mapato kupitia kodi na tozo tutaweza kuyafikia?!

5. Wizara ya viwanda na biashara ikae na wadau wengine kama wizara ya fedha, Kituo cha uwekezaji,chama cha wenye viwanda na wawe na utaratibu wa kukutana mara kwa mara kujadili na kutafuta suluhu ya changamoto zinazojitokeza. Serikali kukaa kimya sio ujanja!
Kushuka kwa bei ya mafuta na gesi kwenye soko la dunia nadhani ndio driving factor....haya matumizi ya alternative source of power ie gari za umeme yatabadilisha mambo mengi sana
 
Lakini tutumikie wakati uliopo kutengeneza mazingira ya kukuza na kujenga uchumi, kusubiri wakati ujao ni kukosa mbinu na maarifa ya kukabiliana na mazingira ya sasa!!
Tuamke,tuwe wa kwa kwanza kujua na kubaini mbinu za kuwazidi na kufanikishi mipango ya kukuza na kuimarisha uchumi kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo!!!
Vijana wengi tu wamesoma hiyo Oil and Gas eventually tutapata technology ama right partners ,

Tusiwe watumwa wa mali zetu au kuingia katika mikataba ya kinyonyaji kisa tunataka kunufaika sasa.

Oil ipo Gas ipo tu, na haiharibiki kama mazao hivyo nashauri tufanye mambo sahihi tusiwe under pressure yeyote.
 
Inetegemea hayo mazingira mazuri wanayosema ni yapi isijekuwa tu wao wanataka wanufaike tu sisi tusipate chochote wakati mali ni yetu.

Kama vipi wasepe tu maana gesi sio maandazi useme yataoza.

Tunaweza subiri ufiki wakati muafaka au aje muwekezaji atayekubaliana na terms zetu.
Shuda inakuja kwenye sheria mpya za uwekezaji wakati kipindi wanakuja walisign mikataba iliyokuwa inafata sheria za zamani.
 
Mahakama inatambua haki ya nchi kubadili sheria zake, hilo halikwepeki Ila kama waliingia makubaliano kwamba mabadiliko ya sheria hayataathiri mikataba iliyokwisha ingiwa hilo litakuwa jambo jingine.
 
Back
Top Bottom