Norway: Mauzo ya magari ya umeme yapiku yale yatumiayo petroli na dizeli

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
613
1,776
electric-cars-being-charged-on-a-street-in.jpg


Mauzo ya magari yanayotumia umeme yafikia 54% ya mauzo ya magari yote mapya huko nchini Norway, ikiwa ni mara ya kwanza kwa nchi hiyo kurekodi mauzo ya juu ya magari hayo dhidi ya yale yatumiayo dizeli na petroli.

Serikali ya Norway ina mpango wa kukataza mauzo ya magari yatumiayo petroli na dizeli ifikapo mwaka 2025, ambapo tayari imeanza mikakati ya kupunguza kodi ili kuhamasisha utengenezwaji wa magari ya umeme kwa wingi.

Kwa mwaka 2020 mauzo ya magari ya umeme yamefikia 54% ya magari yote mapya ya abiria, ikiwa ni ongezeko la kutoka 49% mwaka 2019.

Hata hivyo, mwezi Desemba umerekodi mauzo ya juu zaidi ya magari kwani zaidi ya magari mapya 20,000 yalisajiliwa, ambapo 66%.7 yalikuwa magari yatumiayo umeme na yapatayo 4,232 yalikuwa ni aina ya Tesla Model 3, ikiwa ni zaidi ya 20% ya mauzo yote ya magari kwa mwezi huo.

======

Electric car sales jumped to a record 54% of all new-vehicle sales in Norway last year, but Tesla’s Model 3 lost its place as the country’s bestselling vehicle despite a late surge.

It is the first time a country has recorded more sales of electric cars than those powered by petrol, diesel and hybrid engines over an entire year.

The Norwegian government plans to ban the sale of petrol and diesel cars by 2025, and has used incentives and tax breaks in recent years to encourage an electric-car boom.

Battery-electric vehicles (BEVs) made up 54.3% of new passenger car sales in 2020, up from 42% in 2019, according to figures published by the Norwegian Road Federation (OFV) on Tuesday.

December was a bumper month for car sales in the Nordic country — the best on record — as more than 20,000 new vehicles were registered. Of these, 66.7% were electric vehicles and 4,232 were Tesla Model 3s — more than 20% of all vehicle sales in the month.

However, Tesla’s TSLA, +1.02% popular midsize model — the bestselling car in Norway in 2019 — fell to second place in 2020, losing out to Volkswagen’s VOW, +0.18% Audi e-tron with Volkswagen’s ID.3 in third.

Following a record year for Tesla in Norway in 2019, the U.S. company faced stiffer competition in 2020 as its rivals launched a number of electric cars, while the COVID-19 pandemic also affected sales.

December saw something of a comeback, with Tesla selling 4,232 cars — 54% of its annual 7,770 total. The company is also set to launch its Model Y electric SUV in Norway later this year, Reuters reported.

Source: MarketWatch
 
Tuwapongeze kwa kujua na kujali mazingira

Ila sisi ambao hatujamilik Gari tokea Hapo tunasubr mpunguze Bei wa dunia ya Mwisho Tumiliki.
 
Tanzania hata sheria haijabadilishwa kuruhusu magari ya umeme kutambulika nchini. hata kwenye calculator ya TRA option haimo. nadhan tunaisubiri mitumba ya ulaya ya petrol na diesel. range rover, bently, merc, vw, bmw, n.k watutupie!
 
Kwani mkuu ukitaka kuingiza hapa nchini gari la umeme unakatazwa?
NDIO. halitambuliki kama chombo cha usafiri kinachoweza kusajiriwa na TRA kwa sheria za nchi yetu. labda upate special clearance. sasa kama una mpango wa kuagiza tesla hakikisha hunaga presha, mana hakatok bandarin!
 
Waarabu na mafuta yao watafute kazi nyingine za kufanya.
Sijui kwa nini sikuzaliwa na rais wetu Dr John Joe! ningekuwa nasubiri tuko karagwe kuangalia ng'ombe wetu namuuliza .. baba kwanini shilingi yetu nyingi inayoenda nje kuagiza mafuta usiruhusu magari ya kuchaji? kwanini tusimiliki gesi na magari ya gesi tukauza na kwa jiran ili uwe na nguvu kama Iran?

Alafu kwenye kodi namwambia. Tata kwanini wanaopangisha nyumba mtaani hawalipi kodi iliyopo kisheria na ni pesa nyingi?
 
NDIO. halitambuliki kama chombo cha usafiri kinachoweza kusajiriwa na TRA kwa sheria za nchi yetu. labda upate special clearance. sasa kama una mpango wa kuagiza tesla hakikisha hunaga presha, mana hakatok bandarin!
Mo Dewji Mbona ana Tesla au kalifanya toi.
 
Hao Norway wanachimba mafuta, pia licha ya teknolojia waliyonayo hawatengenezi gari ya aina yoyote hata muundo wa kirikuu.

Norway na Dubai hawachekani Maana wote ni wanunuzi wa magari waliyotengeneza wenzao.
 
haya mambo ya mitandaon huwa nakuwa wa mwisho kuamini.. kwani rolls royse hii ya diamond mil 800 iko madale!

Yaani wewe unamlinganisha Diamond na Mo 😂😂😂😂😂 ,wewe endelea kuwa wa Mwisho kuamini lkn Mo Dewji ana Tesla.
 
Yaani wewe unamlinganisha Diamond na Mo 😂😂😂😂😂 ,wewe endelea kuwa wa Mwisho kuamini lkn Mo Dewji ana Tesla.
Dewij alikua anawapa ujumbe waliomteka kuwa bado ana mkwanja hata kama walimtoa upepo wa kutosha. Kumbuka hii ilitangazwa wiki chache baada ya tukio la kutekwa.
 
Back
Top Bottom