Norway kazi za risk zina pesa nyingi, tusiogope risk katika maisha

Per Diem

JF-Expert Member
Mar 28, 2018
2,191
3,711
Nimeona watu wengi sana wakiogopa kazi ambazo ni risk. Lakini wanashindwa kuelewa kuwa kazi ambazo zina risk kubwa ndio zenye pesa nyingi.

Simaanishi huku Norway kazi ambazo hazina risk hazina pesa, hapana. Kwanza kazi zenye pesa ni zile za wale skilled ambazo kwa mhamiaji huwezi kupata kirahisi au huwezi kupata kabisa.

Hapa ninamaanisha kazi zile za unskilled ambazo ndio hizo kwa ajili yetu sisi wahamiaji. Na ndio hizo ambazo wenyeji hawazipendi hata kidogo, maana kuna sehemu wataenda kufanya kazi kwa urahisi na kupata pesa nyingi tu.

Huku kuna kampuni ambazo wanachukua tender ya kuwafanyia makampuni mengine kazi ikiwemo za service na ku-handle mizigo yao mikubwa bandarini. Hapo kwenye service pia kuna mambo ya usafi wa machines.

Sasa kwenye hizi kazi watu kama sisi ndio huwa tunaingia na tunafanya kweli kiasi kwamba hata siku nyingine ikitokea wana kazi hawaachi kukuita.

Ilitokea kuna kazi ya kupanda juu ya crane ni risk Sana Ila wala sikusita nikapanda fasta tu na overall yangu sina wasiwasi kabisa ikiwa wao wanaona wasiwasi sana (nimeweka picha)

Kikawaida kazi nazofanya za huku bandarini huwa ninachukua 32000 kwa saa moja, Ila hii nilichukua 60000 kwa saa na kwa siku moja nilikuwa nafanya kwa masaa 18.

Kwa hesabu ya kawaida kwa siku inakuwa ni 60000×18 = 1,080,000, kazi kama hii ukifanya kwa wiki bila kuchoka una uhakika wa si chini ya milion 7. Ila haiwezi kufika wiki sana sana ni siku 3 au 4.

Hizi zingine ndio uhakika wa kila siku.

Kuna siku baada ya kumaliza kazi flani nikapata nyingine usiku ya kufanya usafi kwenye meli kubwa iliyokuwa imekuja.

Kwa kifupi ukiwa sehemu yoyote ugenini usibague kazi kama wafanyavyo wenyeji.

Mfano unatoka dar kwenda kutafuta maisha iringa, ukifika iringa jiepushe sana kubagua kazi, kazi yoyote halali na ambayo haitwezi utu wako ifanye.

Hivyo natoa hamasa na moyo kwa vijana wenzangu kutochagua kazi hata kama ina risk kubwa. Maisha Ni mapambano, siku nikirudi kila mtu atahisi huko nilipo mimi ni meneja kumbe.

Niliamua kuchagua haya maisha na sio Slsiri na-enjoy sana.

Tufanye kweli tuache kuwa watu wa lawama.

IMG_20210605_093424_390.jpg
IMG_20210605_095535_422.jpg
IMG_20210605_174232_540.jpg
IMG_20210605_183245_670.jpg
IMG_20210604_142540_073.jpg
IMG_20210604_144622_126.jpg
IMG_20210604_152235_190.jpg
IMG_20210604_191525_220.jpg
 
Roho mbaya inakuja vipi Bro!
Acheni upuuzi wenu
Vijana wengi waliozamia huko Ulaya utawasikia wakihadithia namna wanavyopiga pesa ndefu kwa kufanyakazi za hovyo hovyo.
Lakini sasa ukiwaambia wakupe "mchongo" ili na wewe uzamie wanakataa. Hiyo ndiyo roho mbaya sasa.

Kama "ramani" inasomeka kwanini usiwapigie mapande na wenzako ili nao waje wapambane?
 
Kuna mshkaj wangu yuko Estonia apo (Mzungu alishakuja bongo akakaa kwangu) ,mishe zake anafanya btn Norway na Estonia, hua ananishawish nije kuchek mishe uko .... Vp unakuelewa kulivyo uko chief? Watu wa Estonia hawana issue ya ubaguz? Economy ikoje?
Aisee....
 
Back
Top Bottom